SHILINGI BIL. 30.7 KUWANUFAISHA VIJANA PROGRAMU YA BBT

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Ng’wasi Kamani amesema serikali inaendelea kutekeleza Programu ya Jenga Kesho Iliyobora (Building Better Tomorrow - BBT) ambapo katika mwaka wa fedha 2025/2026 wizara hiyo imepokea shilingi bilioni 30.7 (Sekta ya uvuvi shilingi bilioni 25.9 na sekta ya mifugo shilingi  bilioni 4.75) kwa ajili ya kuwawezesha wavuvi wadogo pamoja na vijana katika maeneo mbalimbali hapa nchini. 

Mhe. Kamani amesema hayo leo Aprili 10, 2026 Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Vitimaalum, Mhe. Maryam Azan Mwinyi, kwenye Kipindi cha Maswali na Majibu cha Bunge la 13, Mkutano wa Tatu, Kikao cha Sita.

Swali la Mbunge huyo lilihoji hatua inayochukuliwa na serikali kuwawezesha Wananchi hususani Vijana na Wavuvi wadogo kushiriki kikamilifu katika uchumi wa Bluu.

“ Mheshimiwa Spika, Kupitia programu ya BBT, vijana 308 wamepatiwa mikopo isiyo na riba na yenye masharti nafuu kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya ufugaji wa samaki kwenye vizimba, ufugaji wa majongoo bahari, unenepeshaji kaa na kilimo cha mwani” alisema Mhe. Kamani 

Aidha, ameongeza kuwa, Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) inaendelea kutekeleza zoezi la utoaji wa mikopo isiyo na riba na yenye masharti nafuu kwa wavuvi wadogo wakiwemo vijana kwa kuwawezesha kupata nyenzo za uvuvi zikiwemo maboti ya kisasa pamoja na nyavu za uvuvi.


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

LESENI, VIBALI VYA MAZAO YA MIFUGO NA VYAKULA VYA SAMAKI KUTOLEWA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI

DKT. MHEDE AONGOZA ZOEZI LA UCHANJAJI WA MIFUGO MKOANI IRINGA, WAFUGAJI WAPONGEZA HATUA YA SERIKALI

SERIKALI KURASIMISHA BIASHARA YA MABONDO