WIZARA YALENGA KUBORESHA KOSAFU ZA SAMAKI

Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeandaa kikao kazi cha wataalam kujadili maandalizi ya kuanzisha Programu ya Taifa ya Uboreshaji wa Kosafu za Samaki (National Fish Breeding Programme), kwa lengo la kuongeza tija, ubora wa mbegu za samaki na kuhakikisha uendelevu wa sekta ya ukuzaji viumbe maji nchini.

Kikao hicho kimefanyika leo tarehe 11 Septemba, 2026, jijini Dodoma, kinawaleta pamoja wataalam kutoka Wizara na taasisi mbalimbali kwa ajili ya kujadili mikakati, fursa na hatua muhimu za kuanzisha programu hiyo.

Akiongoza kikao hicho, Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Viumbe Maji, Dkt. Nazael Madalla, amesema kuwa kuanzishwa kwa programu hiyo ni hatua muhimu katika kuimarisha upatikanaji wa kosafu bora za samaki, kuongeza uzalishaji na tija kwa wafugaji, pamoja na kuchochea maendeleo endelevu ya sekta ya ukuzaji viumbe maji nchini.




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

WATAALAMU WATAKIWA KUKUSANYA TAKWIMU SAHIHI ZA KITAFITI

TANZANIA DAIRY BOARD

LESENI, VIBALI VYA MAZAO YA MIFUGO NA VYAKULA VYA SAMAKI KUTOLEWA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI