Mkurugenzi Msaidizi wa Mazao ya Mifugo, Usalama wa Chakula na Lishe, Bw. Gabriel Bura amewataka wakaguzi wa zao la Ngozi wa Kanda ya Mashariki kusimamia ubora wa Ngozi zinazozalishwa.
Bura
ameyasema hayo leo (12.01.2021) wakati akifungua mafunzo ya siku mbili ya
wakaguzi wa Ngozi wa Kanda ya Mashariki (Dar es Salaam, Pwani na Morogoro)
yanayofanyika katika ukumbi wa Mvuvi House jijini Dar es Salaam.
Wakaguzi
hao wa Ngozi wametakiwa kusimamia uzalishaji wa zao hilo katika hatua zake zote
ili kupata Ngozi zinazofaa kusindikwa katika viwanda.
Aidha,
wakaguzi hao wametakiwa kutumia sheria namba 18 ya mwaka 2008 inayolenga
kuboresha zao la ngozi ili wadau waweze kuzalisha ngozi bora inayokidhi
mahitaji ya viwanda vyetu na hatimaye kuwa na tija ya uzalishaji wa zao hilo.
Bura
amesema uzalishaji wa ngozi za ng’ombe na mbuzi kwa siku ni vipande 31,000
lakini ni asilimia 10 tu ya ngozi zinazopelekwa viwandani hufaa kwa ajili ya
kusindikwa, na asilimia 90 hazifai kutokana na kukosa ubora unaofaa kwa ajili
ya kusindikwa.
“Hivyo
baada ya kupata mafunzo haya ni matarajio ya wizara kuwa mtakwenda kulisimamia
nyema zao hili la Ngozi ili kuhakikisha Ngozi yote inayozalishwa inakuwa bora,”
alisema Bura.
Hapa
nchini vipo viwanda viwili tu vyenye uwezo wa kusindika ngozi hadi hatu ya
mwisho ambavyo ni Moshi Leather Industry chenye uwezo wa kusindika futi za
Mraba elfu 15,000 kwa siku na Himo Tannery and Planter Ltd chenye uwezo wa
kusindika futi za mraba 10,000 kwa siku.
Uwezo
wa usindikaji wa viwanda vyote viwili kwa siku ni sawa na vipande 1000 vya
ngozi ya ng’ombe na 9000 vya ngozi ya mbuzi, hivyo bado kuna uhitaji wa viwanda
vya kusindika Ngozi na vilivyopo kuongeza uwezo wake wa kusindika zao hilo.
Kaimu
Mkurugenzi wa Mazao ya Mifugo, Usalama wa Chakula na Lishe, Bw. Gabriel Bura
(kulia aliyesimama) akifungua mafunzo ya siku mbili ya Wakaguzi wa Ngozi kutoka
Hamashauri na Manispaa za Kanda ya Mashariki (Dar es Salaam, Pwani na Morogoro)
yenye lengo la kuwajengea uwez, yanayofanyika katika ukumbi Mvuvi Huose Jijini
Dar es Salaam (12.01.2021)
Mshiriki
wa Mafunzo ya wakaguzi wa ngozi, Bw. Severine Munishi kutoka Halmashauri ya
Malinyi akichangia mada ya Sheria ya Ngozi katika mafunzo ya kikao cha wakaguzi
wa Ngozi yanayofanyika katika ukumbi wa Mvuvi House Jijini Dar es salaam.
(12.01.2021)
Picha
ya pamoja ya Washiriki wa Mafunzo ya siku mbili ya Wakaguzi wa Ngozi na
Wawezeshaji nje ya Jengo la Mvuvi House Jijini Dar es Salaam. (12.01.2021)
Mtaalam
wa Ngozi Mstaafu, Bw. Emmanuel Muyinga akiwasilisha mada ya Sheria ya Ngozi
namba 18 ya mwaka 2008 kwa Washiriki wa Mafunzo ya Ngozi ya siku Mbili toka
Halmashauri na Manispaa za Kanda ya Mashariki (Dar es Salaam, Pwani na
Morogoro) yaliyofanyika katika ukumbi wa Mvuvi House Jijini Dar es Salaam.
(12.01.2021)
Afisa
Mifugo Mkuu kutoka Idara ya Uzalishaji na Masoko (WMUV), Bw. Edson Kilyenyi
akitoa maelezo mafupi ya kuwakaribisha washiriki wa Mafunzo ya wakaguzi wa
Ngozi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi afungue mafunzo hayo, yanayofanyika
katika ukimbi wa wa Mvuvi House Jijini Dar es Salaam. (12.01.2021)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni