DKT. BASHIRU ASHANGAZWA NA WABUNGE WANAOTETEA UVUVI HARAMU NCHINI
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakukrwa amesema kwa sasa serikali haita chukua hatua za kufunga Ziwa Victoria na badala yake itawafungia wavuvi na wale wote watakaobainika kujihusisha na uvuvi haramu.
Dkt. Bashiru amesema hayo Februari 28, 2026 baada ya kushuhudia nyavu haramu zilizokamatwa na timu ya elimu kwa vitendo kuhusu uvuvi haramu kwa vitendo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Kituo cha Rubambagwe Wilayani Chato Mkoa wa Geita.
Aidha, Balozi Dkt. Bashiru ameshangazwa na baadhi ya wabunge na madiwani kuwa mstari wa mbele kutetea uvuvi haramu ambapo amesema kitendo hicho sio cha kiungwana.

Maoni
Chapisha Maoni