MAUAJI YA MKULIMA YAWE MWANZO NA MWISHO, FUATENI SHERIA, WAZIRI MKUU KITETO IKO SALAMA." WAZIRI NDAKI
Na. Edward Kondela Serikali imewataka wakulima na wafugaji wanaofanya shughuli zao kwenye maeneo wasiyoruhusiwa, kuondoka mara moja na kuwataka wafuate sheria, taratibu na kanuni za nchi ambapo wakulima na wafugaji wanatakiwa kuwa kwenye maeneo waliyotengewa kisheria bila kuingiliana. Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki amebainisha hayo (24.01.2021) akiwa katika Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara kutatua mgogoro wa matumizi ya ardhi uliojitokeza hivi karibuni kati ya wakulima na wafugaji katika ukanda wa malisho ya mifugo wa vijiji vya Amei, Loolera, Lesoit na Lembapuri, mgogoro ambao umesababisha kifo cha mkulima Bw. Emelian Malima miaka 45 anayedaiwa kuuwawa na wafugaji (20.01.2021) katika eneo la ukanda wa malisho ya mifugo. Akizungumza na baadhi ya wakulima na wafugaji wanaofanya shughuli zao katika vijiji hivyo, Waziri Ndaki amesema serikali imekuwa ikitenga matumizi bora ya ardhi maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Wilaya ya Kiteto na kwamba maeneo ya wakulima yametengwa kwa ...