Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili, 2026

SHILINGI BIL. 30.7 KUWANUFAISHA VIJANA PROGRAMU YA BBT

Picha
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Ng’wasi Kamani amesema serikali inaendelea kutekeleza Programu ya Jenga Kesho Iliyobora (Building Better Tomorrow - BBT) ambapo katika mwaka wa fedha 2025/2026 wizara hiyo imepokea shilingi bilioni 30.7 (Sekta ya uvuvi shilingi bilioni 25.9 na sekta ya mifugo shilingi  bilioni 4.75) kwa ajili ya kuwawezesha wavuvi wadogo pamoja na vijana katika maeneo mbalimbali hapa nchini.  Mhe. Kamani amesema hayo leo Aprili 10, 2026 Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Vitimaalum, Mhe. Maryam Azan Mwinyi, kwenye Kipindi cha Maswali na Majibu cha Bunge la 13, Mkutano wa Tatu, Kikao cha Sita. Swali la Mbunge huyo lilihoji hatua inayochukuliwa na serikali kuwawezesha Wananchi hususani Vijana na Wavuvi wadogo kushiriki kikamilifu katika uchumi wa Bluu. “ Mheshimiwa Spika, Kupitia programu ya BBT, vijana 308 wamepatiwa mikopo isiyo na riba na yenye masharti nafuu kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya ufugaji wa samaki kwenye vizimba, ufug...

VIJANA 200 KUNUFAIKA NA FURSA ZA UNENEPESHAJI WA MBUZI NA KONDOO

Picha
Na. Stanley Brayton, WMUV Wizara ya Mifugo na Uvuvi inayotekeleza Mradi wa miaka mitano wa Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT) ya Unenepeshaji wa Mbuzi na Kondoo katika eneo la Kituo cha Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) iliyopo Wilayani Kongwa, imepanga kuwawezesha vijana 200 wa Kitanzania kupata Mafunzo hayo ikiwa na lengo la kuongeza ushiriki wa vijana na wanawake katika ujasiliamali wa Biashara ya Mifugo. Akizungumza leo Aprili 9, 2026 Wilayani Kongwa Jijini Dodoma kwa Niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, wakati wa warsha ya utambulisho wa Mradi huo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Dkt. Fabian Madele, amesema mradi huo wenye thamani ya takribani shilingi Billioni 81, unalenga kuwawezesha vijana kupitia shughuli za unenepeshaji wa mbuzi na kondoo kibiashara, uzalishaji wa malisho na mbegu za malisho, uchakataji wa vyakula vya mifugo, pamoja na matumizi ya teknolojia za kisasa. "Walengwa wakuu wa mradi huu ni vijana, ambao kupitia utekel...

SHILINGI BIL. 30.8 KUTUMIKA KWENYE CHANJO NA UTAMBUZI MIFUGO 2026/2027

Picha
Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi, imetenga shilingi bilioni 30.8 ili kuendelea na awamu ya pili ya Kampeni ya Kitaifa ya Chanjo na Utambuzi wa Mifugo katika maeneo mbalimbali hapa nchini. Hayo yameelezwa leo Aprili 09, 2026 Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Ng’wasi Kamani wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha, Mhe. Marirta Gido Kivunge lililohoji,  je serikali ina mpango gani wa kutoa huduma za dawa na chanjo muhimu ilibkuboresha afya na kuwaongezea thamani ya mifugo? Mhe. Kamani amesema serikali inaendelea na mpango wa kudhibiti magonjwa ya mifugo kwa kutekeleza Mpango wa Chanjo na Utambuzi wa Mifugo wa miaka mitano wenye thamani ya jumla ya shilingi bilioni 216, unaotekelezwa kuanzia 2024/2025 hadi 2028/2029. “Mheshimiwa Mwenyekiti katika bajeti ya Mwaka 2024/2025, Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi ilitenga kiasi cha Shilingi Bilioni 61.2 kwa ajili kuendesha kampeni ya chanjo na utambuzi wa mifugo, ambapo hadi ...

PROFESOR SHEIKH AWATAKA WAKAGUZI WA MAZAO YA UVUVI KULISAIDIA TAIFA KUSAFIRISHA KWA WINGI MAZAO YA UVUVI NJE YA NCHI

Picha
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Uvuvi Prof. Mohammed Sheikh amewataka wakaguzi wa mazao ya uvuvi kufanya kazi zao kwa ubora ili kulisaidia Taifa kuongeza kiwango cha  mazao ya uvuvi yanayosafirishwa nje ya nchi. Prof Sheikh ametoa kauli hiyo 8 April 2026 wakati akizindua mafunzo ya siku tano kwa maafisa wakaguzi wa mazao ya uvuvi 25 yaliyoandaliwa na  Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) kwa kushirikiana na Shirika la Kilimo na Chakula Duniani (FAO). "Takwimu zinaonesha kwasasa tunasafirisha tani 60,000  pekee za samaki kwenda nje ya nchi hivyo uwepo wa mafunzo haya uwe chachu ya kuongeza ubora utakaosaidia Taifa kuongeza kiasi cha samaki kinachopelekwa nje ya nchi" Amesema Prof. Sheikh Akiongea Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) Dkt Semvua Mzighani amesema Mafunzo haya yamelenga kuwajengea uwezo  maafisa ukaguzi wa mazao ya uvuvi juu ya taratibu za ukaguzi wa mazao ya uvuvi pamoja na  viwango vya ub...

PROF. SHEIKH ATEMBELEA KIWANDA CHA KUCHAKATA MWANI TANI 30, 000 ZANZIBAR

Picha
Kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Naibu Katibu Mkuu ( Uvuvi) Prof. Mohamed Ali Sheikh ametembelea Kiwanda na kukagua cha Kuchakata Zao la Mwani kilichoko Kisiwani Pemba katika ziara aliyoifanya Aprili 02, 2026 lengo ikiwa ni kuimarisha ushirikiano katika kuendeleza na kukuza uchumi wa buluu nchini. Kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuchakata tani 30,000 za mwani kwa mwaka na kitazalisha mbolea, chakula cha wanyama hasa ng'ombe na carageenan. Katika ziara hiyo Prof. Sheikh aliambatana na Meneja wa Kiwanda pamoja na Afisa Mdhamini Wizara ya Uchumi wa Buluu Zanzibar.

DKT. BASHIRU AAGIZA PROGRAMU YA AFDP KUFANYIWA TATHMINI

Picha
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa leo Aprili 2, 2026 amepokea taarifa ya Utekelezaji wa Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) kwa kipindi cha Julai 2022- Machi 2026 inayotekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na Mfuko wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), kikao kilichofanyika Ofisi ndogo za wizara zilizopo Kambarage Tower, jijini Dodoma. Programu hiyo inayojikiza kuongeza tija na faida katika mbegu za kilimo, Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji, Kuboresha upatikanaji wa masoko, kuongeza thamani ya mazao pamoja na kuendeleza sekta binafsi, inagharimu kiasii cha dola za marekani milioni 77.416 ulianza kutekelezwa Julai 2021 na utakamilika Desemba 2027. Pamoja na mambo mengine, baada  ya kupokea taarifa hiyo Mhe. Balozi Dkt. Bashiru ameielekeza timu ya wataalam inayotekeleza programu hiyo kutoka wizarani kutathmini kwa kina sababu zilizochelewesha mradi huo hususani mchakato wa zabuni. Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) inatarajiwa kunufaisha kaya 26...

ELIMU YA TEKNOLOJIA YA KISASA YA MNYORORO WA THAMANI WA MWANI NA JONGOO BAHARI YAWAFIKIA WAKULIMA MKINGA

Picha
Na. Stanley Brayton, WMUV Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeendelea na utekelezaji wa Mradi wa Utekelezaji wa Rasilimali za Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji (TASFAM) kwa kutoa Mafunzo ya awali ya kuwajengea uwezo wa Mnyororo wa thamani Wakulima wa Mwani na Jongoo Bahari, ambao wenye lengo la kuimarisha Usimamizi wa Rasilimali za Baharini na kuboresha maisha ya jamii za pwani Tanzania Bara na Zanzibar kwa kuwanyanyua kiuchumi na kuhakikisha wanazalisha kwa wingi zao la Mwani na Jongoo Bahari. Akizungumza leo Machi 28, 2026 Wilayani Mkinga, wakati wa zoezi la kuwajengea uwezo Wakulima wa Mwani na Jongoo Bahari Wilayani hapo, Afisa Uvuvi Mwandamizi Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Fatuma Juma, amesema Mafunzo hayo ni muhimu kwa Wakulima hao kwani wamepata fursa mbalimbali za kuelewa jinsi ya kulima Mwani na kukuza Jongoo Bahari na kuhifadhi mazao hayo ya Uvuvi ili yawe na ubora kabla ya kuingia sokoni. "Mradi huu wa TASFAM umelenga katika kuwainua wavuvi hususan wakuzaji Viumbemaji kama Jongoo ...

