Mkurugenzi wa shamba la SAMEKI, Bw. Meck Sadiki (kulia) akiwaonyesha na kutoa maelekezo ya sehemu wanayofanyia Uzalishaji wa samaki( Hatchery) wataalamu wa Uvuvi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, wakati walipoenda kuwatembelea vijana wa mafunzo ya uvuvi na Ukuzaji viumbe maji kwa Vitendo(Atamizi), Shamba hilo lililopo wilaya ya Sengerema, Mkoa wa Mwanza, Machi, 17.2023.
Kijana wa mafunzo ya uvuvi na Ukuzaji viumbe maji kwa Vitendo(Atamizi) Mwamisa Shabani, kwa niaba ya wenzake akionyesha jinsi ya ulishaji samaki kwenye mabwawa, ambapo vijana hao wanapata mafunzo ya Ufugaji Samaki kwa vitendo katika shamba la SAMEKI, lililopo Wilaya ya Sengerema, Mkoa wa Mwanza, Machi 17.2023.
Sehemu ya Muonekano wa shamba la SAMEKI, linalomilikiwa na Bw. Said Meck Sadiki ambapo vijana wa mafunzo ya uvuvi na Ukuzaji viumbe maji kwa Vitendo wanapata ujuzi kwa vitendo kupitia shamba hilo lililopo Wilaya ya Sengerema, Mkoa wa Mwanza, Machi,17.2023.
Picha ya pamoja ya wataalam kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Wizara ya Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu na vijana wanaopata mafunzo ya uvuvi na Ukuzaji viumbe maji kwa vitendo kwenye kituo cha SAMEKI kilichopo Wilaya ya Sengerema, Mkoa wa Mwanza mara baada ya kukagua na kunzungumza na vijana hao. Machi17,2023.
Vijana waliochaguliwa kwenye mafunzo ya uvuvi na Ukuzaji viumbe maji (Atamizi) wakifanya zoezi la kuvuna samaki kwenye vizimba (Fish cage) katika shamba la SAMEKI Lililopo kwenye ziwa Victoria Wilaya ya Sengerema, Mkoa wa Mwanza, Machi 17,2023.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni