Hayo yamebainishwa Juni 02, 2021 na Afisa uvuvi mwandaizi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bw. Didas Mtambalike mara baada ya kutambulisha mradi huo katika warsha iliyofanyika kwa siku tatu Mkoani Dar es salaam.
Alisema lengo kuu la mradi huo ni kuimarisha usimazi wa uvuvi na mazingira katika ukanda wa pwani ya bahari ya Hindi ambapo matokeo yanayotarajiwa ni kuboresha usalama wa chakula na kupunguza umasikini kwa jamii duni hasa za pwani zinazotegemea uvuvi.
“mradi huu ni wa majaribio kwa miaka mitatu ambapo kwa nchi yetu unatekelezwa katika Wilaya ya Mkinga kuzingatia aina ya shughuli zinazofanywa katika eneo hilo sambamba na kuzingatia mazalia ya samaki na miti, hivyo tunatarajia wakazi wa pale watanufaika pakubwa baada ya mradi” alisema Mtambalike.
Kadharika amebainisha kuwa mradi huo pia unalenga katika kuwajengea uwezo wananchi juu ya sera ya uvuvi pamoja na namna ya kuandaa mpango kazi wa usimamizi wa rasilimali za uvuvi katika maeneo yao.
Alisema baada ya mradi huo Serikali itaondokana na dhana ya ufanyaji wa doria za mara kwa mara katika kudhibiti uvuvi haramu badala yake itatumika njia ya ulinzi shirikishi ambapo wananchi wenyewe wataweza kuwa kwenye mfumo mzuri wa udhibiti.
“tunataka kuondokana na ile dhana ya doria za mara kwa mara kukimbizana na wavuvi sasa hivi tunakuja na mfumo mzuri ambao ni shirikishi katika usimamizi na udhibiti lakini pia tumeangalia eneo la uendelezaji wa rasilimali kwamba wadau wetu waibue miradi midogo midogo ya kimaendeleo” alisema Mtambalike.
Mratibu wa Shirika la Chakula na Kilimo la
Umoja wa Mataifa (FAO) Tanzania, Dkt. Oliva Mkumbo akielezea lengo la warsha ya
kutambulisha mradi wa usimamizi wa rasilimali za Uvuvi bahari kwa Ukuaji wa
uchumi bahari na Utafiti wa awali wa mradi kwa washiriki waliohudhuria warsha
hiyo kwenye ukumbi wa TVLA Jijini Dar es Salaam. (02/06/2021)
Afisa Uvuvi mwandamizi
kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi ( Uvuvi), Bw. Tumaini Chambua akiwasilisha
mada kwenye washra ya kutambulisha mradi wa usimamizi wa rasilimali za Uvuvi
bahari kwa Ukuaji wa uchumi bahari na Utafiti wa awali wa mradi kwa washiriki (
hawapo pichani) waliohudhuria warsha hiyo kwenye ukumbi wa TVLA Jijini Dar es
Salaam. (02/06.2021)
Afisa Uvuvi mwandamizi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi ( Uvuvi), Bw. Didas Mtambalike akichangia hoja kwenye washra ya kutambulisha mradi wa usimamizi wa rasilimali za Uvuvi bahari kwa Ukuaji wa uchumi bahari na Utafiti wa awali wa mradi kwenye ukumbi wa TVLA Jijini Dar es Salaam. (02/06.2021)
Mratibu wa FAO Tanzania, Sekta ya Uvuvi, Dkt.
Oliva Mkumbo, ( wa pili kushoto mbele) akiwa kwenye picha ya pamoja na
washiriki wa warsha ya kutambulisha mradi wa usimamizi wa rasilimali za Uvuvi
bahari wa ukuaji wa uchumi bahari na Utafiti wa awali wa mradi kwenye ukumbi wa
TVLA Jijini Dar - es - salaam. (02/06/2021)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni