DKT. BASHIRU ASHIRIKI UZINDUZI WA MPANGO WA KIMATAIFA WA USTAWI WA UMMA BAHARINI

Septemba 17, 2026 Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa ameshuhudia uzinduzi wa Mpango wa Kimataifa wa Ustawi wa Umma wa Baharini katika Muongo wa Bahari (Global Initiative for the Ocean Decade Marine Public Welfare Action).

Mpango huo unajikita katika uwezeshaji wa kisayansi, uhifadhi wa mazingira, ushiriki wa umma, na uchumi wa bluu ili kutoa matokeo katika usimamizi wa bahari kwa jamii za pwani duniani na kwa vizazi vijavyo.

Mpango huo umezinduliwa wakati wa ufunguzi rasmi wa Jukwaa la Dunia la Maendeleo ya Bahari linaloendelea katika Jiji la Qingdao nchini China.

Pia Mhe. Balozi Dkt. Bashiru alihutubia Jukwaa la Kimataifa la Maendeleo ya Bahari, ambapo aliwaeleza washiriki kuhusu Dira 2050  pamoja na fursa zilizopo katika Sekta ya Uvuvi. 

Amesema Dira2050 ambayo imeanza kutekelezwa Julai Mosi 2026, imeweka msisitizo katika uchumi wa buluu na Uvuvi kama sekta muhimu za ukuaji wa uchumi  kuelea Tanzania ya uchumi wa Kati wa Juu wa Dola trilioni moja ifikapo mwaka 2050, ambapo Tanzania ina rasilimali kubwa ya maji ambayo zi zaidi ya asilimia 30 ya eneo la nchi.

Aidha,  amesisitiza kuwa kiu ya maendeleo duniani kote haitakiwi kusahau kuhifadhi mazingira ya bahari ambayo yanatuwezesha kukua kiuchumi.

Mhe. Balozi Dkt. Bashiru alitumia fursa hiyo kuwakaribisha washiriki kuja kuwekeza nchini katika maeneo mbalimbali ikiwemo eneo la uendeshaji wa pamoja wa Bandari ya Uvuvi. Ameziomba pia taasisi za elimu na utafiti kushirikiana na taasisi zilizo chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja vyuo vikuu.




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

WATAALAMU WATAKIWA KUKUSANYA TAKWIMU SAHIHI ZA KITAFITI

TANZANIA DAIRY BOARD

LESENI, VIBALI VYA MAZAO YA MIFUGO NA VYAKULA VYA SAMAKI KUTOLEWA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI