Nav bar

Jumatano, 1 Novemba 2017

DKT. MARIA MASHINGO ATEMBELEA SHAMBA LA MIFUGO PERAMIHO RUVUMA

KATIBU MKUU WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI (SEKTA YA MIFUGO) DKT MARIA MASHINGO ATEMBELEA SHAMBA LA MIFUGO PERAMIHO RUVUMA.

Katika harakati za kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili Sekta ya Mifugo,Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Sekta ya Mifugo) Dkt. Maria Mashingo leo ametembelea  shamba la Mifugo lililopo Peramiho mjini Songea mkoani Ruvuma.

Aidha katika ziara hiyo Dkt.Maria Mashingo alifuatana na Mkuu wa Wilaya ya Songea Mhe. Pololet Mgema,Meneja wa shamba la Kitulo lililopo Makete, Meneja wa shamba la Sao Hill lililopo Iringa Mafinga na Wataalam Wengine.

Awali Katibu Mkuu Mifugo alifanikiwa kutembelea mikoa ya Mbeya, Songwe, Njombe na Ruvuma.Lengo la kutembelea hiyo mikoa ni kutaka kujua ni kwa kiasi gani mikoa hiyo inapokea ng'ombe kutoka nchi jirani inayoingia hapa nchini kinyume cha sharia.

Katibu Mkuu Dkt. Maria Mashingo akiwa ameshika moja ya soseji zinazoengenezwa katika kiwanda cha nyama kilichopo shambani hapo


Katibu Mkuu akishauriana jambo na Mkuu wa Wilaya ya Songea Mhe. Pololet Mgema


Ng`ombe aina ya Borani waliopo shamba la Mifugo la Peramiho Mjini Songea


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni