Nav bar

Jumatano, 22 Januari 2025

SERIKALI KUIMARISHA MIKAKATI YA KUKUZA SHUGHULI ZA UKUZAJI VIUMBE MAJI ZIWA TANGANYIKA

Na. Stanley Brayton

Serikali imeendelea kufanya juhudi za kuimarisha na kuweka mikakati bora ya kukuza shughuli za Ukuzaji Viumbe maji kupitia vizimba vya kufugia samaki ambapo njia hii inalenga kuboresha zaidi Uzalishaji  wa Samaki na kukuza shughuli za uchumi kwa wananchi na kufungua fursa za uchumi.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara  ya Mifugo na Uvuvi, leo Januari 22, 2025 mkoani Dodoma katika Mkutano wa kujadili ni namna gani ya kuimarisha Tasnia ya Ukuzaji Viumbe Maji kwa njia ya Vizimba na mashirikiano baina ya Wizara na Shirika la Uhifadhi wa Mazingira "The Nature Conservancy" pamoja na Taasisi zingine, Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Viumbe Maji, Dkt. Nazael Madalla amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alielekeza Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuhakikisha inahamasisha na kuendelea Ufugaji Samaki kwa njia ya Vizimba katika maeneno yote yanayofaa kiufugaji.

"hapa nchini kwetu Ziwa Tanganyika ni moja ya maeneo ambayo kuna fursa ya Ufugaji Samaki kwa njia ya Vizimba, na tumekutana hapa na wadau mbalimbali wa Ufugaji Samaki kwa njia ya Vizimba kutoka ndani ya nchi na nje ya nchi kwa ajili ya kujadili ni namna gani tutawezesha Ufugaji huu kwa jamii inayozunguka Ziwa Tanganyika, na kukubaliana kwa mikakati kuhakikisha kwamba kunakuwa na uwezeshaji pamoja na ulinzi  wa mazingira na utunzaji wa mazingira hayo ili kuleta faida nchini." amesema Dkt. Madalla

Aidha, Dkt. Madalla amesema serikali imekuwa ikifanya juhudi katika kukuza Tasnia ya Ukuzaji Viumbe Maji kwani tayari ilishapeleka Vizimba katika Ziwa Tanganyika na jana Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji alikwenda kutembelea Vizimba hivyo ambavyo vipo katika eneo la Katavi ambavyo wafugaji tayari walishaanza kufuga na Samaki wanaendelea vizuri kiasi cha kuwatia moyo wafugaji hao.

Vilevile Dkt. Madalla amesema Serikali kupitia Wizara inaendelea na zoezi la kutoa mafunzo kwa wavuvi juu ya Ufugaji Samaki kwa njia ya Vizimba, kutoa mikopo ya pembejeo,  kuendeleza maeneo ya Ufugaji,  kuanza Taratibu za kuanzisha Kituo cha Ukuzaji Viumbe Maji katika Ziwa Tanganyika, pamoja na kuhamasisha na kuwezesha Sekta Binafsi ili kuwekeza katika Uzalishaji na usambazaji wa pembejeo za Ufugaji Samaki.

Dkt. Madalla amesema kuwa kwa sasa mwitikio wa wananchi kufuga samaki kwa njia ya vizimba umeanza kuongezeka kutokana na serikali kuweka mazingira rafiki ikiwemo mikopo ambayo imekuwa ikiwanufaisha sana wafugaji wengi na baaadhi ya wadau katika Sekta wameainisha ni kwa namna gani ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba ulivyokuwa na tija kubwa kiuchumi kwani kwa sasa wananufaika sana kutokana na mradi huo.

Naye, Mkurugenzi wa Uvuvi kutoka Mamlaka ya Ziwa Tanganyika (LTA), Bi. Nyakorema Beatrice Marwa, amesema warsha hii inatija kubwa sana kwa sababu imekusanya wadau mbalimbali wa Tasnia ya Ukuzaji Viumbe  Maji toka Taasisi za Serikali na Binafsi na wadau wa Ziwa Tanganyika na lengo kutaka kuanda Mpango wa Utekelezaji kwa pamoja ambao haukizani na Sheria zetu na za nchi nne zinazozunguka Ziwa Tanganyika.

