MHE. KAMANI AKUTANA NA MKUU WA MKOA WA MWANZA KUJADILI MAENDELEO SEKTA YA MIFUGO NA UVUVI
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Ng'wasi Damas Kamani leo Septemba 14, 2026 amewasili Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. CP. Salum Rashid Hamduni.
Mazungumzo ambayo yalijikita katika kuboresha Sekta za Mifugo na Uvuvi ili kuongeza tija katika shughuli za uzalishaji wa sekta hizo, hususan suala ya uwezeshaji wa mikopo kwa vijana kwenye sekta hizo pamoja na uwekezaji na udhibiti wa shughuli za uvuvi haramu.




Maoni
Chapisha Maoni