WANUFAIKA WA TASFAM MTAMA WAHIMIZWA KUTUMIA KANUNI BORA ZA UKUZAJI VIUMBE MAJI
Na. Martha Mbena.
Wanufaika wa Mradi wa kuendeleza na kusimamia Uvuvi wa Baharini na Ukuzaji Viumbe Maji (TASFAM) wa Wilaya ya Mtama mkoani Lindi wamehimizwa kutumia kanuni bora za Ukuzaji Viumbe maji.
Akizungumza wakati wa kutoa Elimu kuhusu kanuni ya Viumbe maji Machi 28,2026, Afisa Uvuvi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bw. Justine Ndayeze, amewasisitiza wanufaika hao wasifanye shughuli pasipo kufuata kanuni bora, sheria na taratibu za Ukuzaji viumbe maji ili kuweza kufanya shughuli hizo kwa Uhuru bila kuvunja sheria.
"Tusifanye shughuli kimya kimya bila kufanya taratibu zote zilizowekwa na Wizara za Ufugaji na Ukuzaji viumbe maji", Amesema Bw. Ndayeze.
Aidha, Ndayeze ameongeza kusema kuwa kanuni inasisitiza kufuata kanuni kwa kufuata taratibu zote za kutunza mazingira ya viumbe maji, kupata mbegu bora, kukata vibali vya kusafirisha mazao ya uvuvi na kuwa na kumbukumbu za shughuli za ufugaji.
Kwa upande wake Mnufaika wa mafunzo hayo Bw. Hassan Namkanda wa kata ya Shuka, Wilaya ya Mtama, Mkoani Lindi ameipongeza Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kuwaletea mafunzo ya ufugaji Ukuzaji viumbe maji na elimu ya kanuni bora kwa Wilaya ya Mtama kwani wanaahidi kufuata sheria na kanuni zote zilizowekwa na Wizara hiyo.



Maoni
Chapisha Maoni