ELIMU YA TEKNOLOJIA YA KISASA YA MNYORORO WA THAMANI WA MWANI NA JONGOO BAHARI YAWAFIKIA WAKULIMA MKINGA

Na. Stanley Brayton, WMUV

Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeendelea na utekelezaji wa Mradi wa Utekelezaji wa Rasilimali za Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji (TASFAM) kwa kutoa Mafunzo ya awali ya kuwajengea uwezo wa Mnyororo wa thamani Wakulima wa Mwani na Jongoo Bahari, ambao wenye lengo la kuimarisha Usimamizi wa Rasilimali za Baharini na kuboresha maisha ya jamii za pwani Tanzania Bara na Zanzibar kwa kuwanyanyua kiuchumi na kuhakikisha wanazalisha kwa wingi zao la Mwani na Jongoo Bahari.

Akizungumza leo Machi 28, 2026 Wilayani Mkinga, wakati wa zoezi la kuwajengea uwezo Wakulima wa Mwani na Jongoo Bahari Wilayani hapo, Afisa Uvuvi Mwandamizi Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Fatuma Juma, amesema Mafunzo hayo ni muhimu kwa Wakulima hao kwani wamepata fursa mbalimbali za kuelewa jinsi ya kulima Mwani na kukuza Jongoo Bahari na kuhifadhi mazao hayo ya Uvuvi ili yawe na ubora kabla ya kuingia sokoni.

"Mradi huu wa TASFAM umelenga katika kuwainua wavuvi hususan wakuzaji Viumbemaji kama Jongoo Bahari na wakulima wa Mwani ili waweze kuzalisha Mazao hayo kwa wingi na ubora zaidi ili kuongeza Masoko ya nje." amesema Bi. Fatuma 

Aidha, Bi. Fatuma amebainisha kuwa katika zao la Jongoo Bahari wavuvi na wakulima wamejifunza Sifa za zao hilo, jinsi Jongoo Bahari wanavyozaliana, chakula wanachokula, njia za Ufugaji na mahitaji, Usimamizi, Masoko na mambo mbalimbali ya kuzingatia wakati wa kufuga zao hilo.

Vilevile, Bi. Fatuma  ameweka wazi kuwa na kwenye zao la Mwani Wakulima wamejifunza umuhimu wa Mwani kama chakula, dawa na Maligafi, ambapo pia wamejifunza jinsi ya kulima zao hilo, uchaguzi wa eneo la kupandia zao hilo (maji na udongo), utunzaji, uvunaji na uhifadhi, Masoko pamoja na utengenezaji wa bidhaa mbalimbali zitokanazo na Mwani, ikiwemo Sabuni na Mafuta ya kupaka Mwilini ambayo yana muunganiko wa Samli, mafuta ya maji, nta nyepesi na nzinto, manukato, Mwani, Shubili Poli, na hatua mbalimbali za kutengeneza bidhaa hizo.

Pia, Bi. Fatuma  amesema Wizara inataka kufanya Mageuzi katika Sekta ya Uvuvi na ndio maana imeandaa Mpango Mkakati wa Mageuzi wa Sekta ya Uvuvi na Ukuzaji Viumbemaji kwa mwaka 2026/2050, ambao utaleta mabadiliko katika Sekta ya Uvuvi, ndio maana Mafunzo zaidi katika Sayansi ya Baharini yanaendelea kutolewa kwa kuwajengea uelewa wananchi ili waweze kufuga na kulima Mazao ya Uvuvi kwa tija.

Afisa Uvuvi Mwandamizi Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Fatuma Juma, akielezea fursa mbalimbali za zao la Jongoo Bahari, wakati wa zoezi la kuwajengea uwezo wa Mnyororo wa Thamani Wakulima wa Mwani na Jongoo Bahari, elimu inayotolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Mradi wa Utekelezaji wa Rasilimali za Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji (TASFAM), katika Kata ya Manza, Kijiji cha Tawalani, Machi 28, 2026 Mkinga - Tanga.

Afisa Uvuvi Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Ndg. Silas William, akitoa neno la Utangulizi na kuelezea lengo la Mradi wa TASFAM kwa wakulima wa mwani, wakati wa zoezi la kuwajengea uwezo wa Mnyororo wa Thamani Wakulima wa Mwani na Jongoo Bahari, elimu inayotolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Mradi wa Utekelezaji wa Rasilimali za Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji (TASFAM), katika Kata ya Manza, Kijiji cha Tawalani, Machi 28, 2026 Mkinga - Tanga.

Afisa Uvuvi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Ramla Iddi (kushoto), akielezea namna Jongoo Bahari wanavyozaliana, wakati wa zoezi la kuwajengea uwezo wa Mnyororo wa Thamani Wakulima wa Mwani na Jongoo Bahari, elimu inayotolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Mradi wa Utekelezaji wa Rasilimali za Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji (TASFAM), katika Kata ya Manza, Kijiji cha Tawalani, Machi 28, 2026 Mkinga - Tanga.

Mkulima wa Mwani, Bw. Zali Bakari (aliyeshosha mkono mbele), akielezea changamoto zinazowakumba Wakulima wa Mwani ikiwemo uelewa mdogo wa utunzaji, uanikaji na uhifadhi wa Mwani, wakati wa zoezi la kuwajengea uwezo wa Mnyororo wa Thamani Wakulima wa Mwani na Jongoo Bahari, elimu inayotolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Mradi wa Utekelezaji wa Rasilimali za Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji (TASFAM), katika Kata ya Manza, Kijiji cha Tawalani, Machi 28, 2026 Mkinga - Tanga.

Afisa Ushirika wa Wilaya ya Mkinga, Bw. Jumanne Maziku (aliyesimama), akielezea umuhimu wa Wakulima wa Mwani na Jongoo Bahari kujiunga kwenye vyama vya Ushirika, wakati wa zoezi la kuwajengea uwezo wa Mnyororo wa Thamani Wakulima wa Mwani na Jongoo Bahari, elimu inayotolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Mradi wa Utekelezaji wa Rasilimali za Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji (TASFAM), katika Kata ya Manza, Kijiji cha Tawalani, Machi 28, 2026 Mkinga - Tanga.

Maafisa wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakiwa katika picha ya pamoja na wakulima wa Mwani na Jongoo Bahari, baada ya zoezi la kuwajengea uwezo wa Mnyororo wa Thamani Wakulima wa Mwani na Jongoo Bahari, elimu inayotolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Mradi wa Utekelezaji wa Rasilimali za Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji (TASFAM), katika Kata ya Manza, Kijiji cha Tawalani, Machi 28, 2026 Mkinga - Tanga.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

LESENI, VIBALI VYA MAZAO YA MIFUGO NA VYAKULA VYA SAMAKI KUTOLEWA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI

DKT. MHEDE AONGOZA ZOEZI LA UCHANJAJI WA MIFUGO MKOANI IRINGA, WAFUGAJI WAPONGEZA HATUA YA SERIKALI

SERIKALI KURASIMISHA BIASHARA YA MABONDO