Alhamisi, 24 Septemba 2020
Jumatano, 23 Septemba 2020
Jumanne, 22 Septemba 2020
Jumatatu, 21 Septemba 2020
Alhamisi, 17 Septemba 2020
WATENDAJI WA SHAMBA LA LANGWILA WATAKIWA KUZINGATIA TARATIBU ZA UPANDAJI MALISHO.
Mkufunzi Mkuu wa Mifugo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Kejeri Gilla amesema ni vema kufanya kilimo cha malisho ya mifugo kwa mzunguko katika eneo moja kwa muda usiozidi miaka mitano ili kuzalisha kwa wingi na kupunguza kiwango cha magugu.
Dkt. Gilla alisema hayo
wakati wa ziara ya watumishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye shamba la
malisho la Langwila lililopo mkoani Mbeya walipotembelea kujionea shughuli
zinazoendelea shambani hapo.
"Tusibuni namna ya
kuotesha malisho bali twende kwa utaratibu unaotakiwa na hii itasaidia kupata
muda wa kurutubisha ardhi na kupata malisho yaliyo bora," Alisema Dkt.
Gilla
Hata hivyo Dkt. Gilla amesema
ili kuweza kuwa na mbegu bora ni vyema kuvuna kwa wakati, kuchakata na
kuhifadhiwa vizuri ili kuepuka kuoza kwa mbegu na kuwa na utaratibu wa
kuhakikisha ubora wa mbegu za malisho.
Aidha, alishauri kupitia Idara
ya Uendelezaji wa Malisho na Rasilimali za Vyakula vya Mifugo isaidie
kutengeneza duka la malisho pembezoni mwa Barabara kuu ili kujitangaza na
kusaidia watu kupata huduma kwa ukaribu zaidi na kuweza kuongeza pato la shamba
na taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
Sera na Mipango, Bw. Amos Zephania alisema ili uzalishaji uwe bora na wa tija
ni vyema wafugaji wakapewa elimu ya upandaji na ulimaji wa malisho kwa vitendo
ili kuongeza ufanisi zaidi.
"Tunahitaji kutumia
miundombinu yetu vizuri ili kuweza kujipatia fedha za kuendesha shamba letu kwa
kukodisha matrekta kwa wakulima," Alisema Bw. Zephania
Aliongeza kuwa mikataba ya
kukodisha matrekta kwa wakulima iandaliwe kwa kuonyesha idadi za ekari
zilizokodishwa na kwa kiasi kilichopendekezwa.
"Mashamba yasikodishwe
kwa kufikiria tuu bali ni vyema kuwasiliana, kupata mwongozo na ni vyema pia
Katibu Mkuu Mifugo alifahamu hili ili kuondokana na migogoro isiyo ya lazima,"
Alisisitiza Bw. Zephania
Naye Meneja wa shamba la
Langwila, Bw. Datus Ngerera Alexander aliwashukuru watumishi wa Wizara ya
Mifugo na Uvuvi kwa kufanya ziara shambani kwao na kupokea yale yote waliyofundishwa
na kuelekezwa na kuahidi kuyafanyia kazi kwa wakati.
Kaimu Mkurugenzi wa
Uzalishaji na Masoko kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bw. Steven Michael
akichangia hoja wakati wa ziara ya kutembelea shamba la malisho la Langwila mara
baada ya kutembelea stoo iliyojazwa mbegu za malisho na kushauri kuangalia
namna bora zaidi ya kuhifadhi mbegu hizo. (16.09/2020)
Mkurugenzi wa Manunuzi na Ugavi
kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bw. Emmanuel Mayage akikagua faili la kumbukumbu
ya manunuzi ya vifaa kwenye shamba la malisho ya mifugo Lagwila, mkoani Mbeya
walipotembelea shambani hapo. (16.09.2020)
Afisa Utumishi Mwandamizi
kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bw. Andrew Ponda (katikati) akiwakumbusha
watumishi wa shamba la Langwila juu ya ujazaji wa fomu za opras na umuhimu wake
walipotembelea shamba hilo mkoani Mbeya. (16.09.2020)
Mchumi Mkuu kutoka Wizara ya
Mifugo na Uvuvi, Bw. Ephron Sanga (kushoto) akipata maelezo ya namna ya
kukusanya malisho, kuyafunga kwenye marobota na kuhifadhi kwa ajili ya kuuza.
(16.09.2020)
Kaimu Mkurugenzi wa kituo cha
Utafiti wa Mifugo Uyole, Dkt. Edwin Chang'a (wa nne kutoka kulia) akiwatembeza watumishi
wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika maeneo mbalimbali ya kituo hicho wakati wa ziara
yao mkoani Mbeya. (16.09.2020)
Afisa Mifugo Mkuu kutoka
Wizara ya Mifigo na Uvuvi, Bw. Israel Kilonzo akifungua kikao cha kujadili
namna wanaweza kusaidia shamba la malisho Langwila kufanya vizuri zaidi ikiwa
ni pamoja na ushirikiano baina yao, walipotembelea shamba hilo lililopo mkoani
Mbeya na kuona shughuli zinazoendelea. (16.09/2020)
Watumishi wa Wizara ya Mifugo
na Uvuvi wakiangalia ndama katika eneo lililotengwa kwa ajili ya ndama mara
baada ya kuzaliwa ambapo hupewa huduma na uangalizi wa karibu. (16.09.2020)
Meneja wa shamba la malisho
ya mifugo Langwila, Bw. Datus Ngerera Alexander akieleza namna mashine ya
kukatia nyasi inavyofanya kazi kwa watumishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi
walipotembelea shamba hilo mkoani Mbeya. (16.09.2020)
Mtunza Kumbukumbu Msaidizi
kutoka Wizara ya mifugo na Uvuvi, Bi. Nsia Kileo akichangia mada kwenye kikao
kifupi kilichofanyika kwenye shamba la malisho Langwila mkoani Mbeya. (16.09.2020)
Watumishi kutoka Wizara ya
Mifugo na Uvuvi wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa shamba la mbegu
za malisho ya mifugo Lagwila walipotembelea kujifunza na kujionea mazingira na
shughuli zinazofanywa katika shamba hilo. (16.09.2020)
Kaimu Mkurugenzi wa kituo cha
Utafiti wa Mifugo Uyole, Dkt. Edwin
Peter Chang'a akiongea na watumishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (hawapo
pichani) walipotembelea kituo hicho wakati wa ziara yao mkoani Mbeya. (16.09.2020)
Watumishi wa Wizara ya mifugo
na Uvuvi wakielekea kuangalia jengo kwa ajili ya Kiwanda kidogo cha uchakataji
wa Maziwa ambalo bado lipo kwenye ujenzi kwenye kituo cha Utafiti wa Mifugo
Uyole (TALIRI) mkoani Mbeya. (16.09/2020)
MAFUNZO YA WAPANGA MADARAJA NA WAKAGUZI WA NGOZI YAFANYIKA KWA KANDA YA MASHARIKI
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa
Mazao ya Mifugo na Usalama wa Chakula na Lishe, Bw. Gabriel Bura akifungua
Mafunzo ya Wapanga Madaraja na Wakaguzi wa Ngozi kwa niaba ya Katibu Mkuu
Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Profesa Elisante Ole Gabriel, katika ukumbi
wa Mvuvi House jijini Dar es Salaam. Lengo la Mafunzo hayo ni Kuwajengea uwezo
wa kiutendaji wakaguzi na wapanga madaraja ya Ngozi hapa nchini. (16.09.2020)
Baadhi ya Washiriki wa
Mafunzo ya Wapanga Madaraja na Wakaguzi wa Ngozi Kanda ya Mashariki wakifuatilia
kwa makini hotuba ya ufunguzi iliyokuwa ikitolewa na Mgeni rasmi hayupo katika
picha. Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Mvuvi House jijini Dar es
