Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa (Mb) amesema kwa sasa mahitaji ya maziwa nchini yameongezeka, hivyo kuna haja ya serikali kuongeza Mitamba ya Ng’ombe wa Maziwa ili kuongeza uzalishaji utakaokidhi Soko la Maziwa. Katika ziara yake Kwenye Shamba la Kuzalisha Mifugo la Kitulo Mkoani Njombe Leo Mei 02, 2026 Mhe. Dkt. Bashiru amesema kwa sasa wafugaji wamepata mwamko wa kufuga kisasa lakini uhitaji wa mbegu bora za ng’ombe wa maziwa bado ni mkubwa ukilinganisha na uzalishaji. “Wananchi wamehamasika kufuga kisasa, sio wote lakini idadi iliyopo inaridhisha, eneo la ufugaji wa ngombe wa maziwa linavutia kwa sababu mahitaji ya maziwa hapa nchini ni makubwa kuliko uzalishaji wetu, lakini ili kuongeza uzalishaji wa maziwa hapa ndio tunaweza kupata suluhu kwenye eneo la mbegu bora hapa nchini, watu wanaenda Zambia, Kenya, Africa Kusini watu wanahangaika kupata mbegu bora” alisema Mhe. Balozi Dkt. Bashiru. Aidha, aliongeza kwa kumuagiza Mkurugenzi wa Uzalishaji ...
Maoni
Chapisha Maoni