WABUNGE KUHAMASISHA VIJANA KUOMBA MIKOPO YA SEKTA ZA MIFUGO NA UVUVI

Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi, imetoa rai kwa Wabunge wa Mikoa Nane  ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwahamisha vijana kuchangamkia fursa ya kuomba mikopo ya uwezeshaji vijana kiuchumi awamu ya pili katika sekta za mifugo na uvuvi .

Rai hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Ng'wasi Kamani kwa niaba ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi wakati akizungumza na wabunge wa Mikoa Nane ukiwemo Mkoa wa Kagera, Simiyu, Kigoma, Rukwa, Katavi, Ruvuma, Njombe na Mbeya katika kikao kuhusu uhamasishaji wa vijana kuomba mikopo ya uwezeshaji kiuchumi katika sekta hizo, kikao kilichofanyika leo Septemba 03, 2026 Bungeni jijini Dodoma.

Katika taarifa kuhusu mikopo hiyo, Naibu Waziri Mhe. Kamani alieleza kuwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, ilipokea kiasi cha shilingi bilioni 23.68 ikiwa ni sehemu ya shilingi bilioni 200 za ahadi ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania za kuwezesha vijana  na kampuni changa kujiajiri na kujiinua kiuchumi.

Amesema mikopo ya uwezeshaji vijana kwenye sekta ya mifugo na uvuvi, imelenga kuongeza uzalishaji wa mazao ya mifugo na uvuvi kupitia vijana watakaowezeshwa  mikopo ya masharti nafuu ili wajiajiri katika miradi ya ufugaji, uvuvi na uchakataji ambapo tayari wizara imeshatoa mikopo awamu ya kwanza na wizara inaendelea kupokea maombi awamu pili inayoendelea ambapo mwisho wa maombi ya mikopo kwa awamu ya pili ni Septemba 14, 2026.

Mhe. Kamani amesema awamu ya kwanza kuna mikoa ilikuwa na mwamko mkubwa wa kuchangamkia fursa hiyo ikiongozwa na Mkoa wa Mara, huku baadhi ya mikoa ilionekana kuwa nyuma katika maombi ya mikopo na amewaomba wabunge kwenda kuwahamasisha vijana kuomba mikopo hiyo pamoja na kuzingatia masharti na vigezo vya maombi ili waweze kupata fursa hiyo adhimu.

Baadhi ya wabunge wakati wakichangia kwenye kikao hicho waliipongeza wizara kwa kusimamia na kutekeleza kwa vitendo utoaji wa mikopo kwa vijana hususan katika ufugaji wa samaki kwa vizimba, na kutoa maoni na ushauri kwa wataalam wa wizara ili kurahisisha uratibu wa mikopo na kuwasiaidia vijana kunufaika na fursa hiyo.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Ng'wasi Damas Kamani alipokuwa akizungumza na Wabunge kuhusu Uhamasishaji wa Vijana Kuomba Mikopo ya Uwezeshaji Kiuchumi katika Sekta za Mifugo na Uvuvi, katika kikao kilichofanyika Bungeni jijini Dodoma leo Septemba 03, 2026.





Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Ng'wasi Kamani akizungumza na Wabunge kuhusu uhamasishaji wa vijana kuomba mikopo ya uwezeshaji kiuchumi katika sekta za mifugo na uvuvi wakati wa kikao kilichofanyika leo Septemba 03, 2026.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Dkt. Fabian Madele akieleza jinsi watakavyofanyika kazi maoni ya Wabunge kuhusu Mikopo ya Uwezeshaji Vijana Kiuchumi wakati wa kikao kilichofanyika leo Septemba 03, 2026 Bungeni jijini Dodoma.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

WATAALAMU WATAKIWA KUKUSANYA TAKWIMU SAHIHI ZA KITAFITI

TANZANIA DAIRY BOARD

SHAMBA LA KITULO KUWA KITOVU CHA NG’OMBE BORA WA MAZIWA NCHINI