Watumishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakiongozwa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu, Bw. Zachariyya Kera walifanya ziara ya kutembelea ofisi za Kituo cha Huduma za Mifugo cha Kanda (ZVC) na Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Mkoani Iringa kwa lengo la kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na ofisi hizo.
Akiongea wakati wa ziara hiyo
kwenye ofisi za ZVC na TVLA zilizopo Mkoani Iringa, (14.09.2020), Mkurugenzi wa
Utawala na Rasilimali watu Bw. Zachariyya Kera alitoa ufafanuzi wa mambo
mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwataka wafanyakazi kujua haki zao za msingi na
kufuatilia kwa wakati.
"Watumishi waelimishwe
kuhusu haki zao na wapate stahiki zao kwa wakati," alisema Bw. Kera.
Katika ziara hiyo Watumishi
hao walipata fursa pia ya kutembelea Kiwanda cha Maziwa cha ASAS kilichopo
Mkoani humo na kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa katika kiwanda hicho.
Aidha, watumishi hao wa ZVC
na TAVLA walitumia nafasi hiyo kumueleza Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu
changamoto zinazowakabili ikiwa ni pamoja na upungufu wa watumishi, uhaba wa
Rasilimali fedha na vitendea kazi.
Changamoto nyingine
walizozitaja ni upungufu wa vyumba vya ofisi, upungufu wa mafunzo rejea kwa
Watumishi wa kituo na kukosekana kwa vituo vya kukagulia wanyama.
"Kujengwa kwa machinjio
kubwa ya nguruwe katika mji wa Mbeya katikati ya kanda ya nyanda za juu kusini
kutasaidia kudhibiti magonjwa ya nguruwe katika kanda zingine,"
alisisitiza Bw. Dkt. Jeremiah Choga
Pia, watumishi hao waliiomba
Wizara kuwa na mpango maalum ya utoaji wa mafunzo rejea kwa watumishi kuendana
na kasi ya ukuaji wa sayansi na teknolojia, kuanzisha vituo vya ukaguzi wa
wanyama, mazao ya wanyama na vyakula vya wanyama.
Meneja wa Wakala ya Maabara
ya Veterinari Tanzania (TVLA), Dkt. Qwari Tluway Bura alieleza mpango kazi wao
ikiwa ni pamoja na kusambaza chanjo kwa wafugaji, kutoa mafunzo ya ufugaji bora
wa kuku wa asili, kutanua mtandao wa huduma za Maabara, udhibiti wa minyoo na
magonjwa ya kupe kwa mifugo.
"Tutahamasisha wataalam
wa Mifugo wa vijijini, kata au Wilaya pamoja na wananchi kwa ujumla kuleta
sampuli za kupima ugonjwa wa kichaa cha mbwa katika mikutano ya hadhara,”
Alisisiza Dkt. Bura
Aidha, Viongozi wa ZVC na
TVLA waliishukuru Serikali ya awamu ya tano kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi
kwa kuendelea kuwahudumia wafugaji kwa kuviwezesha vituo kufanya kazi wakati
wote.
Mkurugenzi wa Kiwanda cha
Maziwa cha ASAS Mkoani Iringa, Bw. Fuad Abri akitoa maelezo kwa Watumishi wa
Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuhusu mashine zinavyofanya kazi kwenye Kiwanda hicho.
(14.09.2020)
Mkaguzi na Mdhibiti wa Ubora
kutoka Kiwanda cha Maziwa cha ASAS Mkoani Iringa, Bw. Shadrack Luhwago (kushoto)
akitoa maelezo ya namna wanavyopima ubora wa Maziwa kwenye Kiwanda hicho kwa
Watumishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi walipotembelea Maabara ya Kiwanda hicho.
(14.09.2020)
Mkurugenzi wa Utawala na
Rasilimali Watu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Bw. Zachariyya Kera
(kushoto) akitoa shukrani kwa Mkurugenzi wa shamba la mifugo la Kibebe, Bw.
Richard Philip kwa kukubali kuwapokea na kuwatembeza kwenye shamba hilo na
kuona ufugaji wa kisasa. (14.09.2020)
Mkurugenzi wa Sera na Mipango
kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Bw. Kulwa Zephania (wa tatu kutoka
kushoto) akielekeza jambo nje ya ofisi ya Meneja wa Wakala ya Maabari ya
Veterinari Tanzania (TVLA) Mkoani Iringa walipotembelea kujifunza na kujionea
shughuli zinazoendelea katika ofisi hizo. (14.09.2020)
Mkurugenzi wa shamba la
Kibebe Mkoani Iringa, Bw. Richard Philip (wa kwanza kulia) akiwaonyesha
watumishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi maeneo ya shamba hilo lenye ukubwa wa
hekari 1,200 ambalo lina jumla ya Mifugo 600, wafanyakazi 30, josho, mashine za
kukamulia Maziwa pamoja na sola zinazosaidia katika kuendesha shughuli
zinazoitaji umeme katika shamba hilo. (14.09.2020)
Watumishi wa Wizara ya Mifugo
na Uvuvi wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Kiwanda cha Maziwa cha ASAS
Mkoani Iringa, Bw. Faud Abri walipotembelea Kiwanda hicho. (14.09.2020)
Watumishi wa Wizara ya Mifugo
na Uvuvi wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Kiwanda cha Maziwa cha
ASAS, Bw. Fuad Abri Mara baada ya kutembelea kiwanda hicho kilichopo Mkoani
Iringa. (14.09.2020)
Mkurugenzi wa Manunuzi na
Ugavi, Bw. Emanuel Mayage akiangalia pikipiki pekee ambayo inatumika kwa
shughuli za usafiri, nyingine ikiwa imearibika kwenye ofisi za ZVC Mkoani
Iringa. (14.09.2020)
Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma
za Mifugo, Dkt. Stanford Ndibalema (wa pili kutoka kulia) kutoka Wizara ya
Mifugo na uvuvi (Mifugo) akifafanua jambo kwenye ofisi za Wakala ya Maabara ya
Veterinari Tanzania (TVLA) walipotembelea Mkoani Iringa. (14.09.2020)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni