Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki (wa pili kushoto)
akisalimiana na Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Suleiman
Makame (wa pili kulia)baada ya kuwasili bandarini Jijini Dar es Salaam kwa
ajili ya kupokea meli ya Uvuvi ya Wawekezaji kutoka nchini Uhispania meli
ambayo itakuwa inafanya kazi ya kuvua samaki katika bahari kuu.
(21.03.2022)*
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki
(kulia) akimkabidhi Kibali cha kuvua nje ya mipaka ya Tanzania kwa Meneja wa
Vyombo Vya Uvuvi vya Kampuni ya Albacora ya nchini Uhispania, Bw. Imanol Loinaz
mara baada ya kuwasili kwa meli ya PACIFIC STAR itakayokuwa inafanya kazi ya
uvuvi wa bahari kuu. Waziri Ndaki amekabidhi kibali hicho bandarini Jijini Dar
es Salaam. Katikati ni Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar, Mhe.
Suleiman Makame na kushoto ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega.
(21.03.2022)*
Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi, Mhe. Suleimani Makame (kulia)
akimkabidhi Leseni ya uvuvi wa bahari kuu kwa Meneja wa Vyombo Vya Uvuvi vya
Kampuni ya Albacora ya nchini Uhispania, Bw. Imanol Loinaz mara baada ya
kuwasili kwa meli ya PACIFIC STAR itakayokuwa inafanya kazi ya uvuvi wa bahari
kuu. Waziri Masoud amekabidhi kibali hicho bandarini Jijini Dar es Salaam.
Katikati ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki na kushoto ni Naibu
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega. (21.03.2022)*
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni