WAZIRI DKT. BASHIRU AFANYA MAZUNGUMZO NA BODI YA NARCO
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa leo Agosti 29, mwaka 2026 amekutana na kufanya mazungumzo na Bodi ya Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) kujadili utekelezaji wa majukumu ya kampuni hiyo pamoja na kupata maoni, ushauri na mapendekezo ya bodi kuhusu namna ya kuzitatua changamoto zinazoikabili NARCO ili iweze kujiendesha kwa faida na tija katika uzalishaji na uwekezaji kwenye sekta ya mifugo ikiwemo usimamiaji wa Vitalu na mashamba ya mifugo ya serikali.
Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, uliopo Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma, ambapo Wajumbe wa Bodi ya NARCO, viongozi wa wizara akiwemo Katibu Mkuu Bi. Agnes Meena, Naibu Katibu Mkuu Anayesimamia Sekta ya Mifugo Dkt. Fabian Madele, Naibu Katibu Mkuu Anayesimamia Sekta ya Uvuvi Prof. Mohamed Sheikh na Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu Dkt. Charles Mhina, walishiriki kikao hicho.


Maoni
Chapisha Maoni