Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Desemba, 2020

VIWANDA KUONDOA UMASIKINI WA WAFUGAJI NA WAVUVI

Picha
Na. Edward Kondela   Serikali imesema itahakikisha sekta za mifugo na uvuvi zinawaondoa wananchi katika umasikini, kupata ajira na nchi iweze kuuza bidhaa bora za mazao ya mifugo na uvuvi ndani na nje ya nchi.   Akizungumza jana (28.12.2020) katika siku yake ya kwanza ya ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani mwanza, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki wakati akihitimisha ziara hiyo kwenye kiwanda cha kuchinja na kuchakata nyama cha Chobo kilichopo Kata ya Usagara Wilaya ya Misungwi amesema wizara imekuwa ikichukulia kwa uzito mkubwa suala la viwanda ambalo litaweza kubadilisha fikra za wafugaji na wavuvi.   “Wananchi wetu waondoe umasikini, wananchi wetu wapate ajira na sisi tuuze bidhaa za mazao haya ya mifugo na uvuvi yaliyo bora hapa ndani na kule kwa wenzetu nje, sasa mimi nikikuta hali ya mkwamo kwa kitu ambacho kinatusaidia kuelekea huko napata shida.” Amesema Mhe. Ndaki   Waziri Ndaki akifuatana na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. ...

SAUTI YETU WIKI HII

Picha
 

SALAAM ZA KRISMASI NA MWAKA MPYA

Picha
 

SALAAM ZA KRISMASI NA MWAKA MPYA

Picha
 

SALAAM ZA KRISMASI NA MWAKA MPYA

Picha
 

SERIKALI YASISITIZA MATUMIZI YA CHANJO ILI KUPATA MIFUGO BORA

Picha
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki amesema Tanzania ina chanjo za kutosha dhidi ya magonjwa ya mifugo na kuagiza wafugaji wote nchini pamoja na maeneo ambayo serikali inafuga kuhakikisha mifugo yao inachanjwa ili kuondokana na magonjwa hayo.   Akizungumza jana (24.12.2020) mara baada ya kutembelea Taasisi ya Chanjo Tanzania (TVI) iliyopo Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani, wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani humo, Waziri Ndaki amesema ili kuhakikisha Tanzania inakuwa na mifugo bora inayokidhi soko la kimataifa ni lazima mifugo ichanjwe dhidi ya magonjwa ili yapatikane mazao bora ya mifugo.   “Tunayo chanjo ya kutosha hivyo niwatake wafugaji wote ikiwa ni pamoja na sisi serikali kwenye maeneo ambayo tunafuga tuchanje mifugo yetu ili tupate mifugo iliyo bora, tunataka sasa nchi yetu iende kwenye ubora badala ya uwingi wa mifugo, ili tupate nyama bora na maziwa bora kwa maana ya mazao bora ya mifugo ili tuweze kuuza katika soko la kimataifa.” Amesema Mhe. Ndak...

GEKUL AWAAGIZA WAKURUGENZI HALMASHAURI KUTENGA FEDHA ZA MIFUGO

Picha
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kutekeleza Waraka wa mwaka 2002 ambao unawataka kutenga asilimia 15 ya mapato yanayotokana na shughuli za Sekta ya Mifugo na Uvuvi na kuzirejesha kwenye sekta hizo ili kuboresha shughuli zake.   Gekul alitoa agizo hilo alipokuwa akiongea na Viongozi wa Wilaya ya Mwanga, Mkoani Kilimanjaro alipotembelea kukagua shughuli za Sekta ya mifugo na uvuvi zinazotekelezwa Wilayani humo Disemba 23, 2020.   Kwa mujibu wa Gekul, mwaka 2002 Serikali ilitoa waraka ambao unaelekeza kuwa Halmashauri zote nchini zihakikishe kuwa mapato yanayopatikana kutokana na shughuli za sekta ya mifugo na uvuvi itengwe asilimia 15 na zirudishwe kwa sekta hizo ili kuboresha huduma kwa mifugo ikiwemo ukarabati wa majosho, minada na kununua chanjo za mifugo. “Wakurugenzi rejeeni huo waraka ambao unadumu mpaka mwaka 2025 ili mtekeleze kama ulivyoagiza na tukifanya hivyo itasaidia kuboresha huduma za mifugo ...

VIONGOZI WA KATA NA VIJIJI WAONYWA URAFIKI WAO NA WAFUGAJI

Picha
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki amewataka baadhi ya viongozi wa vijiji na kata wanaoshirikiana na wafugaji kuvunja sheria, taratibu na kanuni za nchi ili kuwanyanyasa wakulima katika maeneo yao kuacha mara moja kufanya hivyo kwani viongozi hao wanakuwa wanashiriki katika migogoro kwa kuchonganisha wakulima na wafugaji.   Akizungumza jana (22.12.2020) wilayani Liwale, kwenye kikao kilichoshirikisha wakulima na wafugaji wa Mkoa wa Lindi kwa ajili ya kutatua kero zao, Waziri Ndaki amekemea urafiki wa baadhi ya viongozi hao na wafugaji ambao umekuwa ukilenga kuwanyanyasa wakulima kutokana na wafugaji kuingiza mifugo kwenye maeneo ya wakulima hao.   “Wakati mwingine mnawapa tabu wakulima kwa sababu wafugaji wanashirikiana na hawa viongozi wetu wa ngazi za chini kufanya mambo yasiyotakiwa sasa tuache, watendaji wa vijiji na kata fuateni sheria, taratibu na kanuni mlizoelekezwa zinazopaswa kuwaelekeza katika kutenda kazi zenu.” Amesema Mhe. Ndaki   Aidh...

ZECO YAPEWA SIKU 14 KUKAMILISHA UKARABATI WA BWAWA LA KIMOKUWA

Picha
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel ameipa Kampuni ya ZECO yapewa siku 14 kukamilisha ukarabati wab wawa la Kimokuwa litakalotumika kwa ajili ya matumizi ya kunyweshea mifugo na matumizi ya binadamu.   Prof. Gabriel ametoa maelekezo hayo leo (22.12.2020) wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya ukarabati wa mradi huo unaotekelezwa katika kijiji cha Kimokuwa, wilayani Longido, mkoani Arusha.   “Mwanzoni kampuni hii ilianza kazi vizuri lakini mwishoni imekuwa na matatizo kwani usimamizi wao wa mradi sio mzuri kitu ambacho kimesababisha umaliziaji wa mradi kuwa na mapungufu,” alisema Prof. Gabriel.   Pia amemtaka mkandarasi kujiridhisha kwenye kingo za bwawa hilo walizoziweka kwani ikitokea zikabomoka hatua kali zitachukuliwa dhidi ya kampuni hiyo.   Kutokana na mapungufu aliyoyaona amempa mkandarasi siku 14 kuhakikisha anakamilisha mradi. Kutokana na kuwepo kwa mapungufu hayo, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe....

SERIKALI YAJA NA MFUMO SHIRIKISHI KUDHIBITI UVUVI HARAMU

Picha
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki amesema serikali itaandaa mfumo shirikishi na endelevu wa kudhibiti zaidi uvuvi haramu ambao utafanya mikoa na wilaya zishiriki kikamilifu katika kutokomeza uvuvi huo badala ya kuwa na operesheni za kutafuta wavuvi haramu.   Waziri Ndaki amebainisha hayo (21.12.2020) alipokuwa katika mkutano wa hadhara na wakazi wa Kijiji cha Mchinga Namba Mbili, kilichopo Wilaya ya Mchinga Mkoani Lindi wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani humo na kubainisha kuwa mfumo huo utasaidia serikali kuondokana na operesheni za za vipindi maalum na badala yake mfumo uwe unafanya kazi siku zote.   “Tuwe na mfumo endelevu wa kumaliza kabisa tatizo la uvuvi haramu kwa hiyo tutafanya hivyo badala ya kuwa na operesheni au zimamoto ya kutafuta wavuvi haramu tuwe na mfumo unaofanya kazi siku zote huku mikoani, wilayani na mahali pengine popote.” Amesema Mhe. Ndaki   Waziri Ndaki amewataka pia watu wanaojihusisha na wanaofikiria kujiingiza katik...

GEKUL AONYA WANAOJIHUSISHA UVUVI HARAMU, UKWEPAJI KODI

Picha
  Na Mbaraka Kambona, Manyara   Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul amewataka wale wote wanaojihusisha na uvuvi usiozingatia sheria na taratibu kuacha mara moja kwani Serikali haitakuwa na huruma kwa watakaokamatwa.   Gekul alitoa onyo hilo alipokuwa akiongea na Wavuvi wa Mkoa wa Manyara alipofanya ziara mkoani humo Disemba 21, 2020.   Kwa mujibu wa Waziri Gekul katika operesheni ya kupambana na uvuvi haramu iliyopita ilitumika karibu bilioni 1. 2 jambo ambalo alisema halivumiliki na hivyo aliwataka wavuvi kutoa ushirikiano kwa serikali ili kukomesha vitendo hivyo.   “Hatutavumilia jambo hili liendelee, Sisi kama Wizara tumesema ni lazima tupate muarobaini wa uvuvi haramu lakini na nyinyi wavuvi muwe tayari kutoa ushirikiano kwa serikali ili uvuvi haramu ukomeshwe mara moja,” alisema Gekul   Aliongeza kwa kusema kuwa uvuvi haramu ukikomeshwa itasaidia kuokoa mazalia ya samaki na kuongeza idadi ya samaki katika maziwa na maeneo men...