Watanzania wametakiwa kuwa wazalendo kwa kunywa maziwa
yanayotengenezwa hapa nchini ili kuendeleza uchumi wa viwanda na Taifa kwa
ujumla.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah
Ulega wakati akifungua maadhimisho ya 23 ya wiki ya maziwa Mkoani Dodoma kwa njia ya kielectronic
"Ninaomba Sana na ninawasisitiza watanzania lazima tuwe na
wivu wa maendeleo kwa ajili ya Taifa letu, lazima tuwe na uzalendo wa Taifa
letu" Ulega
Pia ameongezea na kusema kuwa Mhe. Raisi wetu Dr John Joseph
Pombe Magufuli ametupa Ari kubwa Sana ya uzalendo kwa kupenda vya kwetu.
Imeelezwa kuwa sekta ya Mifugo katika Pato la Taifa hapa nchini
inachangia kwa asilimia saba (7%) huku asilimia thelathini (30%) ikitokana na
sekta ndogo ya maziwa hivyo asilimia 1.2% ya Pato zima la Taifa inatokana na
sekta ya maziwa.
Mhe. Ulega amesema Katika
mwaka 2017/2018 kulikua na jumla ya viwanda (76,) lakini hivi Sasa tunajumla ya
viwanda (99) kwa hivyo tunazidi ongezeko
la viwanda vidogo,vya Kati na vikubwa 20 katika Taifa letu.
Naye Kaimu msajili wa bodi ya maziwa Dr Sophia Mlote amesema
bodi ya maziwa imefanya jitihada kubwa kwa kushirikiana na mashirika mbalimbali
katika kuhakikisha tasnia ya maziwa inakua kwa kiasi kikubwa
Maadhimisho ya wiki ya maziwa yanakwenda sambamba na kauli mbiu
isemayo "wiki ya maziwa 2020 chagua viongozi Bora kwa maendeleo ya tasnia
ya maziwa"
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni