KINGOLWIRA INAFAA KUWA KITUO KIKUBWA CHA UKUZAJI VIUMBEMAJI NCHINI - PROF. SHEIKH

Na. Stanley Brayton

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Prof. Mohammed Ali Sheikh amesema  Kituo cha Ukuzaji Viumbemaji cha Kingolwira kinafaa kuwa Kituo kikubwa na cha Kitaifa cha Ukuzaji Viumbemaji nchini kwani kina Miundombinu nyinyi ambaazo zinajengwa na za kisasa.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, alipotembelea Kituo cha Ukuzaji Viumbemaji cha Kingolwira kwa ajili ya kukagua Miundombinu na Uzalishaji, leo Machi 2, 2026 Mkoani Morogoro, Prof. Sheikh amesema Kituo kinazalisha vifaranga 600,000 kwa mwaka ikiwa kuna Vizimba 6 tu.

"kwa hiyo ni vyema kuharakisha kujenga Miundombinu nyingine haraka hili kuweza kuzalisha vifaranga vya Samaki zaidi ili wananchi wape kufuga.” amesema Prof. Sheikh

Aidha, Prof. Sheikh amesema Mradi huo wa Ukuzaji Viumbemaji wa Kingolwira unaendelea kuboreshwa zaidi kwa kutengeneza Vizimba vingine na Miundombinu nyingine ambazo zitakuwa zinazalisha vifaranga kwa wingi.

Vilevile, Prof. Sheikh amewataka Wataalam wa Kituo cha Ukuzaji Viumbemaji cha Kingolwira kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha vifaranga wanapatika kwa wingi na wenye ubora.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Prof. Mohammed Ali Sheikh (wa tano kushoto), akitoa maelekezo kwa Maafisa wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na watumishi wa Kituo cha Ukuzaji Viumbemaji cha Kingolwira, mara baada ya kukagua Miundombinu ya Kituo hicho, Machi 2, 2026 Morogoro.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Prof. Mohammed Ali Sheikh (wa kwanza kushoto), akikagua Miundombinu ya Mabwawa ya Mradi wa Kituo cha Ukuzaji Viumbemaji cha Kingolwira, mara baada ya kuwasili katika Kituo hicho, Machi 2, 2026 Morogoro.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Prof. Mohammed Ali Sheikh (wa pili kushoto), akikagua Maendeleo ya Ujenzi wa Kituo cha Ukuzaji Viumbemaji cha Kingolwira, mara baada ya kuwasili katika Kituo hicho, Machi 2, 2026 Morogoro.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Prof. Mohammed Ali Sheikh (wa kwanza kulia), akikagua teknolojia ya Uzalishaji wa nzi chuma ambao ni chakula cha kulishia Samaki, mara baada ya kuwasili katika Kituo hicho, Machi 2, 2026 Morogoro.

Picha ni muonekano wa Miundombinu ya Vizimba na mabwawa ya kufugia samaki, yaliyopo katika Kituo cha Ukuzaji Viumbemaji Kingolwira, Machi 2, 2026 Morogoro.


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

LESENI, VIBALI VYA MAZAO YA MIFUGO NA VYAKULA VYA SAMAKI KUTOLEWA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI

DKT. MHEDE AONGOZA ZOEZI LA UCHANJAJI WA MIFUGO MKOANI IRINGA, WAFUGAJI WAPONGEZA HATUA YA SERIKALI

SERIKALI KURASIMISHA BIASHARA YA MABONDO