PROF. SHEIKH AWATAKA IUCN KUZINGATIA VIPAUMBELE VYA WIZARA KATIKA UTEKELEZAJI WA MRADI
Na. Stanley Brayton Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Prof. Mohammed Ali Sheikh amelitaka Shirika la Kimataifa wa Uhifadhi wa Mazingira (IUCN) kuzingatia vipaumbele vya Wizara katika utekelezaji wa Mradi wa Pamoja Tuhifadhi Bahari Yetu ili kuleta tija katika Sekta ya Uvuvi. Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, wakati wa Kikao cha kupitia Mradi wa Pamoja Tuheshimu Bahari Yetu unaoratibiwa na ICUN na kutekelezwa na Wizara za Kisekta na Taasisi zisizo za kiserikali, leo Machi 2, 2026 Mkoani Morogoro, Prof. Sheikh amewataka IUCN kuzingatia vipaumbele vya Wizara katika utekelezaji wa Mradi huo. "ni vyema ICUN kufuata Miongozo na Taratibu za Wizara katika kutekeleza Mradi kwa kuchangia katika Mkakati wa Mageuzi wa Sekta ya Uvuvi na Ukuzaji Viumbemaji kwa mwaka 2026/2050, na programu zenu zilenge kwenye kufanya Mageuzi katika Sekta ya Uvuvi.” amesema Prof. Sheikh Vilevile, Prof. Sheikh amesema kwa sasa Wizara inataka kufanya Mageuzi kat...