WANUFAIKA WA TASFAM MTAMA WAHIMIZWA KUTUMIA KANUNI BORA ZA UKUZAJI VIUMBE MAJI

Picha
Na. Martha Mbena.  Wanufaika wa Mradi wa kuendeleza na kusimamia Uvuvi wa Baharini na Ukuzaji Viumbe Maji (TASFAM) wa Wilaya ya Mtama mkoani Lindi wamehimizwa kutumia kanuni bora za Ukuzaji Viumbe maji. Akizungumza wakati wa kutoa Elimu kuhusu kanuni ya Viumbe maji Machi 28,2026, Afisa Uvuvi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bw. Justine Ndayeze, amewasisitiza wanufaika hao wasifanye shughuli pasipo kufuata kanuni bora, sheria na taratibu za Ukuzaji viumbe maji ili kuweza kufanya shughuli hizo kwa Uhuru bila kuvunja sheria. "Tusifanye shughuli kimya kimya bila kufanya taratibu zote zilizowekwa na Wizara za Ufugaji na Ukuzaji viumbe maji", Amesema  Bw. Ndayeze. Aidha, Ndayeze ameongeza kusema kuwa kanuni inasisitiza kufuata kanuni kwa kufuata taratibu zote za kutunza mazingira ya viumbe maji, kupata mbegu bora, kukata vibali vya kusafirisha mazao ya uvuvi na kuwa na kumbukumbu za shughuli za ufugaji. Kwa upande wake Mnufaika wa mafunzo hayo Bw. Hassan Namkanda wa kata ya Shuka,...

KAMATI YAPITISHA MPANGO NA BAJETI YA WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI 2026/ 2027

Picha
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Mhe. Deodatus Mwanyika, imeridhia randama ya mpango wa bajeti ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya ( Mifugo na Uvuvi) kwa mwaka wa fedha 2026/2027, leo Machi 28, 2026, Bungeni jijini Dodoma. Katika michango yao, wajumbe wa kamati hiyo wameonesha kuridhishwa na vipaumbele vya wizara kwa mwaka fedha 2026/2027 licha ya bajaeti yake kuwa ndogo, huku wakiipongeza Wizara hiyo kwa maono mapana yanayolenga kukuza sekta ya mifugo na uvuvi na kwamba kamati hiyo imeahidi kuendelea kuishauri serikali kuongeza bajeti kwa ajili ya sekta hizo za uzalishaji. Pamoja na pongezi hizo, Kamati imetoa miongozo na ushauri wa kimkakati unaolenga kuimarisha sekta za mifugo na uvuvi hususan kuongeza uzalishaji, kuongeza maeneo ya malisho ya mifugo, udhibiti wa utoroshaji wa mifugo na usimamizi wa mazao ya uvuvi, ujenzi wa bandari,na viwanda vya kuchakata mazao ya uvuvi. Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balo...

WANUFAIKA TASFAM BAGAMOYO WAJENGEWA UELEWA WA MRADI

Picha
Wanufaika wa Mradi wa Uendelezaji wa Rasilimali za Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji (TASFAM) Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Machi 27,2026 wamejengewa uelewa kuhusu maeneo watakayonufaika kupitia mradi huo. Wakizungumza wakati wa mkutano wa kueleweshwa maeneo mbalimbali yatakayoguswa na mradi huo, Wanufaika hao wameishukuru Serikali kwa kuwapa fursa hiyo ya miaka 5 itakayowawezesha kuboresha shughuli zao za uvuvi na ukuzaji viumbe maji. “Tunaomba wataalam  kupitia mradi huu msikae ofisini mje huku uwandani ili muone kwa vitendo namna tunavyofanya shughuli zetu ili kwa pamoja tuweze kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza wakati wa utekelezaji wa mradi huu” Amesema Bw. Machano Ally muasisi wa chama cha Ushirika cha uzalishaji zao la Mwani cha Msichoke. Kwa upande wake Mwenyekiti wa kikundi cha uzalishaji zao la mwani cha “Nasi Tumo” Bw. Rashid Gubi ameiomba Serikali kupitia mradi huo kuwasaidia boti za kisasa zitakazowasaidia kutekeleza shughuli zao kwa urahisi ikiwa ni pamoja na k...