Nav bar

Jumanne, 2 Desemba 2014

WIZARA YAFANYA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI KWA MFUGAJI WA KUKU MIEMBE SABA - KIBAHA NOVEMBA 2, 2014



Mfugaji wa kuku Bibi Fransisca Macha akitoa maelezo kwa Waaandishi wa Habari (wapo nje ya banda ) Kuwa ana kuku 2200 na Kuku wanazalisha trei 21 kwa siku, Ameeleza Changamoto kubwa ni Soko 
Sehemu ya Kuku wa Mayai wanaofugwa na Bibi Fransisca Macha Shamba hilo lipo eneo la Miembe Saba Kibaha  

Msemaji wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Mohammed Bahari (mwenye suti katikati) akiwa na mfugaji wa kuku Miembe Saba- Kibaha  Mama Fransisca Macha (mwenye mtoto), Afisa Mawasiliano Bibi Judith Mhina, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Uzalishaji na Masoko  Bibi Magreth Mkami, na kutoka kushoto ni Afisa Habari kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Fatma Salum na Dkt. Niwael Mtui Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti wa Magonjwa ya Mifugo na Usafirishaji wa Wanyama na Mazao yake.

Msemaji wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Mohammed Bahari (mwenye suti kushoto) akizungumza na waandishi wa habari  nyumbani kwa mfugaji wa kuku  Miembe Saba - Kibaha.
Vijana wanaotoa huduma kwa kuku hao wakisikiliza kwa makini  hoja mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa .

Mwandishi wa Habari  kutoka gazeti la Tanzania Daima Bi. Asha Bani, Akiuliza swali juu ya uagizaji  wa kuku kutoka nje ya nchi.
Mwandishi wa Habari kutoka TBC-1 Bw Egidius Audax, akiomba ufafanuzi wa ni jinsi  gani Elimu inawafikia wafugaji nchini Tanzania, na Katikati ni Mwandishi wa Habari wa Shirika la Utangazaji la Zanzibar Bw Edward Lusagwa

Mwanahabari kutoka kituo cha television cha Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) bwn. Edward Lusagwa akitaka ufafanuzi wa hatua zinazochukuliwa na Wizara kudhibiti ugonjwa wa Kideli  nchini.
  Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti wa Magonjwa ya Mifugo na Usafirishaji wa Wanyama na Mazao yake Dkt. Niwael Mtui, akijfafanuahoja mbalimbali za wahahabari  (hawapo pichani) .
Msemaji wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Mohammed Bahari na baadhi ya watendaji wa Wizara hiyo wakisikiliza kwa makini hoja mbalimbali zilizotolewa na wanahabari .

Mwanahabari kutoka kituo cha televisheni cha Channel Ten Bi. Kisa  Mwaipiana akiuliza swali juu ya uvumi wa dawa za ARV  kupewa kuku wa kisasa .


mwakilishi wa Mkurugenzi wa Uzalishaji na Masoko  Bibi Magreth Mkami akifafanua hoja mbalimbali zilizotolewa na wanahabari (hawapo pichani)

kuku wa nyama na mayai wanaofugwa na Mama Fransisca Macha wakiwa katika mabanda ya kisasa.





Maoni 1 :

  1. Hivi mama hayo mabanda yakufugia hao kuku yanauzwa wapi na nibei gani??

    JibuFuta