Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt David Mathayo David akisalimiana na viongozi wa Wilaya ya Mvomero
|
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mvomero Bibi Joyce Mengele, akisoma taarifa ya Wilaya ya Mvomero.
Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Mvomero akiandika wakati Mkurugenzi akitoa Taarifa ya Wilaya kwa Mhe Waziri.
Mhe Waziri akitaka ufafanuzi fulani kutoka kwa watendaji wa Halmashauri hiyo.
Msafara wa Waziri uliwasili katika Kijiji cha Dakawa Sokoine na picha onaonyesha Baadhi ya waliongozana na Mhe waziri wakisalimia wafugaji mara walipowasili kijijini hapo.
Wanakijiji wameketi huku wakimsikiliza Mkuu wa Msafara Afisa Tawala wa Wilaya, akimkaribisha Waziri na Ujumbe wake na Ujumbe wa Kijiji kusoma Risalla yao kwa Mgeni Rasmi
Kiongozi wa Kabila la wamasai kijiji cha Dakawa Sokoine akiomba Mungu kabla ya kuanza Mkutano.
Kiongozi Mkuu wa Kabila la Wamasai wa Kijiji cha Dakawa Sokoine akijaribu kutoa nasaha zake kabla ya kuanza kutoa risala yao. Alisisistiza ni muhimu kuwa na utulivu subira na pia kuridhika na majibu yatakayotolewa na Mhe. Waziri.a.
Msoma Risala akisoma risala, mbele ya Mhe Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi.
Mara baada ya kumaliza kusoma risala alimkabidhi Mhe. Waziri na alipotaka kuondoka akamuomba arudi asome hoja moja moja naye atazijibu.
Msoma Risala akimkabidhi Mhe. Waziri Risala Husika
Waziri anamuelekeza Msoma risala kuwa utapitia hoja za mwaka jana moja hadi moja nami nitatoa majibu.
Mhe. Waziri akisisitiza jambo wakati wa kujibu Hoja za mwaka 2011
Mhe Waziri alipomaliza hoja za Mwaka jana alimuita kijana mwingine sasa asome hoja za mwaka 2012 mpya jukumu hilo alipewa kijana aliyejulikana kwa jina la Charles Loiruck
Umati wa Jamii ya wafugaji wakifuatilia Mkutano huo Kiji cha Dakawa Sokoine
Mvua ilianza kunyesha lakini Mhe. Waziri akaendelea kutoa majibu ya hoja mbalimbali ambazo ziliulizwa na Jamii hiyo ya wafugaji.
Msoma Risala wa Kijiji cha Dakawa Sokoine mbele yake Waziri (ameketi) anayesikiliza kwa makini
Afisa Tawala wa Wilaya ya Mvomero Bw. Mingele akimshukuru Msoma Risala na kumkaribisha Mhe. Waziri ajibu hoja za wanakijiji cha Dakawa Sokoine.
Simu za Mkoni ni sehemu ya Maedeleo hata Vijijini, wanakijiji wa Wami Sokoine wakirekodi video ya Mkutano mzima unaofanyika
Wakina mama wa Kijiji cha Dakawa Sokoine hawako nyuma nao wamehudhuria Mkutano
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni