Nav bar

Ijumaa, 28 Oktoba 2016

MELI ZA UVUVI KATIKA BAHARI KUU KUTOKA CHINA ZATIA NANGA ZANZIBAR KWA MARA YA KWANZA TAREHE 27/10/2016



Meli  mbilii za Uvuvi katika bahari kuu Tao Hang 1 na Tao Hang 7 zimetia nanga katika bandari ya Zanzibar kwa  mara ya kwanza kwa Madhumuni ya kukaguliwa na kushusha shehena ya samaki ambao hawawahitaji  (Bycatch).

Meli hizi mbili baada ya kuwasili wataalam wa Uvuvi kutoka mamlaka ya Uvuvi katika bahari kuu walienda kuikagua iwapo inakidhi vigezo vya Uvuvi katika bahari kuu na kuzipatia leseni ya Uvuvi hapa kwetu.

Baada ya ukaguzi meli hizi zilionekana kukidhi matwakwa yaliyokuwa yanahitajika na zilipewa leseni ya kuvua katika bahari kuu. Aidha samaki ambao walivuliwa kwa bahati mbaya na ambao wao hawawahitaji walishushwa na kuuzwa kwa wananchi mjini Zanzibar.
Mojawapo la sharti ya kupewa leseni ni kuleta samaki hao na kuwauzia wananchi katika nchi husika
Hivi karibuni serikali ilisimamisha utoaji wa leseni hizi na  kuzifanyia maboresho ili serikali iweze kufaidika zaidi kutokana na Uvuvi katika bahari kuu. Maboresho hayo yamefanyika na utoaji leseni umeanza kama ilivyopangwa


Moja kati ya meli za Uvuvi Tai Hong No 1 ikionekana kwa karibu ikiwa imetia nanga
Mkaguzi kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Uvuvi katika Bahari Kuu Bw. Zouwa akisalimiana na Captain wa meli hiyo baada ya kuingia ndani ya meli
Moja kati ya mitego ya kuvulia samaki zinazoitwa radio boya zikikaguliwa
Mkaguzi akiendelea kukagua floating boya zinazotumika katika kuvua samaki
Chumba cha kuhifadhia samaki (cold room area temperature minus 60)
Mitego ya kukamatia samaki
Mashine mbalimbali zinazosaidia kusukuma meli
Wafanyakazi wa meli hiyo wakifungua sehemu ya kuhifadhia samaki ili wakaguzi waweze kuona samaki waliopo


Mmoja kati ya wamiliki wa meli hiyo ya TAI HONG akizungumza na waandishi wa habari akishukuru kwa kuwa na taratibu hizo na kuipongeza serikali kwa hatua nzuri

Muonekano wa meli ya TAI HONG NO 1 ikiwa imetia nanga

Maoni 1 :

  1. iko vizuri rasilimali hizi zinatakiwa kunufaisha nchi na watu wake

    JibuFuta