Salaam leo. (16.09.2020)
Mshauri wa Masuala ya Ngozi
hapa nchini, Bw. Emmanuel Muyinga akichangia hotuba ya ufunguzi wa Mafunzo ya Wapanga
Madaraja na Wakaguzi wa Ngozi yaliyofanyika katika ukumbi wa Mvuvi House jijini
Dar es Salaam. Bw. Muyinga ameipongeza Wizara kwa kufanya maamuzi ya uteuzi na
usajili wa wakaguzi wa Ngozi. (16.09.2020)
Washiriki wa Mafunzo ya
Wapanga Madaraja na Wakaguzi wa Ngozi kutoka Kanda ya Mashariki, Mikoa ya
Morogoro, Pwani, Dar es Salaam na Tanga wakiwa katika Picha ya pamoja na Kaimu
Mkurugenzi Msaidizi wa Mazao ya Mifugo na Usalama wa Chakula na Lishe, Bw. Gabriel
Bura baada ya kumalizika kwa ufunguzi wa mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi
wa Mvuvi House jijini Dar es Salaam leo. (16.09.2020)
Jumatano, 16 Septemba 2020
WARSHA YA KUKUSANYA MAONI YA MAANDALIZI YA MPANGO KAZI WA KITAIFA KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA MWONGOZO WA HIARI WA KUENDELEZA SEKTA YA UVUVI MDOGO NCHINI YAFANYIKA MKOANI KIGOMA.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya
Uvuvi, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Merisia Mparazo akifungua warsha ya
kukusanya maoni ya Maandalizi ya Mpango Kazi wa Kitaifa kwa ajili ya
Utekelezaji wa Mwongozo wa Hiari wa kuendeleza Sekta ya Uvuvi Mdogo nchini kwa
muktadha wa kuhakikisha usalama wa chakula na kupunguza umasikini. Warsha hiyo
imefanyika kwenye ukumbi wa Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) mkoani
Kigoma leo. (16.09.2020).
Mwenyekiti wa Kikosi Kazi cha
Kitaifa cha Maandalizi ya Mpango wa Utekelezaji wa Mwongozo wa Hiari wa
Kuendeleza Sekta ya Uvuvi Mdogo nchini, Alhaj Yahya Mgawe akishiriki kusimamia
zoezi la ukusanyaji wa maoni ya Mpango huo kwenye warsha iliyofanyika kwenye
ukumbi wa Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) mkoani Kigoma leo. (16.09.2020).
Sehemu ya washiriki (wadau wa
sekta ya Uvuvi) wa warsha ya kukusanya maoni ya Maandalizi ya Mpango Kazi wa
Kitaifa kwa ajili ya Utekelezaji wa Mwongozo wa Hiari wa kuendeleza Sekta ya
Uvuvi Mdogo nchini kwa muktadha wa kuhakikisha usalama wa chakula na kupunguza
umasikini wakifuatilia kwa makini maelekezo ya wataalam wa Uvuvi kwenye warsha
iliyofanyika kwenye ukumbi wa Wakala ya Elimu na Mafunzo Uvuvi (FETA) mkoani
Kigoma leo. (16.09.2020).
Afisa Uvuvi kutoka Wizara ya
Mifugo na Uvuvi, Bi. Emanuela Mawoko (mwenye tisheti ya bluu), akisimamia zoezi
la kukusanya maoni ya Maandalizi ya Mpango Kazi wa Kitaifa kwa ajili ya
Utekelezaji wa Mwongozo wa Hiari wa kuendeleza Sekta ya Uvuvi Mdogo nchini kwa
muktadha wa kuhakikisha usalama wa chakula na kupunguza umasikini. Warsha hiyo
imefanyika kwenye ukumbi wa Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) mkoani
Kigoma leo. (16.09.2020).
WATAALAM WA MIFUGO WATAKIWA KUTIMIZA WAJIBU WAO.
Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Hezron Nonga amewasihi watumishi wa umma kuwa wazalendo kwa kutimiza wajibu wao na kuwatia moyo kwamba wapo hapo kwa makusudi ya Mwenyezi Mungu.
Prof. Nonga amesema hayo
katika shamba la kuzalisha mitamba Saohill Mkoani Iringa wakati wa majadiliano
ya namna watakavyoboresha na kufanya shamba hilo kuzalisha zaidi na kupata
mafanikio makubwa.
"Kutotimiza yale mnayopaswa
kufanya ni dhambi kama dhambi zingine na tukiendelea kuwaza hasi hatutakuwa
wazalendo na wala hatutaendelea,” Alisema Prof. Nonga.
Prof. Nonga amesisitiza
kutengenezwa kwa programu nzuri itakayosaidia kujua magonjwa ya mifugo ili
kusaidia kutoeneza magonjwa kwa mifugo mingine na kuwa na utaratibu wa kuchanja
mifugo kila mara.
"Tuwe na mikakati ya
kutambua magonjwa ili kusaidia katika udhibiti wa magonjwa na vifo pamoja na
uongozi mzuri ili kusaidia shamba kuendelea," alisisitiza Prof. Ezron
Nonga.
Kwa upande wake Kaimu
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Masoko kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo),
Bw. Stephen Michael amewataka watumishi hao kujitathmini na kuona ni wapi
wametoka na wanapoelekea katika uzalishaji, uboreshaji na uendelezaji wa shamba
la Saohill na sio kufanya mambo kwa makadirio ambayo husababisha kuendelea kushuka
kwa uzalishaji katika shamba hilo.
Naye Mkurugenzi Msaidizi wa
Utawala na Rasilimali watu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Bw.
Fraksed Mushi amewakumbusha watumishi wa shamba la mitamba Saohill kufuata
sheria, na kusisitiza kuwa likizo ni muhimu na lazima kwa kila mtumishi kwani
ni haki kisheria.
"Likizo za uzazi kwa
mwanamke ni siku 84 na kwa upande wa mwanaume ni siku tano (5)," alimalizia
Bw. Mushi.
Aidha, watumishi katika
shamba la Saohill wamewashukuru watumishi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa
kuwaelimisha na kuwapa uelewa kwenye mambo ambayo walikuwa hawayajui na
kukumbushwa baadhi ya maadili wanayopaswa kuyaishi kwenye utumishi wa umma.
Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo
kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Hezron Nonga awaasa wafanyakazi kuwa
wazalendo na kufanya yale wanayopaswa kufanya kwenye ofisi za shamba la Saohill
walipoenda kutembelea na kujifunza mambo mbalimbali kwenye shamba hilo Mkoani
Iringa. (15.09.2020)
Kaimu Mkurugenzi wa
Uzalishaji na Masoko wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Bw. Steven Michael
akifungua mjadala wa watumishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na
wafanyakazi wengine wa shamba la Saohill kwenye ofisi za shamba hilo Mkoani
Iringa. (15.09.2020)
Watumishi wa Wizara ya Mifugo
na Uvuvi wakiangalia baadhi ya mashine zinazotumika kwenye shamba ya Saohill
kwa ajili ya kukatia, kukusanya na kufunga malisho kwenye karakana ya shamba
hilo Mkoani Iringa. (15.09.2020)
Baadhi ya watumishi wa Wizara
ya mifugo na Uvuvi wakipima uzito wa marobota ya malisho ya mifugo kwa kuyabeba
walipotembelea shamba la Mifugo la Saohill Mkoani Iringa. (15.09.2020)
Baadhi ya malisho ya
Mifugo waliyovunwa na kufungwa kwenye
marobota 1,200 katika shamba la Saohill tayari kwa kubebwa na kwenda kuhifadhiwa.
(15.09.2020)
Mabanda kumi na mbili ya
madume yanayofahamika kama NAIC 2 yenye uwezo wa kuweka madume 24, yapo katika
shamba la Saohill Mufindi Mkoani Iringa. Lengo lilikuwa ni kuhifadhi madume ila
hadi sasa hakuna mfugo wowote unaoishi huko. (15.09.2020)
Jumanne, 15 Septemba 2020
SERIKALI YAZIDI KUWEKA MIKAKATI ILI WAFUGAJI WAWE NA NG’OMBE BORA.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel amesema serikali imelenga kuhakikisha wafugaji nchini wanakuwa na ng’ombe bora, wenye kutoa nyama bora na maziwa mengi wanaopatikana kwa njia ya uhimilishaji (kumpatia ng’ombe mimba kwa njia ya mrija).
Prof. Gabriel amesema hayo
katika Kijiji cha Matebete Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya wakati akizindua
rasmi kambi ya uhimilishaji katika kijiji hicho kwa wafugaji wa jamii ya
kimasai na kuwataka waache kufuga kwa mazoea bali wawe na ng’ombe bora na wenye
tija huku akiwalenga zaidi akinamama nchini kujikita katika ufugaji wa kisasa.
“Haya ni mafanikio makubwa
niwaombe akinamama wengine Tanzania waige mfano wa kina mama wenzano wa jamii
ya kimasai walioamua kufuga kisasa kwa kuwa na ng’ombe bora hatuwezi kuendelea
kwenye ufugaji wa zamani lazima tufuge kisasa na uhimilishaji unafanyika kwa
ng’ombe yeyote hata wa kienyeji.” Amesema Prof. Gabriel
Prof. Gabriel akizungumzia
faida za uhimilishaji amesema njia hiyo ya kumpatia ng’ombe mimba kwa njia ya
mrija ni muhimu katika kuendeleza ubora wa mifugo hiyo ili kutengenzea mbari na
kosaafu bora ya ng’ombe.
Amefafanua kuwa uhimilishaji
ni muhimu kwa kuwa mfugaji anaweza kuchagua ng’ombe anayemtaka na ubora wake
pamoja na kudhibiti magonjwa ya mifugo hiyo kwa ng’ombe dume kupanda ng’ombe
wengi kwa wakati mmoja.
Ili kutoa hamasa kwa wafugaji
wa jamii ya kimasai katika Kijiji cha Matebete kilichopo Wilaya ya Mbarali
Mkoani Mbeya Katibu Mkuu Wizara Mifugo na Uvuvi amesema wafugaji
watakaohimilisha ng’ombe elfu moja wa mwanzo wizara itagharamia kama sehemu ya
uzinduzi na uimarishaji wa kambi za uhimilishaji.
Kwa upande wake Kaimu
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Masoko kutoka Wizara ya Mifugo Bw. Stephen Michael
amesema wizara imekuwa ikifanya kazi karibu na wananchi hali iliyofikia kuweka
kambi ya uhimilishaji katika Kijiji cha Matebete na kuwafanyia ng’ombe vipimo
kabla ya kupandikizwa mbegu.
Naye Afisa Mifugo kutoka
Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Fadhil Chamwazi ameongeza kuwa kambi za
uhimilishaji zina malengo ya kuhamasisha wafugaji kutumia huduma ya
uhimilishaji na kuwajengea uwezo jamii ya wafugaji na wataalam juu ya faida ya
uhimilishaji.
Bw. Chamwazi amesema zoezi
hilo limeanza katika mwaka wa fedha 2019/20 na kwa mwaka 2020/2021
limezinduliwa mkoani Tabora na sasa katika Mkoa wa Mbeya katika Kijiji cha
Matebete na kubainisha kuwa vigezo vinavyoangaliwa kwa ng’ombe kabla ya
kupandikizwa mbegu ya uzazi kwa njia ya mrija, wataalamu wanakagua afya ya
ng’ombe pamoja na kuzingatia umri na muonekano wake.
Nao baadhi ya wafugaji wa
jamii ya kimasai katika kijiji hicho wamefurahishwa na zoezi hilo na kuiomba
serikali kuendelea kuwapatia elimu zaidi na kuwafahamisha namna bora zaidi za
ufugaji wa ng’ombe bora wa kisasa ili waweze kupata matokeo chanya katika
ufugaji wao.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo
na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel akimpongeza mfugaji wa jamii ya
kimasai katika Kijiji cha Matebete Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya, baada ya
ng’ombe wake kufanyiwa vipimo kwa ajili ya kufanyiwa uhimilishaji. (14.09.2020)
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo
na Uvuvi (Mifugo). Prof. Elisante Ole Gabriel (aliyesimama katikati), akiwa na
wasichana wa jamii ya kimasai katika Kijiji cha Matebete Wilaya ya Mbarali,
Mkoani Mbeya waliohitimu masomo kutoka vyuo mbalimbali nchini. Kutoka kulia ni
Bi. Naishiye Eliakimu amehitimu shahada ya ualimu, Bi. Naumu Silomi amehitimu
diploma ya uhandisi wa ndege, Bi. Rahabu Galahenga amehitimu diploma ya sheria
na Bi. Hawa Julius amehitimu diploma ya ualimu. (14.09.2020)
Kaimu Mkurugenzi wa
Uzalishaji na Masoko kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Bw. Stephen
Michael akizungumzia kambi ya uhimilishaji katika Kijiji cha Matebete Wilaya ya
Mbarali, Mkoani Mbeya na namna wizara inayoshirikiana na wananchi ili kuhakikisha
wanapata mifugo bora. (14.09.2020)
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo
na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel (aliyesimama katikati), Kaimu
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Masoko, Bw. Stephen Michael (aliyesimama upande
wake wa kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji wa Malisho na Rasilimali
za Vyakula vya Mifugo, Dkt. Lovince Asimwe (aliyesimama upande wake wa kushoto)
wakiwa wamevalia mavazi ya kabila la kimasai baada ya kupatiwa zawadi na
wafugaji wa Kijiji cha Matebete. (14.09.2020)
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo
na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza na Bi. Rahabu
Galahenga ambaye amehitimu diploma ya sheria. Prof. Gabriel amefika katika
Kijiji cha Matebete kilichopo Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya kwa ajili ya
kuzindua kambi ya uhimilishaji. (14.09.2020)
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo
na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza na wafugaji wa jamii
ya kimasai katika Kijiji cha Matebete kilichopo Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya
wakati wa uzinduzi wa kambi ya uhimilishaji katika kijiji hicho. (14.09.2020)
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo
na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel (aliyevaa miwani) akiwaongoza
wafugaji wa jamii ya kimasai katika Kijiji cha Matebete kilichopo Wilaya ya
Mbarali Mkoani Mbeya kuzindua zoezi la uhimilishaji (kupandikiza ng’ombe mimba
kwa njia ya mrija). (14.09.2020)
WAVUVI WADOGO KUINULIWA KIUCHUMI
Mwenyekiti wa Kikosi kazi cha
Kitaifa cha Uandaaji wa Mpango wa utekelezaji wa Mwongozo wa Hiari wa
kuhakikisha Uvuvi Mdogo Unakuwa Endelevu, Alhaj Yahya Ibrahim Mgawe akitoa neno
la utangulizi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua warsha ya Uandaaji wa
Mpango huo iliyofanyika kwenye Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani
Kigoma. (15.09.2020)
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji, Bw. Ferdinand Filimbi akifungua warsha
ya uandaaji wa Mpango wa utekelezaji wa Mwongozo wa Hiari wa kuhakikisha Uvuvi
Mdogo Unakuwa Endelevu iliyofanyika kwenye Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji
mkoani Kigoma. (15.09.2020)
Bi. Upendo Hamidu
akiwasilisha mada kwenye warsha ya uandaaji wa Mpango wa utekelezaji wa
Mwongozo wa Hiari wa Kuhakikisha Uvuvi Mdogo Unakuwa Endelevu iliyofanyika
kwenye Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma. (15.9.2020)
Baadhi ya washiriki wa warsha
ya uandaaji wa Mpango wa utekelezaji wa Mwongozo wa Hiari wa Kuhakikisha Uvuvi
Mdogo Unakuwa Endelevu wakifuatilia uwasilishwaji wa mada kwenye warsha hiyo
iliyofanyika kwenye Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma.
(15.9.2020)
Kikosi kazi cha kitaifa cha
uandaaji wa Mpango wa utekelezaji wa Mwongozo wa Hiari wa kuhakikisha Uvuvi
Mdogo Unakuwa Endelevu kwenye picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Wizara
ya Mifugo na Uvuvi na Wakuu wa Idara zilizo chini ya Halmashauri ya Manispaa ya
Kigoma Ujiji, Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma, wawakilishi kutoka FETA na Benki
mara baada ya ufunguzi rasmi wa warsha ya ukusanyaji maoni ya utekelezaji wa
Mpango huo iliyofanyika mjini Kigoma.
(15.9.2020)
WATUMISHI WA WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI WATEMBELEA OFISI ZA ZVC, TVLA MKOANI IRINGA.
Watumishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakiongozwa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu, Bw. Zachariyya Kera walifanya ziara ya kutembelea ofisi za Kituo cha Huduma za Mifugo cha Kanda (ZVC) na Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Mkoani Iringa kwa lengo la kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na ofisi hizo.
Akiongea wakati wa ziara hiyo
kwenye ofisi za ZVC na TVLA zilizopo Mkoani Iringa, (14.09.2020), Mkurugenzi wa
Utawala na Rasilimali watu Bw. Zachariyya Kera alitoa ufafanuzi wa mambo
mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwataka wafanyakazi kujua haki zao za msingi na
kufuatilia kwa wakati.
"Watumishi waelimishwe
kuhusu haki zao na wapate stahiki zao kwa wakati," alisema Bw. Kera.
Katika ziara hiyo Watumishi
hao walipata fursa pia ya kutembelea Kiwanda cha Maziwa cha ASAS kilichopo
Mkoani humo na kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa katika kiwanda hicho.
Aidha, watumishi hao wa ZVC
na TAVLA walitumia nafasi hiyo kumueleza Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu
changamoto zinazowakabili ikiwa ni pamoja na upungufu wa watumishi, uhaba wa
Rasilimali fedha na vitendea kazi.
Changamoto nyingine
walizozitaja ni upungufu wa vyumba vya ofisi, upungufu wa mafunzo rejea kwa
Watumishi wa kituo na kukosekana kwa vituo vya kukagulia wanyama.
"Kujengwa kwa machinjio
kubwa ya nguruwe katika mji wa Mbeya katikati ya kanda ya nyanda za juu kusini
kutasaidia kudhibiti magonjwa ya nguruwe katika kanda zingine,"
alisisitiza Bw. Dkt. Jeremiah Choga
Pia, watumishi hao waliiomba
Wizara kuwa na mpango maalum ya utoaji wa mafunzo rejea kwa watumishi kuendana
na kasi ya ukuaji wa sayansi na teknolojia, kuanzisha vituo vya ukaguzi wa
wanyama, mazao ya wanyama na vyakula vya wanyama.
Meneja wa Wakala ya Maabara
ya Veterinari Tanzania (TVLA), Dkt. Qwari Tluway Bura alieleza mpango kazi wao
ikiwa ni pamoja na kusambaza chanjo kwa wafugaji, kutoa mafunzo ya ufugaji bora
wa kuku wa asili, kutanua mtandao wa huduma za Maabara, udhibiti wa minyoo na
magonjwa ya kupe kwa mifugo.
"Tutahamasisha wataalam
wa Mifugo wa vijijini, kata au Wilaya pamoja na wananchi kwa ujumla kuleta
sampuli za kupima ugonjwa wa kichaa cha mbwa katika mikutano ya hadhara,”
Alisisiza Dkt. Bura
Aidha, Viongozi wa ZVC na
TVLA waliishukuru Serikali ya awamu ya tano kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi
kwa kuendelea kuwahudumia wafugaji kwa kuviwezesha vituo kufanya kazi wakati
wote.
Mkurugenzi wa Kiwanda cha
Maziwa cha ASAS Mkoani Iringa, Bw. Fuad Abri akitoa maelezo kwa Watumishi wa
Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuhusu mashine zinavyofanya kazi kwenye Kiwanda hicho.
(14.09.2020)
Mkaguzi na Mdhibiti wa Ubora
kutoka Kiwanda cha Maziwa cha ASAS Mkoani Iringa, Bw. Shadrack Luhwago (kushoto)
akitoa maelezo ya namna wanavyopima ubora wa Maziwa kwenye Kiwanda hicho kwa
Watumishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi walipotembelea Maabara ya Kiwanda hicho.
(14.09.2020)
Mkurugenzi wa Utawala na
Rasilimali Watu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Bw. Zachariyya Kera
(kushoto) akitoa shukrani kwa Mkurugenzi wa shamba la mifugo la Kibebe, Bw.
Richard Philip kwa kukubali kuwapokea na kuwatembeza kwenye shamba hilo na
kuona ufugaji wa kisasa. (14.09.2020)
Mkurugenzi wa Sera na Mipango
kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Bw. Kulwa Zephania (wa tatu kutoka
kushoto) akielekeza jambo nje ya ofisi ya Meneja wa Wakala ya Maabari ya
Veterinari Tanzania (TVLA) Mkoani Iringa walipotembelea kujifunza na kujionea
shughuli zinazoendelea katika ofisi hizo. (14.09.2020)
Mkurugenzi wa shamba la
Kibebe Mkoani Iringa, Bw. Richard Philip (wa kwanza kulia) akiwaonyesha
watumishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi maeneo ya shamba hilo lenye ukubwa wa
hekari 1,200 ambalo lina jumla ya Mifugo 600, wafanyakazi 30, josho, mashine za
kukamulia Maziwa pamoja na sola zinazosaidia katika kuendesha shughuli
zinazoitaji umeme katika shamba hilo. (14.09.2020)
Watumishi wa Wizara ya Mifugo
na Uvuvi wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Kiwanda cha Maziwa cha ASAS
Mkoani Iringa, Bw. Faud Abri walipotembelea Kiwanda hicho. (14.09.2020)
Watumishi wa Wizara ya Mifugo
na Uvuvi wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Kiwanda cha Maziwa cha
ASAS, Bw. Fuad Abri Mara baada ya kutembelea kiwanda hicho kilichopo Mkoani
Iringa. (14.09.2020)
Mkurugenzi wa Manunuzi na
Ugavi, Bw. Emanuel Mayage akiangalia pikipiki pekee ambayo inatumika kwa
shughuli za usafiri, nyingine ikiwa imearibika kwenye ofisi za ZVC Mkoani
Iringa. (14.09.2020)
Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma
za Mifugo, Dkt. Stanford Ndibalema (wa pili kutoka kulia) kutoka Wizara ya
Mifugo na uvuvi (Mifugo) akifafanua jambo kwenye ofisi za Wakala ya Maabara ya
Veterinari Tanzania (TVLA) walipotembelea Mkoani Iringa. (14.09.2020)