Kaimu Mkurugenzi wa Uvuvi, akimuwakilisha Katibu Mkuu sekta ya Uvuvi, Bw. Steven Lukanga, (aliyesimama) akitoa neno la ukaribisho na kujitambulisha mbele ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki (Mb) (wapili kulia) na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (wa kwanza kulia) kwenye kikao cha kupitia mpango wa Usimamizi wa Rasilimali ya Kambamiti, kilichofanyika katika ukumbi wa NBC, Dodoma, 09.02.2023.
Sehemu ya wajumbe wakifatilia wasilisho la rasimu ya mpango wa usimamizi wa Rasilimali ya Kambamiti kutoka kwa Mwenyekiti wa kikosi kazi cha kitaifa kinachoratibu Muongozo wa kuendeleza Uvuvi mdogo Nchini Bw. Yahaya Mgawe (wa tano kulia) kwenye kikao kilichofanyika katika ukumbi wa NBC, Dodoma, 09.02.2023.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki (Mb) (katikati) akiendesha majadiliano kwenye kikao cha kupitia mpango wa Usimamizi wa Rasilimali ya Kambamiti, (kulia) ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb) na (kushoto) Kaimu katibu Mkuu wa sekta ya Uvuvi, Bw. Steven Lukanga na wataalamu wa sekta ya uvuvi (hawapo pichani) wakifatilia majadiliano hayo, kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Jengo la NBC, Dodoma, 09.02.2023.
Afisa Usimamizi Shirikishi wa Jamii kutoka Mwambao Coastal Community Network Tanzania (MCCNT), Bw. Edward Mlagala (aliyesimama) akitoa shukrani kwa niaba ya shirika hilo kwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi (hayupo pichani) kwa kuendelea kutoa mchango mkubwa kwenye ukanda wa pwani kwenye kikao cha kupitia mpango wa usimamizi wa Rasilimali ya Kambamiti kilichofanyika katika ukumbi wa NBC, Dodoma, 09.02.2023.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki, (Mb) ( wa katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wataalamu wa sekta ya Uvuvi waliohudhulia kikao cha kupitia mpango wa Usimamizi wa Rasilimali ya Kambamiti, na (kulia kwakwe) ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Abdallah Ulega (Mh), Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Mikutano NBC, Dodoma, 09.02.2023.
Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Viumbe Maji wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Nazael Madalla (aliyesimama) akichangia mada kwenye kikao cha kupitia mpango wa usimamizi wa Rasilimali ya Kambamiti mbele ya Waziri wa Mifugo na uvuvi (hayupo pichani) kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa mikitano NBC, Dodoma, 09.02.2023.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni