DKT. NCHEMBA KUZINDUA MAONESHO YA NANE NANE 2026 AGOSTI MOSI

Waziri wa Kilimo, Mhe. Daniel Chongolo  ametembelea na kukagua maandalizi kuelekea Maonesho ya Kimataifa ya Nane Nane kwa Mwaka 2026, na kueleza kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba.

Mhe. Chongolo ameeleza kuwa uzinduzi huo utafanyika kesho Agosti Mosi 2026 katika Viwanja vya Maonesho ya Kimataifa vya Dkt. John Malecela jijini Dodoma.

Aidha, katika ziara yake ya ukaguzi wa Maandalizi hayo, Mhe. Chongolo ameeleza kufurahishwa  jinsi Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) ilivyojipanga kwa kutoa huduma ya nyama choma na akaeleza kuwa kutakuwa na shughuli mbalimbali za maonesho katika sekta za kilimo, mifugo na uvuvi ambapo ameeleza kuwa  Paredi la Mifugo linaloratibiwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi llitafanyika Agosti 5, Mwaka huu.

Vilevile, alieleza kuwa baada ya uzinduzi wa maonesho hayo, serikali, wadau, taasisi wataendelea kutoa huduma mbali kwa wananchi wakati na baada maonesho hayo.

Kaulimbiu ya Mwaka Huu: Tambua Soko, Zalisha kwa Tija Kutekeleza Dira 2050




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

WATAALAMU WATAKIWA KUKUSANYA TAKWIMU SAHIHI ZA KITAFITI

UTEKELEZAJI WA UFUGAJI SAMAKI KWA VIZIMBA WAANZA ZIWA TANGANYIKA

TANZANIA DAIRY BOARD