Wanawake wanaojihusisha
na shughuli za uvuvi wametakiwa kuwa
wabunifu ikiwa ni pamoja na kujengeana uwezo Ili kukuza biashara zao huku
wakikumbushwa kujilinda dhidi ya
maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi.
Ushauri huo umetolewa (24.06.2021) na Afisa Maendeleo ya Jamii
Mkoa wa Mara, Bi. Neema Ibamba katika warsha ya siku tatu ya wadau hao Mjini
Musoma Mkoani Mara.
Ibamba amesema kuwa biashara yoyote inahitaji ubunifu na kwamba wadau hao kutoka Mikoa ya Kanda ya
ziwa lazima waende na wakati.
Aliongeza kuwa ubunifu
unaotakiwa ni pamoja na kuwa na vifungashio vizuri vya kisasa kwa ajili ya bidhaa zao pamoja na
kuangalia fursa nyingine za masoko zinazowagusa.
Aidha katika kukuza kipato
cha familia, Ibamba amewataka wanawake kuendelea kushirikiana na waume zao
badala ya kuwadharau kutokana na kipato wanachopata.
"Biashara ama kupata
kipato kisiwe kigezo cha kufanya dharau kwa wanaume wenu kwa kuwa mna pesa,
hakikisheni kile mnachokipata mnakiweka mezani ili kiwasaidie," alisema
Ibamba.
Aidha Ibamba amewataka
wanawake hao kujua mbinu mbalimbali za kuweza kujikinga na maambukizi ya
ugonjwa wa Ukimwi hususani katika mialo ya kuuzia samaki na dagaa na kuwaasa kuendelea kushikamana kwa
umoja wao Ili waweze kupiga hatua kwenye biashara zao kwa sasa na siku zijazo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Usimamizi wa Mazingira na Maendeleo (EMEDO), Bi.Editrudith Lukanga amesema kuwa
ushirikiano ndiyo njia pekee ya kuwafikisha wanawake katika mafanikio.
Lukanga amewataka wanawake
hao kuendelea kushirikiana na waume zao
Ili kulinda ndoa zao badala ya kuwa chanzo cha migogoro katika ndoa hizo.
Ameongeza kuwa shirika lao
limekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha Umoja wa Wanawake wanaojihusisha na
Uvuvi (TAWFA) unazidi kuimarika na kuhusisha kundi kubwa.
Kwa upande wake, Afisa
Uvuvi Mwandamizi ambaye pia ni mratibu wa dawati la jinsia la Uvuvi la Wizara
kutoka Wizara ya Mifugo na Uvivi, Bi. Upendo Hamidu amesema kuwa Wizara hiyo itahakikisha inaweka
mipango imara Ili kuwasaidia wanawake katika shughuli zao.
Warsha hiyo ya siku tatu
imeandaliwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi
kwa kushirikiana na Shirika la EMEDO na kufanyika mjini Musoma mkoani Mara.
Mgeni
Rasmi ambaye pia ni Afisa Maendeleo ya jamii Mkoa wa Mara, Bi. Neema Ibamba
akiongea na washiriki wa warsha ya wanawake wanaojihusisha na Uvuvi (TAWFA) Kanda
ya ziwa (hawapo pichani) kwenye warsha hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa John
Ludini Mwembeni Complex Musoma. 24/06/2021.
Mteknolojia
wa samaki Mwandamizi, Bw. Masui Munda
akiwasihi washiriki wa washra ya wanawake wanaojihusisha na Uvuvi (TAWFA) Kanda
ya ziwa kushirikiana kwa kushikana
mikono Ili kuweza kupata maendeleo zaidi
Mkoani Mara. (24/06/2021)
Afisa
Uvuvi Mwandamizi na Mratibu wa dawati la jinsia la Uvuvi la WMUV, Bi. Upendo
Hamidu (picha ya juu), Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Usimamizi wa Mazingira
na Maendeleo (EMEDO), Bi. Editrudith Lukanga (kushoto) na Mwenyekiti wa NTT, Mr.
Yahya Mgawe wakiongea na washiriki wa warsha ya wanawake wanaojihusisha na
Uvuvi (TAWFA) hawapo pichani wakati wa warsha hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi
wa John Ludini Mwembeni Complex Musoma. (24/06/2021)
Mgeni
rasmi ambaye pia ni Afisa Maendeleo ya jamii Mkoa wa Mara, Bi. Neema Ibamba (katikati
waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa warsha mara baada ya
warsha ya wanawake wanaojihusisha na Uvuvi (TAWFA) Kanda ya ziwa iliyofanyika
kwenye ukumbi wa John Ludini Mwembeni Complex Musoma (24/06/2021.)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni