WIZARA ya mifugo na
uvuvi, imeandaa mikakati ya kuboresha sekta ya mifugo hapa nchini, moja ya
mkakati huo ni ule wa kudhibiti magonjwa ya mifugo ambapo imewahimiza wafugaji
kuzingataia matumizi ya majosho yenye dawa za kuogesha ng’ombe ili kutokomeza
magonjwa yatokanayo na kupe.
Hayo yalielezwa hivi
karibuni na Naibu Waziri wa mifugo
na uvuvi Mheshimiwa Abdalah Ulega wakati wa zoezi la uhamasishaji wa uogeshaji
wa ng’ombe kanda ya kati mkoani Singida, katika kijiji cha Mgori kilichopo
halmashauri ya wilaya ya Singida vijijini.
Katika uhamasishaji huo waziri Ulega aliwataka wafugaji
kufanya zoezi la uogeshaji wa mifugo uliyoanzishwa uwe wenye tija na endelevu,
kwa vile hivi sasa hakuna sababu za kushindwa kuogesha mifugo yao katika majosho yenye dawa ya
kudhibiti kupe yaliyotolewa na serikali
bure.
Alisema hivi sasa serikali katika zoezi hili, imetoa dawa
bure kwa halmashauri zote nchini, na kukarabati majosho yote yaliyokuwa hayafanyi
kazi, ili wafugaji waweze kuogesha mifugo yao, kukinga ugonjwa hatari
unaoenezewa na kupe, ambao unaoongozwa katika vifo vya ng’ombe hapa nchini.
Hapo, mwanzo shughuli hizo zilikuwa zikifanywa kwa kutofuata
taratibu nzuri za makusanyo yalikuwa yakitoka kwa wafugaji walipokuwa wakipata
huduma za kuogesha mifugo yao, hazikuwa na taarifa ya mapato na matumizi na
hivyo kushindwa kuwa na utaratibu endelevu wa shughuli hiyo, majosho mengi
yalisimama kufanya kazi na mifugo haikugoeshwa.
Katika kampeni hii ya uhamasishaji wa uogeshaji wa mifugo,
tozo imepunguzwa ambapo hivi sasa kila ng’ombe anaogeshwa katika majoshi ni shilingi
50 tu, huku nyuma uogeshaji ulikuwa unatozwa wastani wa shilling mia 200 kwa
kila ng’ombe na kwa mbuzi ilikuwa shililngi 10.
“nyie wafugaji msikalie rasilimali hii ya mifugo mliokuwa
mnayo, kwani ni uchumi mkubwa sana mliyokuwa nayo kwenu na pia kwa Taifa ili
kuongeza mapato, yanayotokana na mifugo yenu” alisema mheshimiwa Ulega.
Aidha alifafanua kuwa ufugaji kwa kufuata taratibu za ufugaji
wa kisasa na kibiahsra kwa kuvuna mifugo inapozidi katika eneo uliyokuwa nayo,
itakusaidia kupata kipato katika kuboresha maisha yako na ya familia. Uhamasishaji huu unafuatia uzinduzi wa
kampeni ya uogeshaji wa mifugo, iliyofanywa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mh.
Luhaga Mpina katika kijiji cha
Buzirayombo Halmashauri ya Chato Mkoa wa Geita.
Naibu Waziri Wa Mifugo Na Uvuvi Mh. Abdallah Ulega, katikati mwenye shati la rangi ya bluu akiandaa dawa ya josho ili kuogesha mifugo |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni