Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Mei, 2020

"WATANZANIA TUNYWE MAZIWA YA HAPA NCHINI"-ULEGA

Picha
Watanzania wametakiwa kuwa wazalendo kwa kunywa maziwa yanayotengenezwa hapa nchini ili kuendeleza uchumi wa viwanda na Taifa kwa ujumla. Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega wakati akifungua maadhimisho ya 23 ya wiki ya maziwa   Mkoani Dodoma kwa njia ya kielectronic  "Ninaomba Sana na ninawasisitiza watanzania lazima tuwe na wivu wa maendeleo kwa ajili ya Taifa letu, lazima tuwe na uzalendo wa Taifa letu" Ulega Pia ameongezea na kusema kuwa Mhe. Raisi wetu Dr John Joseph Pombe Magufuli ametupa Ari kubwa Sana ya uzalendo kwa kupenda vya kwetu. Imeelezwa kuwa sekta ya Mifugo katika Pato la Taifa hapa nchini inachangia kwa asilimia saba (7%) huku asilimia thelathini (30%) ikitokana na sekta ndogo ya maziwa hivyo asilimia 1.2% ya Pato zima la Taifa inatokana na sekta ya maziwa. Mhe. Ulega amesema   Katika mwaka 2017/2018 kulikua na jumla ya viwanda (76,) lakini hivi Sasa tunajumla ya viwanda (99) kwa hivyo tunazidi...

MAAZIMIO YA MKUTANO WA MAWAZIRI WA KILIMO, USALAMA WA CHAKULA, KILIMO, MIFUGO NA UVUVI (SADC jijini Dsm, (22.05.2020)

Picha
* Mkutano umetoa miezi mitatu kwa kila mwanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kufanya tathmini ya madhara ya ugonjwa wa Covid - 19 katika sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi. * Mkutano umeweka mikakati ya usalama wa chakula na lishe katika ukanda wa SADC licha ya changamoto mbalimbali. * Mkutano umeazimia mikakati ya kulinda magonjwa yanayovuka mipaka yanayohusu mimea na wanyama na kuathiri kilimo na mifugo. * Mikakati imewekwa kutathmini namna wavuvi wanavyoathirika na ugonjwa wa Covid - 19. * Mikakati imewekwa kwa shughuli za uvuvi katika ukuzaji viumbe kwenye maji hususan kwa nchi zizisizokuwa na maji ya asili (maziwa, bahari na mito). * Mkutano umeweka mikakati ya nchi wanachama wa SADC kujilinda na ugonjwa wa covid - 19. Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina (Mb) ambaye pia Mwenyekiti wa Mawaziri wa Kilimo, Usalama wa Chakula, Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) (kulia), akiwa na...

WAFANYABIASHARA WATAKIWA KUTHAMINI SOKO LA NYAMA.

Picha
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amewataka wafanyabiashara wanaouza nyama nchini kutopandisha bei ya nyama kipindi hiki cha sikukuu ya Eid El Fitr  ili kuhakikisha kila mwananchi anapata kitoweo hicho. Akizungumza (18.05.2020) jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri Mhe.Ulega amemtaka pia Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Bw. Jumanne Shauri ndani ya siku saba kuhakikisha wanawapeleka wafanyabiashara wanaofanya biashara katika machinjio ya vingunguti kujionea eneo jipya lililotengewa na Manispaa ya ilala. Mhe. Ulega amebainisha hayo wakati akikagua ujenzi wa mradi wa machinjio ya kisasa katika eneo la vingunguti katika Manispaa ya Ilala, ambapo amesisitiza wafanyabiashara wa nyama wanapaswa kuuza nyama kwa bei ya kawaida kulingana na hali ilivyo ili kuhakikisha watu wote wanapata kitoweo hicho. Aidha amesema imekuwa ni kawaida kwa wafanyabiashara wa Nyama kupandisha bei kipindi cha sikukuu kinapofika hali inayosababisha  wananchi kutopa...

UKIFUGA KISASA HUWEZI KULALA NJAA. - MRUTTU

Picha
Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti na Mafunzo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Hassan Mruttu amesema wafugaji wakifuga kisasa kwa kunenepesha na kuvuna mifugo yao ni rahisi kupata masoko ndani na nje ya nchi kwani watu wengi wanategemea bidhaa za ng'ombe. Ameyasema hayo wakati akiongea na  wafugaji kwenye kijiji cha Nkerenge Wilaya ya  Misenyi Mkoani Kagera, (12/05/2020) Dkt. Mruttu amesema faida kuu za kufuga kwa mkakati ni pamoja na kupata masoko ya uhakika kutokana na  ng'ombe atakuwa akijiuza na sio kutafuta mnunuzi kwani  muonekano wake tuu utamvutia mnunuzi. " Biashara ya mifugo ni nzuri na inafaida sana kwani mfugaji hawezi kulala njaa hata siku moja, inamuwezesha mfugaji kuvuna, kuuza na kufanya mambo ya maendeleo." Amesema Dkt. Mruttu Aidha Mtafiti kutoka Taasisi ya Utafiti Tanzania (TALIRI) Bi. Neema Urassa amehimiza wafugaji kuendelea kuwekeza kwenye lishe bora ya ng'ombe na kufuga kwa kufuata kanuni bora za ufugaji ili kupata...

PROF. GABRIEL ATOA TAHADHARI YA CORONA KWA WAFANYAKAZI

Picha
Mwenyekiti wa baraza la Wafanyakazi Sekta ya Mifugo ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel, amewataka watumishi wa Sekta ya Mifugo kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya virusi vya corona kwa kufuata maagizo yanayotolewa na wataalamu wa afya huku wakiendelea kuchapa kazi kwa bidii. Akizungumza na wajumbe wa baraza la wafanyakazi kwenye kikao cha baraza la wafanyakazi kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya jiji la Dodoma leo,  Prof. Gabriel amesema 'Janga hili ni la kimataifa na kwa vyovyote vile mmesikia katika nchi mbalimbali." Amesema "Kwa niaba ya sekta ya mifugo wafugaji wote wa Ng'ombe zaidi ya milioni 32.5 na Mbuzi ambao wako zaidi ya milioni 20 na kondoo zaidi ya milion 5.5, kuku zaidi ya milion 79 kwa kweli tunamshukuru sana Dkt. John Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuchukua uamuzi mzito wa kutoipeleka nchi kwenye kufungiwa watu kukaa nyumbani (Lockdown). ...

WAFUGAJI WAELEZWA UMUHIMU WA UHIMILISHAJI.

Picha
Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti na Mafunzo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Hassan Ally Mruttu ameongoza zoezi la utoaji mafunzo ya umuhimu wa uhimilishaji na faida ya zoezi hilo kwa  wafugaji Mkoani Kagera. Akiongea wakati wa mafunzo elekezi ya uhamasishaji wa umuhimu wa uhimilishaji wa ng'ombe kwenye kijiji cha Kagenyi Wilaya ya Kyerwa Mkoani Kagera Jana (10/05/2020) Dkt. Hassan Mruttu amesema lengo la mafunzo hayo ni kutaka wafugaji kufuga kwa kuongezea thamani ng'ombe wao. "Ufugaji wa kisasa unawezesha mfugaji kupata ng'ombe wengi na bora wwnaokuwa kwa haraka na kutoa maziwa na nyama kwa wingi kuliko ng'ombe wasioboreshwa." Amesema Dkt. Mruttu. Aidha ametoa wito kwa wafugaji kusaidiana na kupeana taarifa za upandikizaji wa mbegu bora za ng'ombe (uhimilishaji) ili wafugaji wengi waweze kufikiwa na huduma hiyo. Naye mtafiti wa Mifugo, Bi. Neema Urassa kutoka Taasisi ya Utafiti wa Mifugo nchini (TALIRI) amewaelekeza  wafu...