Nav bar

Jumatano, 1 Novemba 2017

KATIBU MKUU SEKTA YA MIFUGO ATEMBELEA MKOA WA SONGWE

KATIBU MKUU WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI (SEKTA YA MIFUGO) DKT MARIA MASHINGO ATEMBELE MKOA WA SONGWE.

Katika kuhakikisha usalama wa Malisho ya Mifugo ya ndani ya nchi yetu unakuwepo wa kutosha,Katibu mkuu Mifugo Dkt.Maria Mashingo amefanya ziara katika mkoa wa Songwe Ili kujua ni kwa kiwango gani mifugo kutoka nchi jirani inaingia Mkoani humo.

Akiwa katika mkoa wa Songwe Dkt Maria Mashingo alipata fursa ya kutembelea Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi,Kiwanda Kidogo cha maziwa cha mbozi,Halmashauri ya Mji wa Tunduma,Halmashauri ya Wilaya ya Ileje pamoja na mpaka waTunduma na Isongole Ireje.

Wakitoa maelezo kwa katibu Mkuu baadhi ya Watendaji wakuu wa Halmashauri hizo Wamesema kuwa hakuna mifugo yoyote inayoingia kutoka nchi jirani,yaani Malawi na Zambia hapa nchini.

Wamemweleza katibu Mkuu kuwa changamoto kubwa inayopatikana kwa sasa ni mifugo kutoka mikoa ya kanda ya ziwa ndio inayoingia katika baadhi ya halmashauri.

Akiongea mbele ya Katibu Mkuu,Afisa Mifugo wa Mkoa wa Songwe Bw.Mpoki Alinanuswe alisema;
"Hakuna mifugo kutoka nchi jirani inayongia hapa nchini,sana sana mifugo yetu ndo inayotoka kwenda nchi jirani kama Zambia kufuata malisho"

Aidha Dkt Maria Mashingo aliwasisitiza watumishi waliopo katika Mpaka wa Tunduma na Isongole kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii,na wanakusanya Maduhuri kwa uadilifu na Uaminifu mkubwa kwani serikali inategeme tozo na kodi hizo Ili iweze kuzitumia katika maendeleo.

"Hakikisheni mnakuja na mkakati mahususi wa kuzuia njia za panya kwa kuwashirikisha halmashauri zenu ili kuziba mianya yote ya njia za panya ambazo zinapitisha bidhaa mbalimbali bila kulipa kodi"

Mpaka wa Tunduma na Isongole kwa upande wa Zoosanitary imeonyesha kuwa dhaifu sana  katika Ukusanyani wa Maduhuri ukilinganisha na zoosanitary ya Kasumulo.

Katibu Mkuu Dkt. Maria Mashingo akiangalia baadhi ya mashine zinazotumika katika kusindika maziwa


Baadhi ya vifaa vinavyotumika katika kusindika maziwa katika kiwanda hicho

 

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ireje Bw. Haji Mussa akimweleza Katibu Mkuu Hali ya Uchumi wa Wilaya ya Ireje

Mtaalamu Mwelekezi wa kiwanda kidogo cha maziwa mbozi Bw. Joashi Kiyoya akimweleza Katibu Mkuu jinsi mashine aina ya Batch pasteurize inavyofanya kazi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni