Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti, 2020

TAMATAMAH AFUNGUA MKUTANO WA WADAU KUHUSU MJADALA WA VIWANGO VYA MAZAO YA DAGAA NA MWANI

Picha
 Serikali imesema ipo katika mchakato wa kutengeneza viwango vya kitaifa vya ubora na usalama wa mazao ya Mwani na Dagaa ili kuyapa mazao hayo fursa pana ya masoko ya uhakika ndani na nje ya nchi. Hayo yalisemwa na Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Rashid Tamatamah alipokuwa akifungua mkutano wa Wadau kuhusu mjadala wa viwango vya mazao ya Dagaa na Mwani uliofanyika jijini Dar es Salaam Agosti 24, 2020. Dkt. Tamatamah alisema kuwa kutengenezwa na kuanzishwa kwa viwango vya kitaifa vya ubora na usalama wa mazao hayo ya uvuvi kutaimarisha na kukuza soko la kitaifa na kimataifa la bidhaa zinazotokana na mazao hayo ya uvuvi. “Mazao ya Dagaa na Mwani kwa muda mrefu yamekuwa hayana viwango vya ubora jambo ambalo limekuwa likifanya bidhaa hizo kutokutambulika katika soko la kimataifa ndio maana sasa serikali imeamua kutengeneza viwango vya ubora vya mazao ya uvuvi hasa Daagaa na Mwani ili yaweze kupata masoko yenye uhakika ndani na nje ya nchi,”alisema Dkt. Tamatamah Alisema ku...

ZIARA YA MAKATIBU WAKUU WILAYANI MAFIA.

Picha
  Kaimu Muhifadhi Mfawidhi, Hifadhi ya Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU), Bw. Amin Abdallah (kushoto) akisoma taarifa ya utekelezaji wa Majukumu ya taasisi hiyo kwa Makatibu Wakuu kutoka Wizara nne tofauti walipotembelea taasisi hiyo. Kulia ni Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah. (22.08.2020) Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah (kulia) akieleza jambo kwa Mkuu wa Wilaya ya Mafia, Bw. Shaib Nnunduma (kushoto) wakati wa kikao cha Makatibu Wakuu na Mkuu huyo wa Wilaya pamoja na kamati yake ya ulinzi na usalama ya Wilaya kilichofanyika katika Ofisi za Mkuu wa Wilaya. (22.08.2020) Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah (Kulia) akiongea na Watumishi wa Hifadhi ya Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) (hawapo pichani) alipotembelea Taasisi hiyo iliyopo katika eneo la Hifadhi ya Bahari ya Kisiwa cha Mafia. Kushoto ni Kaimu Muhifadhi Mfawidhi, Hifadhi ya Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU), Amin Abdallah. ...

TANZIA

Picha
 

TANGAZO KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI

Picha
 

KATIBU MKUU SEKTA YA UVUVI DKT. RASHID TAMATAMAH ATEMBELEA VIZIMBA VYA KUFUGIA SAMAKI :KONGWA FARM WILAYA YA MAGU MKOANI MWANZA.(09/08/2020)

Picha
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah (kulia) akifafanua jambo kwa mmiliki wa shamba la kufugia samaki linalojulikana kama "Konga Farm" Bi Loycana Mwidunda alipofika kwenye Vizimba vya shamba hilo vilivyopo Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza (09.08.2020). Mmiliki wa Shamba la Kufugia samaki linalojulikana kama "Konga Farm" Bi. Loycana Mwidunda (katikati) akitoa maelezo kuhusu Shamba lake kwa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah (kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Viumbe Maji Dkt. Nazaeli Madala (kulia) wakati wa ziara ya viongozi hao Wilayani Magu (09.08.2020)      Waliokaa mbele Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah (kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Viumbe Maji Dkt. Nazaeli Madala wakiwa kwenye boti kuelekea kwenye vizimba vya kufugia samaki vya Shamba la "Konga Farm" vilivyopo Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza (09.08.2020).

PICHA KILELE CHA MAONYESHO YA NANENANE MKOANI ARUSHA TAREHE 09/08/2020

Picha
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akikagua ng'ombe bora kwenye kilele cha maadhimisho ya maonyesho ya nanenane Mkoani Arusha (09/08/2020)    Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akipata maelezo kutoka kwa msambazaji wa madini ya Mifugo kutoka kampuni ya usambazaji wa madini (JOSERA), Bw. Elirehema Laizer alipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye kilele tea  maadhimisho ya maonyesho ya nanenane Mkoani Arusha (09/08/2020)  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akiangalia mashine ya kukatia nyama kwenye banda la SIDO alipotembelea kwenye kilele cha maadhimisho ya maonyesho ya nanenane Mkoani Arusha (09/08/2020)    Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akiongea na wananchi (hawapo pichani) kwenye maadhimisho ya kilele cha maonyesho ya nanenane Mkoani Arusha (09/08/2020)    Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. abdallah Ulega akimpongeza Bw. Anthony Fabian Mny...

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI, MHE. ABDALLAH ULEGA ATEMBELEA GEREZA LA KARANGA KUJIONEA UJENZI WA KIWANDA CHA BIDHAA ZA NGOZI (KILIMANJARO LEATHER INDUSTRIES CO. LTD

Picha
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akikagua ramani ya ujenzi wa kiwanda cha bidhaa za ngozi Kilimanjaro Leather Industries Co. Ltd kilichopo katika eneo la Gereza la Karanga Mkoani Kilimanjaro, ambapo ujenzi wa kiwanda hicho utagharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 60. Pembeni yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho Mhandisi Masoud Omary. (08.08.2020)  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kufika katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro akiwa na baadhi ya maafisa kutoka katika wizara hiyo na kukutana na mkuu wa mkoa huo Dkt. Anna Mghwira ambapo wamezungumza mambo mbalimbali ya kuboresha sekta ya mifugo na uvuvi kabla ya kuelekea katika Gereza la Karanga kujionea ujenzi wa kiwanda cha bidhaa za ngozi cha Kilimanjaro Leather Industries Co. Ltd. (08.08.2020)    Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akikagua baadhi ya mitambo itakayofungwa katika kiwanda cha bidhaa za ngozi cha Kiliman...

HABARI PICHA ZA MAONYESHO YA NANENANE KWENYE MIKOA YA SIMIYU, LINDI, ARUSHA, MBEYA, DODOMA, TAREHE 08/08/2020

Picha
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah (kushoto) akitoa maelezo kuhusu mradi wa "deep sea" kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (kulia) baada ya Waziri Mkuu kufika kwenye mabanda ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi muda mfupi uliopita kwenye Viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu (08.08.2020).    Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akitoa maelezo kuhusu teknolojia ya uhimilishaji kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (kulia) baada ya Waziri Mkuu kufika kwenye mabanda ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi muda mfupi uliopita kwenye Viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu (08.08.2020), Wa pili kutoka kulia ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina.    Kutoka Kulia Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel, Katibu Mkuu Wizara ya ...

HABARI PICHA ZA MAONYESHO YA NANENANE KWENYE MIKOA YA DODOMA NA ARUSHA, TAREHE 07/08/2020

Picha
Mgeni rasmi, Waziri wa Mambo ya ndani, Mhe. George Simbachawene akiangalia mbegu bora za malisho ya wanyama zinazozalishwa na Taasisi ya Utafiti wa Mifugo(TARILI) alipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea kwenye Viwanja vya Nzuguni, Kanda ya Kati, Dodoma Agosti 7, 2020.   Afisa Mauzo, Kampuni ya Inas, Hussein Juma(kulia) akimkaribisha Mgeni rasmi, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. George Simbachawene kuonja vipande vya Nyama   vilivyokaushwa na kutafunwa kama kichangamsha mdomo alipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea kwenye Viwanja vya Nzuguni, Kanda ya Kati, Dodoma Agosti 7, 2020.    Mkuu wa Kitengo cha Uhimilishaji, Kanda ya Kati, Idara ya Uzalishaji na Masoko, Denis Sichwale(Kulia) akitoa maelezo kuhusu Uhimilishaji kwa Mgeni rasmi, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. George Simbachawene alipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika Maonesho ya Nane Nane ...