Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (katikati) akiongea na uongozi wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD)(hawapo pichani) alipokutana nao kujadiliana kuhusu maandalizi ya mradi wa mabadiliko ya tasnia ya maziwa hususan kwa wafugaji wadogo na ng'ombe wa maziwa(SDTP). Waziri Ulega alikutana na uongozi huo jijini Dodoma Machi 2023. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Sekta ya Uvuvi), Bi. Agness Meena. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Sekta ya Mifugo), Dkt. Daniel Mushi.
Kiongozi wa ujumbe wa Taasisi ya Bergs and More kutoka nchini Italia, Bw. Hagay Maayan (kushoto) akimuonesha Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (kulia) mambo ambayo taasisi yao inashughulika nayo walipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma Machi 20, 2023.
Mkurugenzi wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo nchini Tanzania (IFAD), Bw. Robson Mutandi akimueleza Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (hayupo pichani) kuhusu maandalizi ya mradi wa mabadiliko ya tasnia ya maziwa hususan kwa wafugaji wadogo na ng'ombe wa maziwa(SDTP). Waziri Ulega alikutana na uongozi huo jijini Dodoma Machi 2023. Wengine katika picha ni Wataalam aliofuatana nao.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akiongea na Viongozi wa Taasisi ya Bergs and More kutoka nchini Italia (hawapo pichani) walipomtembelea ofisini kwake jijini DODOMA Machi 20, 2023. Uongozi huo ulifika ofisini kwa Waziri Ulega kujitambulisha na kuona namna wanavyoweza kushirikiana katika fursa mbalimbali zilizopo katika Sekta ya Mifugo na Uvuvi hususan tasnia ya Nyama.
Mkurugenzi wa Mradi wa TMPP kutoka Shirika la HEIFER INTERNATIONAL, Bw. Mark Tsoxo (wa pili kushoto) akieleza jambo wakati wa kikao cha kujadiliana kuhusu maandalizi ya mradi wa mabadiliko ya tasnia ya maziwa hususan kwa wafugaji wadogo na ng'ombe wa maziwa(SDTP) kilichofanyika jijini Dodoma Machi 20, 2023.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (katikati) akiongea na Viongozi wa Chama cha Wafugaji (CCWT) Tanzania walipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma Machi 20, 2023. Kulia ni Mwenyekiti wa CCWT, Bw. Murida Mushota. Viongozi hao walimtembelea Mhe. Waziri kujadiliana nae mambo mbalimbali yanayohusu Wafugaji nchini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni