Kaimu Mkurugenzi wa
Utafiti na Mafunzo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Hassan Ally Mruttu
ameongoza zoezi la utoaji mafunzo ya umuhimu wa uhimilishaji na faida ya zoezi
hilo kwa wafugaji Mkoani Kagera.
Akiongea wakati wa
mafunzo elekezi ya uhamasishaji wa umuhimu wa uhimilishaji wa ng'ombe kwenye
kijiji cha Kagenyi Wilaya ya Kyerwa Mkoani Kagera Jana (10/05/2020) Dkt. Hassan
Mruttu amesema lengo la mafunzo hayo ni kutaka wafugaji kufuga kwa kuongezea
thamani ng'ombe wao.
"Ufugaji wa
kisasa unawezesha mfugaji kupata ng'ombe wengi na bora wwnaokuwa kwa haraka na
kutoa maziwa na nyama kwa wingi kuliko ng'ombe wasioboreshwa." Amesema
Dkt. Mruttu.
Aidha ametoa wito kwa
wafugaji kusaidiana na kupeana taarifa za upandikizaji wa mbegu bora za ng'ombe
(uhimilishaji) ili wafugaji wengi waweze kufikiwa na huduma hiyo.
Naye mtafiti wa
Mifugo, Bi. Neema Urassa kutoka Taasisi ya Utafiti wa Mifugo nchini (TALIRI)
amewaelekeza wafugaji kuwa pamoja na uhimilishaji wa ng'ombe kwa kutumia
mbegu za ng'ombe walioboreshwa ni muhimu wafugaji kubadili mtizamo na
kukubali kufuga kibiashara na kuzingatia uvunaji wa ng'ombe kwa msimu
unaofaa.
Aliongeza kuwa
uzalishaji wa ng'ombe bora na bidhaa zake utachangia katika kukidhi mahitaji ya
lishe bora ya kaya na upatikanaji wa malighafi za viwanda.
Kwa upande wake afisa
mifugo wa Wilaya ya kyerwa Mkoani Kagera Bw. Fred Kija amewasihi wafugaji
kuendelea kupeana taarifa za uhimilishaji ili kusaidia wafugaji wengi kuweza
kufikiwa na kupata huduma iyo
Hata hivyo mwenyekiti
wa wafugaji kijiji cha Kaitambuzi Bw. Charles Bwanakunu ameelezea changamoto
wanazozipata ikiwa ni pamoja na serikali ya kijiji kuchukua ardhi yao na
kumuomba Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina na serikali
kwa ujumla kuwasaidia kutatua changamoto hiyo ili wafugaji wa kyerwa waweze
kupata haki yao na kufanya kazi zao bila usumbufu.
Aidha ameishukuru
serikali kwa kuweza kuona umuhimu wao kama wafugaji na kuwafikia kwa
kuwapa elimu ya ufugaji wa kisasa, uhimilishaji, kuvuna na kufuga kibiashara na
kuahidi kufanya kazi maarifa hayo yaliyoyapa.
Watafiti kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi
wakiangalia mifugo iliyotengwa kwa ajili ya zoezi la uhimilishaji kwenye
shamba la KMC LTD wilayani Kyerwa Mkoani Kagera. (10/05/2020)
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni