WANAWAKE WANAOJIHUSISHA NA UVUVI WATAKIWA KUWA WABUNIFU
Wanawake wanaojihusisha na shughuli za uvuvi wametakiwa kuwa wabunifu ikiwa ni pamoja na kujengeana uwezo Ili kukuza biashara zao huku wakikumbushwa kujilinda dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi. Ushauri huo umetolewa (24.06.2021) na Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Mara, Bi. Neema Ibamba katika warsha ya siku tatu ya wadau hao Mjini Musoma Mkoani Mara. Ibamba amesema kuwa biashara yoyote inahitaji ubunifu na kwamba wadau hao kutoka Mikoa ya Kanda ya ziwa lazima waende na wakati. Aliongeza kuwa ubunifu unaotakiwa ni pamoja na kuwa na vifungashio vizuri vya kisasa kwa ajili ya bidhaa zao pamoja na kuangalia fursa nyingine za masoko zinazowagusa. Aidha katika kukuza kipato cha familia, Ibamba amewataka wanawake kuendelea kushirikiana na waume zao badala ya kuwadharau kutokana na kipato wanachopata. "Biashara ama kupata kipato kisiwe kigezo cha kufanya dharau kwa wanaume wenu kwa kuwa mna pesa, hakikisheni kile mnachokipata m...