MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA UHURU WA SIKU YA WANYAMA DUNIANI YALIYOFANYIKA KITAIFA MKOA WA DAR-ES-SALAAM, VIWANJA VYA MNAZI MMOJA TAREHE 4/10/2011. MGENI RASMI WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI MHE DKT DAVID MATHAYO DAVID (MB)
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt David Mathayo David (Mb) akizindua nembo ya Shirika lisilo la kiserikali la Kuzuia Ukatili kwa Wanyama Tanzania (Tanzania Society for Prevention of Cruerity to Animals -TSPCA)
Waziri akiangalia Nembo ya TSPCA mara baada ya kuizindua . Pembeni mwa Waziri ni Mwenyekiti wa TSPCA Dkt Sinare
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt David Mathayo David akimkabidhi cheti na Hundi ya thamani ya Shilingi laki tano (500,000/=) Mwandishi Bora wa Makala za wanyama kwa mwaka 2011 Bw Godfrey Monyo wa Kampuni ya The Guardian LTD, ITV na Radio One.
Waziri akionyesha alichomkabidhi Mwandishi Godfrey Monyo katika picha ya pamoja.Mwenye miwani ni Mkurugenzi Mkuu wa Afrika wa WSPCA Bw Nick De Souza.
Paredi ya Mbwa na wanao wahudumia katika viwanja vya Mnazi Mmoja wakati wa Maadhimisho ya Siku
Paredi ya Mbwa pamoja na Wahudumu wao wakipita mbele ya mgeni Rasmi Waziri wa Maendeleo ya mifugo na Uvuvi (hayupo pichani) na kutoa heshima. Hii inaonyesha ni jinsi gani Wanyama walivyo karibu na Binadamu na wanauelewa na usikivu.
Mbwa kama Wanyama wengine wanahitaji kupendwa na wanaowafuga au kuwahudumia. Hii inaonyesha uhalisi wa maisha ya mwanadamu katika kuishi na wanyama wengine. Picha inaonyesha wanaowahudumia mbwa wakiwa wamewakumbatia wanyama hao kama ishara ya kuwapenda.
Mbwa wakipewa amri na wanaowahudumia kuwa wakae na kutulia na Mbwa hao wametii amri kama wanavyoonekana kwenye picha.
Mbwa wa Polisi aliyefundishwa kupita kwenye sehemu ambazo zina njia zisizorasmi akipita kwenye chuma la duara alilowekewa. Hii ilikuwa ni katika siku ya Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanyama Duniani. Pembeni ni Wananchi waliohudhuria katika Maadhimisho hayo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni