Chama cha wanawake wataalamu kutoka Wizara ya Kilimo,Mifugo,Uvuvi na Mazingira, Tanzania association of women leaders in agriculture and environment ( TAWLAE) leo wamefungua rasimi mkutano wa mwaka wa 21 na kuhudhuriwa na Naibu katibu Mkuu Bi Butamo Philipo kwa niaba ya waziri wa Mazingira Mhe. January Makamba ambao umefanyika leo katika viwanja vya wizara ya mifugo na uvuvi.
Akiongea katika mkutano huo wenyekiti ya chama cha wanawake viongozi katika kilimo na mazingira Dkt. Sofia Malote amesema Lengo kubwa la mkutano huo ni kuunganisha wakulima na tafiti mbalimbali zilizoandaliwa na wataalamu hao
"Maadhimisho ambayo yamebeba kaulimbiu isemayo uchumi wa viwanda Tanzania wanawake tupo tayari,hapa ni kazi tu".
Aidha Dkt. Sofia Malote amesema kazi ya TAWLAE ni
kuwaunganisha wakulima wadogo au wakubwa na tafiti mbalimbali ambaozo zimetafitiwa hapa nchini ili kuongeza uwekezaji na ajira kwa
watanzania katika kilimo.Akizungumza katika
wasilisho lake Dkt.Malote amesema kilimo kilikuwa na faida ndogo kwa sababu utalaam,teknolojia
na juhudi zilikuwa bado hazijatumika vizuri katika kilimo.
Ili kuingia katika uchumi wa viwanda ni lazima uzalishaji wa kilimo uwe na tija uwepo na uboreshaji wa masoko na
teknolojia ambapo wataalamu wanawake ndio wanajukumu kubwa katika kuleta
mapinduzi ya kilimo alisema Dkt.Malote
wanawake wakimkaribisha mgeni rasmi |
Mgeni rasmi Bi. Butamo Philipo akitoa maelezo machache kwa wanawake wa TAWLAE |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni