Wakala ya Mafunzo ya Mifugo nchini (LITA) imeungana na Taasisi nyingine zilizopo chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuongeza hamasa kwa timu za Wizara hiyo zinazoshiriki michuano ya SHIMIWI inayoendelea jijini Mwanza kwa kutoa mchango wa Jezi zitakazotumiwa na timu mchezo wa kuvuta kamba upande wa wanaume.
Akizungumza mara baada ya kupokea Jezi hizo Mwenyekiti wa SHIMIWI Wizarani hapo Bw. Sebastian Shilangalila amesema kuwa jezi hizo zimeiongezea timu hiyo morali ya kupambana na kuhakikisha inaibuka na ushindi kwenye michezo yao yote iliyosalia.
“Mchango unaotolewa na Taasisi zetu kwa kweli unatupa hamasa kubwa ya kupambana huku tulijua hatuko peke yetu kwenye mapambano haya hivyo niwashukuru sana LITA kwa mchngo huu na sisi kama timu tunaahidi tutaendelea kupambana mpaka tone la mwisho la jasho letu” Amesema Bw. Shilangalila.
Mchango huo unakuja siku chache baada ya Taasisi za Wakala ya Maabara ya veterinari nchini (TVLA), Mamlaka ya kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu (DSFA) kutoa sare na vifaa mbalimbali kwa timu hiyo ili inayoendelea kufanya vema kwenye michezo mbalimbali ya michuano hiyo.



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni