DKT. BASHIRU AAGIZA PROGRAMU YA AFDP KUFANYIWA TATHMINI

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa leo Aprili 2, 2026 amepokea taarifa ya Utekelezaji wa Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) kwa kipindi cha Julai 2022- Machi 2026 inayotekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na Mfuko wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), kikao kilichofanyika Ofisi ndogo za wizara zilizopo Kambarage Tower, jijini Dodoma.

Programu hiyo inayojikiza kuongeza tija na faida katika mbegu za kilimo, Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji, Kuboresha upatikanaji wa masoko, kuongeza thamani ya mazao pamoja na kuendeleza sekta binafsi, inagharimu kiasii cha dola za marekani milioni 77.416 ulianza kutekelezwa Julai 2021 na utakamilika Desemba 2027.

Pamoja na mambo mengine, baada  ya kupokea taarifa hiyo Mhe. Balozi Dkt. Bashiru ameielekeza timu ya wataalam inayotekeleza programu hiyo kutoka wizarani kutathmini kwa kina sababu zilizochelewesha mradi huo hususani mchakato wa zabuni.

Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) inatarajiwa kunufaisha kaya 260,000 ambapo takribani watu milioni 1.3 wakiwemo wakulima, wazalishaji wadogo na wakati wa mbegu na pembenjeo za kilimo, wavuvi wadogo, wachakataji wa mazao ya uvuvi, wakuzaji viumbe maji na wachakataji wa mwani kutoka halmashauri 46 za  mikoa 12 ya Tanzania Bara na Zanzibar watanufaika.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa akizungumza na Timu ya Wataalam inayoratibu Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) kutoka Wizarani wakati akipokea taarifa ya utekelezaji wa programu hiyo, kikao kilichofanyika Aprili 2, 2026 Kambarage Tower, Dodoma.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Ng’wasi Kamani akichangia hoja wakati wa kikao cha Waziri wa Mifugo na Uvuvi pamoja na Timu ya Wataalam inayoratibu Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) kutoka Wizarani, kikao kilichofanyika Aprili 2, 2026 Kambarage Tower, Dodoma.

Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, ambaye ni Naibu Katibu (Mifugo) Dkt. Fabian Madele akitoa ufafauni wa baadhi ya hoja zilizoibuliwa wakati kikao cha Waziri cha kupokea taatifa ya utekelezaji wa Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP), kilichofanyika Aprili 02, 2026 Kambarege Tower, Dodoma.



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

LESENI, VIBALI VYA MAZAO YA MIFUGO NA VYAKULA VYA SAMAKI KUTOLEWA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI

DKT. MHEDE AONGOZA ZOEZI LA UCHANJAJI WA MIFUGO MKOANI IRINGA, WAFUGAJI WAPONGEZA HATUA YA SERIKALI

SERIKALI KURASIMISHA BIASHARA YA MABONDO