Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili, 2022

KIKAO CHA MAFUNZO REJEA YA UFUGAJI SAMAKI KWA MAAFISA UGANI MJINI SONGEA

Picha
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Bw. Emmanuel Kisongo akifungua kikao cha mafunzo rejea ya ufugaji samaki kwa maafisa ugani (hawapo pichani) kutoka halmashauri za mikoa ya Mbeya, Songwe, Katavi, Kigoma na Ruvuma na kuwataka maafisa hao kuwa chachu ya kuhamasisha ufugaji samaki kwa wananchi. Mafunzo hayo yameandaliwa na Idara ya Ukuzaji Viumbe Maji kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na yanafanyika kwa siku nne Mjini Songea. (21.03.2022)*  Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah (kulia aliyekaa) akiwa pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. William Anangyise (wa pili kutoka kushoto aliyekaa) wakisaini mkataba wa Makubaliano ya Kujenga, Kuanzisha na Kusimamia Kituo cha Taifa cha Ukuzaji Viumbe Maji bahari kati ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam na Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa halfla fupi ya uwekaji saini mkataba huo iliyofanyika kwenye Shule Kuu ya Sayansi na Teknolojia ya Uvuvi - Kampasi ya Kunduchi Jijini Dar es Salaam. (22.03.20...

MWONGOZO WA CHAKULA BORA CHA SAMAKI NJIANI KULETA TIJA KWA WAFUGAJI*

Picha
  Na. Edward Kondela Serikali imesema imeandaa mwongozo wa uandaaji wa chakula bora cha samaki na kwamba itahakikisha mwongozo huo unafuatwa na watengenezaji wa chakula hicho ili kuleta tija kwa wafugaji wa samaki ambao wamekuwa wakipata changamoto ya kutopata chakula bora cha samaki hapa nchini. Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Viumbe Maji kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Nazael Madalla, amebainisha hayo (21.03.2022) Mjini Songea, katika Mkoa wa Ruvuma, kando ya mafunzo rejea kwa maafisa ugani kutoka halmashauri za mikoa ya Mbeya, Songwe, Katavi, Kigoma na Ruvuma ambao wamealikwa kwa ajili ya kujifunza na kukumbushwa njia bora za ufugaji samaki, ili kuhamasisha wananchi kufuga samaki. Dkt. Madalla amesema licha ya serikali kufanya juhudi mbalimbali zikiwemo za kuhakikisha upatikanaji wa vifaranga vingi vya samaki, kwa sasa serikali inaweka nguvu zaidi katika kuhakikisha vyakula bora vya samaki vinazalishwa hapa nchini ili kuwapunguzia gharama wafugaji wa samaki kwa kuwa...

WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI KUPOKEA MELI YA UVUVI YA WAWEKEZAJI JIJINI DAR ES SALAAM

Picha
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki (wa pili kushoto) akisalimiana na Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Suleiman Makame (wa pili kulia)baada ya kuwasili bandarini Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupokea meli ya Uvuvi ya Wawekezaji kutoka nchini Uhispania meli ambayo itakuwa inafanya kazi ya kuvua samaki katika bahari kuu. (21.03.2022)*    Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Suleiman Makame (kulia) akisalimiana na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Dkt. Christina Ishengoma (kushoto) wakati wakiwasili bandarini Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupokea meli ya Uvuvi ya Wawekezaji kutoka nchini Uhispania meli ambayo itakuwa inafanya kazi ya kuvua samaki katika bahari kuu. Katikati ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki. (21.03.2022)*  Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki (kulia) akimkabidhi Kibali cha kuvua nje ya mipaka ya Tanzania kwa Meneja wa Vyo...

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KILIMO MIFUGO NA MAJI WAKIKAGUA UJENZI WA BWAWA LA KUNYWESHEA MAJI MIFUGO CHALINZE

Picha
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki akitoa ufafanuzi kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji wakati ilipotembelea Kijiji cha Chamakweza wilayani Chalinze mkoa wa Pwani kukagua ujenzi wa Bwawa la kunyweshea Maji Mifugo. Kushoto ni Mhe. Dkt. Chistina Ishengoma ambaye ndio Mwenyekiti wa Kamati hiyo. (18.03.2022)*   Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki akiwa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Viongozi, Wataalam na Wafugaji wakati walipokuwa wanatembelea kukagua Bwawa la kunyweshea Maji Mifugo la Chamakweza wilayani Chalinze mkoa Pwani. (18.03.2022)*  Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Mhe. Dkt. Christina Ishengoma (wa pili kutoka kushoto) akijiridhisha kama maji yanatoka kwenye bomba wakati Kamati hiyo ilipofika kukagua ujenzi wa Bwawa la kunyweshea Maji Mifugo la Chamakweza wilayani Chalinze mkoa Pwani. Kulia ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki. (18.03.202...

NZUNDA AHIMIZA WELEDI, UWAJIBIKAJI*

Picha
  Na Mbaraka Kambona, Morogoro Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Bw. Tixon Nzunda amewataka Watumishi wa Wizara hiyo, Sekta ya Mifugo kufanya kazi kwa weledi, uadilifu, uwajibikaji na usikivu kwa umma ili waweze kutoka huduma bora kwa jamii. Nzunda alitoa wito huo alipokuwa akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi, Sekta ya Mifugo kilichofanyika Mkoani Morogoro Machi 18, 2022. Wakati akizungumza na Watendaji na Watumishi wa Wizara hiyo aliwataka kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake waimarishe uwajibikaji ili waweze kuwaletea  maendeleo wananchi. "Jukumu letu la kwanza ni kuhakikisha tunatoa huduma bora kwa umma kwa kiwango cha juu na zinazokidhi matarajio na matakwa ya wananchi", alisema Nzunda Pia, aliwataka wajiandae kufanya mabadiliko makubwa katika Sekta hiyo huku akiwahimiza kuja na mikakati ya kupata rasilimali fedha nje ya bajeti ya Serikali. "Ili tuweze kuleta mabadiliko hayo ni wajibu wetu kuwa wabunifu na kuwashirikisha Wada...

UMUHIMU WA USHIRIKIANO BAINA YA VIONGOZI WA WILAYA YA MULEBA NA WAVUVI MKOANI KAGERA

Picha
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Uvuvi Dkt. Rashid Tamatamah akifafanua kwa wajumbe (hawapo pichani) katika kikao kilichomhusisha pia Mkuu wa Wilaya ya Muleba na maafisa wafawidhi wa Kanda ndogo za Bukoba na Muleba pamoja na vikosi vya ulinzi na usalama katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Kagera, juu ya  umuhimu wa ushirikiano baina ya viongozi wa Wilaya ya Muleba na wavuvi  pamoja na kuhakikisha halmashauri ya wilaya hiyo inatoa vibali maeneo ya visiwani ili kuwaondolea kero wavuvi kusafiri mwendo mrefu kufuata vibali hivyo pamoja na wavuvi kuruhusiwa kuuza mazao ya uvuvi mahali popote nchini kwa kuzingatia sheria za nchi. (15.03.2022)*  Mkurugenzi wa Idara ya Uvuvi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Emmanuel Bulayi (aliyesimama) akifafanua vifungu mbalimbali vya Sheria ya Uvuvi, kwa wajumbe katika kilichofanyika kwenye Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Kagera, na kuwakutanisha Mkuu wa Wilaya ya Muleba na maafisa wafawidhi wa Kanda ndogo za Bukoba na Muleba pa...