Pia, Meneja wa Mradi wa Ziwa Tanganyika wa Shirika la Uhifadhi wa Mazingira "The Nature Conservancy" (TNC), Bw. Fridolin Nzambimana amesema kuwa TNS wanachokifanya ni kuimarisha mashirikiano baina yao na serikali pamoja na Taasisi nyingine ili kuendeleza na kukuza Tasnia ya Ukuzaji Viumbe maji kwa njia ya kutumia Vizimba na ambayo inalinda rasilimalinza Uvuvi.

Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Viumbe Maji, Dkt. Nazael Madalla, akielezea kwa kutumia projekta (haipo pichani) Malengo, Sheria, Kanuni na Taratibu za Serikali na Wizara katika Ukuzaji Viumbe Maji kwa njia ya Vizimba, ni katika Mkutano wa kujadili ni namna gani ya kuimarisha Tasnia ya Ukuzaji Viumbe Maji kwa njia ya Vizimba na mashirikiano baina ya Wizara na Taasisi ya Uhifadhi wa Mazingira "The Nature Conservancy" pamoja na Taasisi zingine, kilichofanyika katika Ukumbi wa Morena, Januari 22, 2025, Dodoma.
Mkurugenzi wa Ukuzaji Viumbe Maji Shirika la Uhifadhi wa Mazingira "The Nature Conservancy", Bw. Taylor Voortees, akielezea shughuli zinazofanywa na TNC, ni katika Mkutano wa kujadili ni namna gani ya kuimarisha Tasnia ya Ukuzaji Viumbe Maji kwa njia ya Vizimba na mashirikiano baina ya Wizara na Shirika la Uhifadhi wa Mazingira "The Nature Conservancy" pamoja na Taasisi zingine, kilichofanyika katika Ukumbi wa Morena, Januari 22, 2025, Dodoma.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) Dkt. Ismael Kimirei, akiwasilisha hoja, ni katika Mkutano wa kujadili ni namna gani ya kuimarisha Tasnia ya Ukuzaji Viumbe Maji kwa njia ya Vizimba na mashirikiano baina ya Wizara na Shirika la Uhifadhi wa Mazingira "The Nature Conservancy" pamoja na Taasisi zingine, kilichofanyika katika Ukumbi wa Morena, Januari 22, 2025, Dodoma.
Mratibu wa Ukuzaji Viumbe Maji Ukanda wa Ziwa Tanganyika -Shirika la Uhifadhi wa Mazingira, Dkt. Imani Kapinga ,akiwasilisha hoja, ni katika Mkutano wa kujadili ni namna gani ya kuimarisha Tasnia ya Ukuzaji Viumbe Maji kwa njia ya Vizimba na mashirikiano baina ya Wizara na Shirika la Uhifadhi wa Mazingira "The Nature Conservancy" pamoja na Taasisi zingine, kilichofanyika katika Ukumbi wa Morena, Januari 22, 2025, Dodoma.
Picha ni sehemu ya wadau wa Ukuzaji Viumbe Maji, wakiwa katika Mkutano wa kujadili ni namna gani ya kuendeleza Tasnia ya Ukuzaji Viumbe Maji kwa njia ya Vizimba na mashirikiano baina ya Wizara na Taasisi ya Uhifadhi wa Mazingira "The Nature Conservancy" pamoja na Taasisi zingine, kilichofanyika katika Ukumbi wa Morena, Januari 22, 2025, Dodoma.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Viumbe Maji, Dkt. Nazael Madalla (mstari wa mbele katikati), akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa Ukuzaji Viumbe Maji, ni katika Mkutano wa kujadili ni namna gani ya kuendeleza Tasnia ya Ukuzaji Viumbe Maji kwa njia ya Vizimba na mashirikiano baina ya Wizara na Taasisi ya Uhifadhi wa Mazingira "The Nature Conservancy" pamoja na Taasisi zingine, iliyofanyika katika Ukumbi wa Morena, Januari 22, 2025, Dodoma.










Hakuna maoni:

Chapisha Maoni