PROF. SHEIKH ASISITIZA NIDHAMU,KUJITUMA SHIMIWI 2026

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Mohammed Sheikh amewataka watumishi watakaoiwakilisha Wizara hiyo kwenye michuano ya SHIMIWI mwaka huu kuhakikisha wanadumisha nidhamu na wanajituma kwenye michezo yote watakayoshiriki kwenye michuano hiyo.

Prof. Sheikh amesema hayo wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wachezaji hao iliyofanyika leo Septemba 18,2026 kwenye ofisi za Wizara hiyo zilizopo Mtumba jijini Dodoma ambapo amewataka wachezaji hao kuhakikisha wanarejea na vikombe vingi zaidi ya walivyotwaa mwaka jana mkoani mwanza.

“Najua mnalipwa posho lakini juhudi zenu za kujitoa ndio kubwa zaidi kuliko posho mlizolipwa na kwa hilo niwapongeze sana kwani sio kila mtu anaweza kujitoa kiasi hicho” Amesema Prof. Sheikh.

Aidha Prof. Sheikh amewataka wachezaji hao kudumisha furaha na amani wakati wote wa michuano hiyo huku akisisitiza umoja kwa wachezaji wote mbali na kila mtu kushiriki mchezo aliofanyia mazoezi.

Kwa upande wake katibu wa Michezo Wizarani hapo Bw. Salamala Masoud amesema kuwa takribani wachezaji 100 wa Wizara hiyo wanatarajiwa kushiriki michezo mbalimbali ikiwepo mchezo wa mpira wa miguu, kuvuta kamba,mbio ndefu na fupi,bao na kurusha vishale.

Michuano hiyo inatarajiwa kutimua vumbi kwa takribani wiki 3 kuanzia Septemba 20,2026 mkoani kilimanjaro.









Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

WATAALAMU WATAKIWA KUKUSANYA TAKWIMU SAHIHI ZA KITAFITI

TANZANIA DAIRY BOARD

LESENI, VIBALI VYA MAZAO YA MIFUGO NA VYAKULA VYA SAMAKI KUTOLEWA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI