SERIKALI YAONGEZA MSUKUMO KUIMARISHA MAENEO YA MALISHO

Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi, imesema inaendelea kutoa elimu kwa wafugaji kuhusu matumizi endelevu ya maeneo ya malisho, uzalishaji na uhifadhi wa malisho, afya ya mifugo pamoja na matumizi ya teknolojia za kuongeza tija katika ufugaji.

Akijibu swali Bungeni leo Septemba 04, 2026 la Mbunge  wa Bububu, Mhe.Salum Khamis Salim,  aliyehoji ni lini serikali inampango gani wa kutoa elimu kwa wafugaji pamoja na kuongeza maeneo ya malisho yanayolingana na idadi ya mifugo, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Ng'wasi Damas Kamani amesema katika bajeti ya mwaka 2026/2027, Wizara imetenga Shilingi bilioni moja kwa ajili ya kuwapa mafunzo Maafisa Ugani kuhusu teknolojia na mbinu mpya za uzalishaji na masoko.

Mhe. Kamani amesema pia Serikali imeanzisha Kituo cha Huduma kwa Mteja kitakachopokea na kutatua changamoto za wafugaji, pamoja na kutoa taarifa, ushauri na elimu kuhusu huduma mbalimbali za mifugo.

Aidha,  katika mwaka 2025/2026, Wizara kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi na Serikali za Mitaa imetenga hekta 196,324.25 katika vijiji 187 vya Wilaya 22, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa lengo la kutenga hekta milioni 2.53 ifikapo mwaka 2030.


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

WATAALAMU WATAKIWA KUKUSANYA TAKWIMU SAHIHI ZA KITAFITI

TANZANIA DAIRY BOARD

SHAMBA LA KITULO KUWA KITOVU CHA NG’OMBE BORA WA MAZIWA NCHINI