Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe amezindua bweni la wanafunzi wa kike katika chuo cha Wakala ya Mafunzo ya Mifugo (LITA) kampasi ya Morogoro lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 216 lililogharimu zaidi ya shilingi milioni 970 fedha za mapato ya ndani
Akizungumza baada ya
kuzindua jengo hilo Aprili 06,2024, Prof
Shemdoe ameipongeza LITA kwa kufanikisha ujenzi huo kwa kutumia fedha za ndani
ambapo kukamilika kwakwe kutasaidia kwa kiasi kikubwa kuondokana na changamoto
ya mabweni kwa wanafunzi katika kampasi hiyo
Prof. Shemdoe alisema kuwa
Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi inaendela kufanya jitihada za
makusudi katika kuboresha miundombinu katika kampasi zote nane za LITA ambazo
kwa sasa kila kampasi inaendelea na ujenzi wa miundombinu mbalimbali pamoja na
ukarabati wa majengo chakavu
“Bajeti ya mwaka 2024/2025
imezingatia sehemu ya vipaumbele muhimu vinavyolenga kutatua changamoto
zilizopo kwa awamu ili kuiwezesha Wakala kuwa na uwezo wa kudahili na kutoa
mafunzo bora kwa vijana na wafugaji, Wizara itaendelea kuwaunga mkono hasa kwa
kuendelea kuchangia fedha za maendeleo.” Alisema Prof. Shemdoe
Awali akitoa taarifa ya
ujenzi wa bweni hilo Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Mafunzo ya Mifugo (LITA) Dkt
Pius Mwambene, amesema kuwa ujenzi huo
umetumia miaka miwili hadi kukamilika ambapo kwa sasa wameanza kwa kujenga
bweni la wanawake na kisha baadaye watahamia kwenye ujenzi bweni la wanaume
Amesema hatua hiyo ni
miongoni mwa jitihada zinazofanywa na Wakala katika kutatua changamoto ya miundombinu
ya kufundishia ambayo itawawezesha wanafunzi na watumishi kutekeleza majukumu
yao wakiwa katika mazingira bora
“Bweni hili limetimiza
takribani miaka miwili na sasa lipo tayari kutumika ambapo tumetumia shilingi
970,388,312 fedha ambazo zimetoka katika mapato ya ndani ya taasisi yetu,
lakini pia pamoja na mafanikio haya zipo changamoto chache tuomba msaada
ikiwemo uhaba wa usafiri ususani mabasi ili kuwezesha wanafunzi kujifunza kwa
vitendo nje ya kampasi zao” alisema Dkt. Mwambene
Naye Mkurugenzi wa Utafiti,
Mafunzo na Ugani kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Angello Mwilawa amesema
Wakala inaendelea kujiandaa na utekelezaji wa mtaala mpya wa kufundishia ambao
unatarajiwa kuanza kutumika mwaka mpya wa masomo mwezi octoba mwaka huu ambapo mpaka
sasa wadau wawili wameshajitokeza kusadia
Amesema mtaala wa sasa
unatarajiwa kufikia tamati mwezi april mwaka huu na kutoa nafasi ya kuhuisha
mitaala mipya ambapo wadau waliojitokeza katika kusaidia uhuishaji wa
mitaala hiyo ni pamoja na shirika la kilimo
endelevu (Sustainable Agriculture Tanzania (SAT)
Katibu Mkuu Wizara ya
Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe akiongea wakati wa ufunguzi wa kikao cha
11 cha Baraza kuu la Wafanyakazi la Wakala ya Mafunzo ya Mifugo (LITA) katika
Kampasi ya Morogoro, Aprili 06,2024
Mtendaji Mkuu wa Wakala ya
Mafunzo ya Mifugo (LITA) Dkt. Pius Mwambene akitoa neno la utangulizi mara
baada ya uzinduzi wa bweni la Wasichana na wakati wa kikao cha 11 cha baraza
kuu la wafanyakazi wa Wakala ya Mafunzo ya Mifugo (LITA) katika kampasi ya
Morogoro , Aprili 06,2024
Katibu Mkuu Wizara ya
Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe (wa tatu kutoka kushoto) akikata utepe
ishara ya uzinduzi wa Bweni la wasichana lililopo kwenye Wakala ya mafunzo ya
Mifugo (LITA) kampasi ya Morogoro Aprili 06,2024
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni