KATIBU MKUU WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI DKT MARIA MASHINGO AFANYA ZIARA KATIKA MKOA WA RUVUMA.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Sekta ya mifugo) Dkt Maria Mashingo leo amefanya ziara katika Halmashauri ya Wilaya ya Madaba mkoani Ruvuma.
Mashingo amefanya ziara hiyo ikiwa ni m wendelezo wa ziara yake ya Mikoa minne aliyoanzia Mbeya,Njombe na sasa Ruvuma,lengo ikiwa ni kujua kama mikoa hiyo inamifugo kutoka nchi jirani iliyoingia kinyume cha sheria.
Katika ziara yake hiyo kila alipopita Dr Maria Mashingo alisisitiza kila mkoa na halmashauri zake zote kuhakikisha wanapiga chapa mifugo yote hususani ng'ombe ili ifikapo Disemba 17 mifugo yote iwe imepigwa chapa.
Akitoa taarifa fupi ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba kwa Katibu Mkuu,Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bw.Shafi Mpenda amemweleza Katibu mkuu kuwa wao walijiwekea utaratibu wa kuzuia mifugo kuingia katika Wilaya yao mifugo yote isiyokuwa na kibali pale mpakani mwa Njombe na Ruvuma (Igawisenga).
"Tumeimarisha sana ukaguzi hapa mpakani,Hakuna mifugo inayoingia katika wilayani hii bila kibali,na wengine tumekuwa tunawarudisha na mifugo yao huko huko walikotoka."
Alisisitiza "Kimsingi Hakuna mifugo inayoingia kutoka nchi jirani,changamoto tuliyonayo ni mifugo kutoka mikoa mingine ya Tanzania."
Katika hatua nyingine Katibu Mkuu Mifugo ametembelea shamba la Hanga Ngadinda la Mifugo,Kiwanda kidogo cha kusindika Maziwa na kituo cha kuzalisha Vifaranga vya samaki cha Ruhila Aquaculture Development Centre kilichopo Songea Mjini
Akimweleza katibu mkuu kero zinazojitokeza katika shamba la mifugo la Hanga-Ngadinda Bw.Cornel Kapinga Katibu wa chama cha Wafugaji kanda ya Kusini (CCWT) amesema kuwa Wakulima wanaingia katika Vitalu vya wafugaji na kulima mazao ya chakula hatimaye husababisha Migogoro ya wakulima na Wafugaji.
"Hili shamba ni kwa ajili ya wafugaji lakini wakulima wanaingia na kulima mazao ya chakula"alisema Kapinga.
Pia Bw. Kapinga alimweleza Katibu mkuu baadhi ya kero wanazokumbana nazo katika shamba hilo kuwa ni pamoja na Miundombinu ya Maji kuwa ni shida kubwa shambani hapo,Kodi kubwa kulipia vitalu na aliomba wafugaji wamilikishwe hivyo vitalu ili waweze kuviendeleza.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Songea Mhe. Palolet Mgema amesema kuwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi imekuwa ikilalamikiwa kuwa haifanyi kazi yake Ipasavyo,hayo yamedhihilishwa na Bajeti ndogo na migogoro kati ya wakulima na wafugaji.
"Maeneo ya wafugaji yapo katika kila Halmashauri,changamoto iliyopo maeneo hayo hatuna uhakika kama yatatosheleza mifugo iliyopo, halafu pia maeneo husika hayajapimwa"
Katibu Mkuu (Mifugo) Dkt. Maria Mashingo akijibu baadhi ya hoja zilizoibuliwa na wawekezaji washamba la Hanga Ngadinda |
vifaa vya kutunzia maziwa |
Katibu Mkuu akiwa ofisini kwa Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma (RAS) pamoja na baadhi ya wataalamu aliofuatana nao katika ziara hiyo |
Katibu Mkuu akisalimiana na baadhi ya wafugaji mara tu alipowasili katika shamba la mifugo la Hanga Ngadinda Madaba |
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Madaba Bw. Shafi Mpenda akitoa taarifa ya Wilaya yake kwa Katibu Mkuu katika Kijiji cha Igawisenga |
Baadhi ya bwawa yaliyopo katika kituo cha Ruhila Aquaculture Development Centre Mjini Songea |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni