PROF. SHEIKH ATEMBELEA KIWANDA CHA KUCHAKATA MWANI TANI 30, 000 ZANZIBAR
Kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Naibu Katibu Mkuu ( Uvuvi) Prof. Mohamed Ali Sheikh ametembelea Kiwanda na kukagua cha Kuchakata Zao la Mwani kilichoko Kisiwani Pemba katika ziara aliyoifanya Aprili 02, 2026 lengo ikiwa ni kuimarisha ushirikiano katika kuendeleza na kukuza uchumi wa buluu nchini.
Kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuchakata tani 30,000 za mwani kwa mwaka na kitazalisha mbolea, chakula cha wanyama hasa ng'ombe na carageenan.
Katika ziara hiyo Prof. Sheikh aliambatana na Meneja wa Kiwanda pamoja na Afisa Mdhamini Wizara ya Uchumi wa Buluu Zanzibar.

Maoni
Chapisha Maoni