Nav bar

Jumamosi, 11 Juni 2022

​MFUMO WA KIELETRONIKI KUONGEZA TIJA NA UFANISI KATIKA KUSIMAMIA BIASHARA YA MIFUGO

Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na Taasisi ya Trade Mark East Africa (TMEA) inaendelea kutoa mafunzo ya mfumo wa kielektroniki wa usimamizi na utoaji vibali mbalimbali wa sekta ya mifugo uitwayo (MIMIS)  utaongeza tija na Ufanisi kwenye kusimamia biashara ya mifugo.


Hayo yamesemwa na Afisa Mifugo mfawidhi wa Kituo cha  ZVC Tabora, Bi. Adelina Mkumbukwa wakati akifungua mafunzo hayo yaliyofanyika 07 june 2022, katika ukumbi wa Gold Crest Hotel jijini Mwanza.


"Niwaombe mfuatilie kwa makini mafunzo haya ili tuwe na uelewa wa pamoja juu ya namna mfumo utakavyokwenda kuboresha mazingira ya ufanyaji wa biashara kwa sekta ya mifugo" amesema Mkumbukwa.


Bi Mkumbukwa amesema mfumo utasaidia kuwezesha wadau kufatilia kibali husika namna kinavyofanyiwa kazi na wizara itakapofikia sehemu ya kufanya malipo, ambapo mdau atapata "control number" kwenye dirisha lake au kupitia ujumbe mfupi wa maneno (sms) kwenye simu yake.


Naye Daktari  kutoka bodi ya nyama kanda ya Ziwa, Dkt. Anthony Msomi  amesema  mafunzo haya haya ni swala mtambuka na limekuja kwa wakati muafaka ili kuweza kurahisisha utendaji kazi na utoaji wa vibali kwa wadau wa sekta ya mifugo, kuwapunguzia gharama za utoaji vibali lakini pia kurahisisha muda wa kuchakata hivyo vibali,


"Huu mfumo ni mzuri sana kwetu sisi wataalamu na watumiaji ambao ni wateja wetu kuhakikisha wote kwa pamoja tunalenga kuiweka wizara yetu ya mifugo na idara zake kuiweka katika hali nzuri" amesema Dkt. Msomi. 


Pia Dkt. msomi amesema mfumo huo utawezesha kufanya kazi kwa wakati na kuhakikisha yanafanyika vizuri ili kuwezesha kuongeza tija katika kuwaunganisha na wateja wa mataifa ya nje na masoko ya nje na kwa pamoja kuweza kuongeza pato la Nchi.

Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi (sekta ya mifugo) Bw. Baltazar Kibola akiwaelezea wadau wa sekta ya mifugo kanda ya ziwa na kanda ya Tabora, namna ya kutumia mfumo mpya wa kielektroniki wa usimamizi wa utoaji vibali mbalimbali  vya kusafirishia mifugo na mazao yake ndani na nje ya nchi uitwao Mifugo Integrated Management Information System ( MIMIS), wakati wa mafunzo ya mfumo huo  yaliyofanyika katika ukumbi wa Gold Crest Hotel, jijini Mwanza, 07 june 2022.

Watumishi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakiwa wanaongea na washiriki  wa mafunzo ya mfumo wa kieletroniki uitwao Mifugo Integrated Management Information System (MIMIS)  (nyakati tofauti) wakielezea aina ya vibali mbalimbali ambavyo vinatolewa katika idara zao ambapo vitakuja kutolewa katika mfumo huo. wakati wa mafunzo hayo yaliyotelewa kwenye ukumbi wa Gold Crest Hotel, jijini Mwanza, 07 june 2022.


Wawezeshaji kutoka Taasisi ya Trade Mark East Africa (TMEA) na Kampuni ya ICTPACK (waliosimama) wakijibu maswali kutoka kwa washiriki wa mafunzo ya mfumo wa kielektroniki wa usimamizi na utoaji wa vibali mbalimbali wa sekta ya Mifugo (MIMIS), Lengo ni kupata uelewa wa pamoja wa juu ya namna mfumo utakavyokwenda kuboresha mazingira ya ufanyaji wa biashara kwa sekta ya mifugo, mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Gold Crest Hotel, Jijini Mwanza 07 June 2022.

Sehemu ya washiriki wa mafunzo ya mfumo wa usimamizi wa utoaji vibali mbalimbali sekta ya Mifugo unaojulikana kama "Mifugo Integrated Management Information System " (MIMIS) wakifatilia mafunzo yaliyokuwa yakitolewa na mwezeshaji (hayupo pichani) ambapo mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Gold Crest Hotel Jijini Mwanza, 07 June 2022.


Mkuu wa kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi  (sekta ya Mifugo)  Bw. Baltazar Kibola (wapili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Washiriki waliohudhuria mafunzo ya usimamizi utoaji vibali mbalimbali sekta ya mifugo uitwao "Mifugo Integrated Management Information System" (MIMIS) wakiwa nje ya hotel ya Gold Crest, jijini Mwanza, mara baada ya kumaliza mafunzo hayo kwa siku hiyo, 07 june 2022.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni