UTALII WA NYANGUMI KUFUNGUA UCHUMI WA BULUU MTWARA 2026

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Mhe. Abdallah Mwaipaya, amezindua rasmi Tamasha la Nyangumi (Nyangumi Festival 2026) katika Viwanja vya Mashujaa, Mtwara Mjini, akisema uwepo wa nyangumi katika bahari za Mtwara ni lango la kukuza uchumi wa buluu, utalii wa kiikolojia na biashara, sambamba na kuimarisha uhifadhi wa mazingira ya bahari.

Akizungumza katika uzinduzi wa tamasha hilo Mh. Mwaipaya ameendelea kwa kusema kuwa Nyangumi Festival imetoa nafasi kwa Mkoa wa Mtwara kuonesha utamaduni, vipaji vya vijana, bidhaa mbalimbali za wajasiria mali, Sanaa, michezo na vivutio vinavyopatikana katika Mkoa wa mtwara.

 “Natoa wito kwa wananchi wote kushiriki kikamilifu katika shughuli za tamasha hili nakutumia fursa zinzotokana nalo, ili kufungua biashara na kutengeneza ajira katika sekta mbali mbali zinazohusiana na uchumi wa buluu hususan kwa vijana na wanawake”. Amesema Mh. Mwaipaya

Aidha Mh. Mkuu huyo wa Wilaya ameeleza umuhimu wa uhifadhi shirikishi wa rasiliamali za bahari kati ya Serikali na jamii kwa kushikiana na wadau na mashirika ya uhifadhi ili kuwezesha ulinzi wa rasilimali za bahari na matumizi endelevu ya rasilimali hizo kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho, huku akisisitiza kuwa kuilinda bahari ni wajibu wa kila mmoja kwani tukilinda bahari tunalinda maisha na mustakabali ya jamii zetu. 

Tamasha la Nynangumi 2026 lililobeba kauli mbiu isemayo “Kulinda nyangumi, Kuhifadhi Bahari, Kukuza Utalii endelevu” ni jukwa la kuongeza uelewa kuhusu uhifadhi wa mazingira ya bahari na rasilimali za asili sambamba na kukuza utalii endelevu kwa mkoa wa Mtwara na Tanzania kwa ujumla.

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mh. Abdallah Mwaipaya (katikati) akupokea maelezo kutoka kwa Meneja wa Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) Dkt. Emmanuel Sweke wakati alipotembela banda la MPRU katika Maonesho ya Nyangumi 2026.

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mh. Abdallah Mwaipaya (kushoto) akisalimiana na Meneja wa Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) Dkt. Emmanuel Sweke katika viwanja vya Mashujaa, Mtwara

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mh. Abdallah Mwaipaya (kushoto) akisalimiana na Mhifadhi Mfawidhi wa Hifadhi ya Bahari ya Ghuba ya Mnazi na Maingilio ya Mto Ruvuma (MBREMP) Dkt. Redfred Ngowo katika viwanja vya Mashujaa, Mtwara



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

WATAALAMU WATAKIWA KUKUSANYA TAKWIMU SAHIHI ZA KITAFITI

TANZANIA DAIRY BOARD

SHAMBA LA KITULO KUWA KITOVU CHA NG’OMBE BORA WA MAZIWA NCHINI