Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Julai, 2023

ULEGA AZUNGUMZA NA WANANCHI WA KIJIJI CHA RUTORO WILAYANI MULEBA MKOANI KAGERA KWA AJILI YA KUTATUA MGOGORO

Picha
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akiongea na Wananchi wa Kijiji cha Rutoro (hawapo pichani) wakati wa ziara ya Mawaziri Nane wa Kisekta iliyolenga kutatua mgogoro katika Kijiji hicho cha Rutoro Wilayani Muleba, Mkoani Kagera Julai 20, 2023. Timu hiyo ya Mawaziri nane iliongozwa na Mwenyekiti, ambaye ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt. Angeline Mabula. Mawaziri wengine walioshiriki katika ziara hiyo ni Naibu wa Waziri wa Kilimo, Mhe. Antony Mavunde, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja na Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe. Khamis Hamza Chillo.

KATIBU MKUU WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI AMEFANYA KIKAO NA UONGOZI WA GIZ NCHINI TANZANIA.

Picha
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe leo tarehe 19Julai,2023 jijini Dar es Salaam amekutana na Uongozi wa Shirika la Misaada la ujerumani (GIZ) na kufanya kikao na Uongozi wa GIZ Tanzania pamoja na  Uongozi wa Hifadhi za Bahari na maeneo Tengefu (MPRU), TAFICO pamoja na maafisa wengine wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi. Lengo la Kikao hicho ni kumjulisha Katibu Mkuu kuhusu mradi wa “Transboundary conservation and sustainable management of coastal and marine biodiversity" utakaofadhiliwa na Serikali ya ujerumani kupitia shirika lake la Misaada la (GIZ)  kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya.  Aidha, Mradi huo wa “Transboundary conservation and sustainable management of coastal and marine biodiversity, utatekelezwa katika maeneo ya Kwale Tanga,Tanzania,pamoja na Kenya. Vilevile, Mradi huo utakuwa na shughuli nyingi ikiwemo uhifadhi wa mazingira, uchumi na kuongeza uwezo na  maendeleo kwa jamii ya Kitanzania. Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riz...

KATIBU MKUU WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI AFUNGUA KIKAO CHA KWANZA CHA "OCEAN INNOVATION HUB" JIJINI DAR ES SALAAM.

Picha
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof.Riziki Shemdoe Jana tarehe 18 Julai, 2023 alifungua kikao cha kwanza cha kuanzisha TANZANIA OCEAN INNOVATIO HUB chini ya Marine Park Reserve Unit (MPRU) kwa kushirikiana  na Early Carrier Ocean Professionals (ECOP). Aidha, lengo la kikao hicho ni kuwafanya vijana wawe sehemu ya wanufaikaji wa fursa za bahari na watatuzi wakuu wa changamoto za matumizi ya bahari.  Pamoja na mambo mengine, Mhe. Maryvonne Pool, Balozi wa Seychelles nchini Tanzania alishiriki kikamilifu katika kikao hicho cha kwanza pamoja na washiriki wengine 30. Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof.Riziki Shemdoe, akisalimia na Balozi wa Seyshelles  Mhe.Maryvonne Pool, mara baada ya kumaliza kikao cha kwanza cha kuanzisha Tanzania Ocean Innovation Hub kilichofanyika jana tarehe 18July 2023 Jijini Dar es Salaam. Picha mbalimbali za Washiriki wa kikao cha kwanza cha Tanzania Ocean Innovation Hub Kilichofanyika Jana tarehe 18 July 2023 jijini Dar es Salaam. Leng...

WADAU WA MAENDELEO WAUNGA MKONO BBT

Picha
Taasisi ya Kimataifa ya Heifer imeendelea kuunga mkono jitihada za Serikali ya  Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwawezesha vitendea kazi vijana wanaofanya shughuli za unenepeshaji wa mifugo katika kituo cha Mabuki kilichopo Wilayani Misungwi, Mkoani Mwanza Julai 18, 2023. Akiongea na vijana katika hafla fupi ya kupokea vitendea kazi hivyo ikiwemo Lori moja na pikipiki Nne, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega aliwashukuru Wadau hao wa Heifer huku akisema kitendo hicho ni uungaji mkono jitihada za Mhe Rais Samia za kuwawezesha vijana na kina mama kujiajiri na kukuza kipato chao kupitia programu ya BBT Mifugo na Uvuvi. Alisema kuwa Dkt. Samia anataka kuifanya programu hiyo ya BBT  kuwa ya kielelezo ambapo vijana wengi waweze kujikomboa kwa kujiajiri kupitia shughuli za Kilimo, Mifugo na Uvuvi. Aliongeza kwa kusema kuwa ni wakati sasa kwa vijana hao kuanza kufanya ubunifu wa kufanya biashara yao hiyo kidigitali kupitia mifumo ya biashara mtandao ili kupunguza kutegem...

PROF. SHEMDOE AONGOZA KIKAO KAZI CHA KUPITIA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA MWAKA 2022/2023

Picha
  Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe akitoa maelekezo wakati Kikao kazi cha kupitia utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2022/2023 kilichofanyika mkoani Morogoro kwenye ukumbi wa Hoteli ya Morena. (15.07.2023) Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Dkt. Daniel Mushi (wa pili kutoka kushoto) akizungumza wakati Kikao kazi cha kupitia utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2022/2023 kilichofanyika mkoani Morogoro kwenye ukumbi wa Hoteli ya Morena. (15.07.2023) Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Bi. Agnes Meena (wa kwanza kulia) akizungumza wakati Kikao kazi cha kupitia utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2022/2023 kilichofanyika mkoani Morogoro kwenye ukumbi wa Hoteli ya Morena. (15.07.2023) Wakuu wa Idara na Vitengo wakiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Manaibu Makatibu Wakuu wakifuatilia wasilisho la utekelezaji wa bajeti lililowasilishwa na Bi. Danietta Tindamanyire. Kikao kimefanyika mkoani Morogoro kwenye ukumbi wa Hoteli y...

PROF. SHEMDOE AFUNGUA KIKAO KAZI CHA KUPITIA RASIMU YA ANDIKO LA MRADI WA UWEKEZAJI ENDELEVU KATIKA SEKTA YA MIFUGO

Picha
  Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe akichangia mada baada ya wasilisho kutoka kwa wawakilishi kutoka Benki ya Dunia wakati wa Kikao kazi cha kupitia rasimu ya andiko la mradi wa uwekezaji endelevu katika Sekta ya Mifugo nchini Tanzania kutoka Benki ya Dunia kinachofanyika mkoani Mrorogoro kwenye ukumbi wa Hoteli ya Morena. (14-15.07.2023) Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Dkt. Daniel Mushi, akiuliza swali wakati wa Kikao kazi cha kupitia rasimu ya andiko la mradi wa uwekezaji endelevu katika Sekta ya Mifugo nchini Tanzania kutoka Benki ya Dunia kinachofanyika mkoani Mrorogoro kwenye ukumbi wa Hoteli ya Morena. (14-15.07.2023) Afisa Mwandamizi wa Uchumi wa Kilimo kutoka Benki ya Dunia, Bi. Emma Isinika akiwasilisha mada wakati wa Kikao kazi cha kupitia rasimu ya andiko la mradi wa uwekezaji endelevu katika sekta ya mifugo nchini Tanzania kutoka Benki ya Dunia kinachofanyika mkoani Mrorogoro kwenye ukumbi wa Hoteli ya Morena. (14-15.07.20...

MAUZO YA NYAMA YAONGEZEKA NJE YA NCHI - ULEGA

Picha
  Serikali imesema, kiwango cha usafirishaji nyama hapa nchini kimeongezeka hadi kufikia tani 12,243.79 zenye thamani ya dola za Kimarekani milioni 51.894 ziliuzwa nje ya nchi 2022/23 ikilinganishwa na tani 1,774.20 zilizouzwa nje ya nchi 2020/21 . Hayo yamesemwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega julai 14,2023 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF 2023) ambao unatarajiwa kufanyika Septemba 5-9 mwaka huu jijini Dar es Salaam huku Rais Samia Suluhu Hassan akitarajiwa kuwa mgeni rasmi. Kwa mujibu wa Ulega ongezeko hilo ni moja ya jitihada zinazofanywa na Rais Samia na wizara yake inaziunga mkono kwa vitendo kupitia Programu ya BBT-LIFE ambapo katika awamu ya kwanza takribani vijana 738 wakiwemo vijana 238 kutoka sekta ya mifugo na vijana 500 kutoka sekta ya uvuvi wamenufaika na mafunzo ya unenepeshaji wa mifugo ,majongoo Bahari na ufugaji wa Samaki kibiashara. “Tumejipanga kuongeza uzalishaji Kufuat...

​PINDA AWATAKA WADAU WA MIFUGO NA UVUVI KUCHANGAMKIA FURSA

Picha
Na. Edward Kondela Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda amewataka wadau wa sekta za mifugo na uvuvi nchini kuchangamkia fursa zilizopo katika sekta hizo ili kujikwamua kiuchumi. Mhe. Pinda amezungumza hayo (12.07.2023) jijini Dodoma wakati wa mkutano wa wadau wa sekta za mifugo na uvuvi kuelekea mkutano mkuu wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Barani Afrika (AGRF) utakaofanyika hapa nchini kuanzia Septemba 4 hadi 8 mwaka huu. Amesema sekta hizo zimekuwa zikitoa mchango mkubwa katika familia ikihusisha akina mama na vijana na kwamba zikitumika vizuri zinaweza kubadilisha kwa kiasi kikubwa maisha katika ngazi ya familia na kuwataka wadau wa sekta hizo kuangalia fursa zitakazotokana na mkutano huo utakaofanyika Mwezi Septemba ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan atakuwa mwenyeji wa mkutano huo. Ameongeza kuwa amefurahishwa na programu maalum ya vituo atamizi ambapo Wizara ya Mifugo na Uvuvi inawajengea uwezo vijana katika kuwapatia mafunzo ya ufugaji b...

SERIKALI YAWEKA NGUVU KATIKA UTAFITI WA RASILIMALI ZA BAHARI NCHINI ILI KUWA NA UVUVI ENDELEVU

Picha
Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na Serikali ya Norway imepokea meli ya utafiti ya Dr. Fridtjof Nansen ambayo inafanya utafiti wa ikolojia ya Bahari na rasilimali za uvuvi zinazopatikana katika Bahari ya Hindi na kusaidia kuimarisha usimamizi wa Rasilimali za Bahari. Akiongea, katika hafla ya kuipokea rasmi meli hiyo katika Bandari ya Dar es salaam leo 11 Julai 2023, Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi wa Serikali ya Zanzibar, Mhe. Suleiman Makame, amesema utafiti huo unafanyika Tanzania Bara na visiwani (zanzibar) na utatoa taswira ya aina za samaki wanaopatikana  baharini kwa ajili ya kuweka mipango madhubuti ya usimamizi. Utafiti huo, umeanza kufanyika 28 Juni 2023 na utakamilika 28 Julai 2023.  "Tumekuwa tukifanya uvuvi bila kujua ni aina gani ya samaki na viumbe wengine wa Bahari tulionao, kwa hiyo tutakapokuwa na takwimu sahihi za rasilimali za samaki waliomo baharini tutaweka mkakati wa kudhibiti mazao ya baharini hasa aina za samak...

TAASISI ZATAKIWA KUTUMIA VYEMA MAPATO YA NDANI

Picha
Na. Edward Kondela Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Sekta ya Mifugo Dkt. Daniel Mushi ametoa rai kwa taasisi zilizo chini ya wizara hiyo kufanya kazi kwa bidii na kujijengea uwezo wa kujipatia vyombo vya kazi ili wafanye kazi kwa ufasaha. Dkt. Mushi amebainisha hayo (10.07.2023) wakati alipokuwa akizindua gari aina ya Toyota Hilux Pickup Double Cabin 2 GD STD Manual iliyonunuliwa na Bodi ya Nyama nchini (TMB) kwa thamani ya Shilingi Milioni 99.9. Akizungumza katika ofisi za bodi hiyo jijini Dodoma amesema ni vyema taasisi za Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuwa na matumizi mazuri ya fedha kwa kununua vifaa mbalimbali vya kutendea kazi badala ya kufanya matumizi ya fedha yasiyo na tija. Kwa upande wake Kaimu Msajili wa Bodi ya Nyama Bw. John Chassama amesema gari hilo wamenunua kwa mapato ya ndani ambapo wamepanga kulipeleka Kanda ya Arusha na kwamba mipango ni kuhakikisha kila kanda inakuwa na gari ili kuboresha utendaji kazi. Bw. Chassama amesema pamoja na ununuzi wa magari mpang...

MATUKIO MBALIMBALI WAKATI WA MAONYESHO YA 47 YA KIMATAIFA YA BIASHARA SABASABA

Picha
  Afisa Utafiti wa Mifugo Mkuu kutoka Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Dkt.  Scholastica Doto (kushoto) akielezea kazi zinazofanywa na Wakala  kwa Balozi wa Uturuki Nchini Tanzania Dkt. Mehmet Gu"lw"ogui (kulia) alipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya 47 ya kitaifa ya biashara sabasaba jijini Dar es salaam Julai 13,2023 Afisa Masoko kutoka kampuni ya SEAWEED, Bi. Sophia Mang'ena (kulia) akionyesha bidhaa walizonazo kwa   Balozi wa Uturuki Nchini Tanzania Dkt. Mehmet Gu"lw"ogui bidhaa walizonazo ikiwa ni pamoja na pilipili zinazopatikana kwenye kampuni hiyo alipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya 47 ya kimataifa ya biashara sabasaba jijini Dar es salaam Julai 13,2023 Mkurugenzi wa Kampuni ya NASHA Aquar Fish Bw. Masumbuko Nzingula (kulia) akieleza fursa za uwekezaji kwenye mnyororo wa thamani wa ufugaji samaki kwa Mkurugenzi wa Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kutoka Keshi la kujenga Tai...